Calvary Christian Centretunduma TAG

Calvary Christian Centretunduma TAG

Comments

Mungu akuongoze ktk hilo na UBARIKIWE sana

Calvary Christian centretunduma TAG. Is a spiritual institution focused to draw people to love of GOD. We teach the word of God in all truth. We are located in Tunduma township along Sumbawanga road..

[06/28/19]   Bwana Yesu asifiwe. Tunawakaribisha katika ibada ya sikukuu ya watoto ambayo itafanyika siku ya Juma pili kuanzia SAA mbili kamili asubuhi hadi SAA sits Na nusu mchana. Usipange kukosa mambo mazuri kutoka Kwa watoto wanao mjua Mungu hapa Calvary.

[06/26/18]   Ukiondoa ufahamu hakuna kitu chenye maana.

"Usitupe dhahabu mbele ya nguruwe, wasije wakageuka wakakurarua".

Katika maandishi mengi ya mfalme Suleman utaona kuna kujirudia sana kwa maneno ufahamu, upumbavu, hekima, ujinga, maarifa, busara na mengine mengi ya aina hii, lakini kuna wakati anamtaja nguruwe kuwasilisha wasifu wa upumbavu au ujinga. Haishi hapo anaendelea zaidi kufanya ulinganifu wa thamani kati ya ufahamu na mali (Dhahabu) na anaishia kuchagua ufahamu badala ya dhahabu.

Ilitokea wakati fulani rafiki yangu mmoja alikuwa akitembea kutokea nyumbani kuelekea katika eneo lake la kazi, kulikuwa na watu wengine pia aliokuwa ameandamana nao. Wale waliokuwa wamemtangulia walipita karibu na kitabu kilichokuwa chini barabarani, anaeleza kuwa walikiona na walikipita, anaeleza zaidi kuwa kuna mmoja alienda mbele zaidi alikipiga teke kwa maana ya kuwa kili mpa kero.

Baada ya kufika lile eneo aliinama na kuanza kukitazama kile kitabu. Kilikuwa ni kitabu ambacho amewahi kusikia habari zake lakini hakuwahi kukinunua, kile kitabu kinaitwa Success Strategy cha Mwandishi Oyedepo.

Anaeleza baada ya kukipekua, kilikuwa na kurasa zake zote na bado kilikuwa na stika ya bei usoni pake. Alikifuta vumbi na kukiweka katika mfuko wake kwa furaha sana.

Wakati wote akifanya hivi, watu walikuwa wakimshangaa. Inakuwaje huyu jamaa anafanya hivi!? Inawezekana kabisa kuna watu waliokuwa wanamuona kama punguani lakini yeye alijua ni nini amekipata. Katika muktadha huo lile andiko la Sulemani linatimia "Pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe".

Wakati watu wakimshangaa yeye pia alikuwa akishangaa, inakuwaje mtu anashindwa kuona kitu cha thamani kiasi hicho? Watu wapo bize kutafuta maisha huku wakikanyaga maarifa chini ambayo yangewasaidia kurahisisha maisha yao badala ya mapambano yenye matunda kidogo kila siku?

Ukweli ni kuwa kabla haujaelewa na kufunguka ufahamu wako hakuna chochote chenye thamani. Unakumbuka kile kisa cha babu zetu kubadilishana almas na vipande vya vioo, tofauti ni ufahamu tu.

Kitu ambacho hauna ufahamu nacho hakiwezi kuwa na thamani kwako, ndio maana badala ya kukaa katika mabishano (mara nyingi yanachagizwa na ujinga) tafuta kufahamu somo hilo inawezekana usiwe na sababu ya kufanya hivyo.

Baba yangu aliwahi kuniambia "usibishane na mtu kwa vile alivyo, kuna kitu anakipata kwa kuwa vile alivyo" ukitaka kumsaidia anza kuelewa kwanza kwa nini na anafaidika na nini kwa kuwa vile alivyo.

Kuna jambo ambalo inawezekana usione kama vina maana leo lakini baada ya kupata ufahamu juu ya hilo ukaona thamani ya hicho kitu. Kuna watu ambao wanatengeneza mikoba kwa kutumia mifuko ya majani ya chai na wanauza Kwa bei nzuri kwa watalii, wewe unafanya nini na mifuko hiyo? Kama ufahamu wako ukiweza kubadilika inawezekana kabisa utaanza kuona kila kitu ulichonacho kina thamani kiasi gani.

Ongeza ufahamu wako, kuona thamani ya vitu vinavyokuzunguka.

Ushindi Ellioth M.O.D

[06/02/18]   Bwana Yesu kristo asifiwe. Tunawakaribisheni watu Wa rika zote kwenye ibada ya kesho Siku ya juma pili. Ibada ya kwanza itaanza SAA moja Na kuisha SAA 9:30, ya pili itaanza SAA NNE kamili hadi SAA 12:30 pm. Njooni tumwabudu Bwana tumwambie matendo yake yanatisha kama nini..

[01/01/18]   Heri ya mwaka mpya. Uwe mwaka wa baraka na mafanikio makubwa sana kwako na familia yako.

[11/16/17]   Roho mtakatifu ni zaidi ya kila kitu. Anatuonesha na kutufundisha yote. Pasipo Roho mtakatifu ni ngumu kumpendeza Mungu.

Calvary Christian Centretunduma TAG

Yesu asifiwe watu wa Mungu.

Mungu wetu mkuu amezidi kuwa mwema sana. Ninawashukuru na kuwaombea kila mara lakini zaidi ninatiwa moyo Kila ninaposikia juu ya kujitoa kwenu kwa kazi ya Mungu. Mwe na nia hiyo hiyo katika Kristo maana ina ujira mwema.

Nina mambo mengi ya kufurahi na kujivuna kwa ajili yenu. Hata mara baada ya kuwa na wajenzi wengi lakini nyinyi mnabaki kuwa msingi kwa hapa ambapo leo nimefika.

Baada ya kutokuonana muda mrefu, ninajiandaa kurudi nyumbani sasa sio kama nilivyoondoka lakini hasa kwa ajili ya kuonesha matunda kwa ile mbegu na mbolea ambayo mliitia katika kunikuza.

Kitabu hiki ni zao la mafundisho yenu, Maombi yenu na ushauri wenu. Ile mbegu mliyopanda haikupandwa katika mwamba bali katika udongo na imeweza kuzaa.

Ni heshima yangu basi, kuweka wakfu kazi hii kwa familia yangu ya Calvary Christian Center...

Ninarudi nyumbani, nimekumbuka nyumbani, nimekumbuka siku zile nilopoitwa mtoto...

Ninarudi na kitabu hiki mkononi, baraka kwa ulimwengu na ufalme wa Mungu. Zao la ile mbegu njema mliipanda ndani yangu...

[08/14/17]   Tunayaweza yote ktk yeye atutiae nguvu.
Hivyo tutashinda na zaidi ya kushinda Kwa kuwa tunaye aliye Mkuu Yesu

DON MOEN (Praise & Worship Leader)

"See our hearts and remove anything that is standing in the way of coming to You today..." Make this your prayer today!

Leo ni Siku ambayo haitasahaulika kihistoria jimboni Songwe, kwani wanawake Wa Jimbo walikuwa wanaiweka rasmi au wakfu idara hii katika Jimbo LA Songwe. Mgeni Rasmi katika hafla hii alikuwa ni Askofu Wa Jimbo LA Songwe Rev Eliud amosi Kalinga. Sherehe ilifana sana na katika yote tunamrudishia Mungu utukufu.

CMF sikukuu

[05/06/17]   Wale wasikilizaji Wa Redio ushindi kesho ibada hii itarushwa redioni. Kuanzia asubuhi hadi mchana. Mungu akujalie Neema uamke salama na tukajae utukufu mwingine Siku ya kesho

[05/06/17]   Haleluya ndugu zangu wote ktk Bwana. Tunawakaribisheni nyote ktk ibada ya Siku ya kesho tar 07/05/2017 ili tuhitimishe Kwa pamoja sikukuu ya wanaume(CMF) njoo upate na ushuhuda Wa mwanaume aliyeoa jini mahali hapa, lakini pia usikilize mahubiri ya mchungaji Yohana Msigala. Yupo pia muimbaji Amwembe mwasongwe. Karibu ili Mungu atuhudumie sote .

[04/07/17]   Yesu pekee anaweza, muamini mambo yako yatakuwa salama. Aliteswa na kusulubiwa kwa ajili yetu hivyo tutashinda na zaidi ya kushinda kwakuwa yeye alishinda. Tumtazame yeye aliyepigiliwa pale msalabani.

[12/09/16]   Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu wote. Mnakaribishwa katika semina ya neno LA Mungu inayofundishwa na Mtumishi Wa Mungu kutoka Arusha. Karibu uhudumiwe na Mungu kupitia Mtumishi huyu.

[11/19/16]   Bwana Yesu apewe sifa ndugu zangu. Niwakaribishe ktk ibada ya kesho Siku ya j pili itakayo anza asubuhi SAA mbili kamili hadi SAA sita na nusu mchana. Nyote mnakaribishwa ili tumwabudu na kumsifu Mungu kwa pamoja. Usiku mwema

[10/23/16]   Karibuni katika ibada ya Leo jumapili inayoanza SAA mbili kamili asubuhi kwa maombi had I SAA tatu, kuanzia SAA tatu kamili had I SAA NNE kamili in ibada ya kingereza na kuanzia SAA NNE kamili had I SAA sita na nusu ni ibada kuu.. Karibuni tumsifu na tumwabudu Bwana kwa pamoja.

Asante Mungu kwa kutupatia mch Eliud Amosi Kalinga kama na kuendelea na nafasi yake ya uaskofu ktk jimbo la kusini magharibi. Lkn pia askofu mkuu ni yuleyule. Barnabas Mtokambali.

[07/04/16]   Habari ndugu!
Ili ufanikiwe unahitajika kuvunja maagano yote ya giza ambayo unayajua ama kuto yajua kwani ndio yanayokufanya ushindwe kuendelea mbele. Kataa kuwa na mtazamo wa kikale wa kukili kuwa kwenu nyie ni wa hali fulani na kuridhika na hali uliyonayo.
Anza sasa kukili ushindi kama daudi alivyokili ushindi hatimaye akamuuwa goliathi. Mungu atubariki sote.

[05/28/16]   Yesu asifiwe wapendwa! Tunamshukuru Mungu muweza wa yote kwani tuhai hata leo! Basi nichukue nafasi hii kuwakaribisha kesho katika ibada ambayo itaanza mnamo saa tatu kamili asubuhi ikiwa ni ibada ya kingereza inayoishia saa nne asubuhi, na baada ya hapo ni ibada ya kawaida ambayo itaanza saa nne hadi saa sita na nusu mchana. Ni maeneo ya Transformer uliza kanisa la ghorofani T.A.G hutapotea kabisa. Ubarikiwe na karibu sana.

[04/17/16]   Leo ni siku njema Bwana ameifanya, twendeni nyuani mwake na tumpe sifa. J pili njema

[04/04/16]   Haleluya wapendwa. Siku ya kesho katika kanisa letu lililop Hapa Tunduma maeneo ya mwaka -Transformer kuna semina nzuri ya neno la Mungu. Fika uhudumiwe na Mungu kwa viwango vya tofauti. Karibu sana.

[03/20/16]   Tunamshukuru Mungu kwa ibada ya leo. Tumehudumiwa vizuri na mch wetu wa kanisa E. Kalinga.
Ujumbe wa leo ni kwa habari kutokuwa wasaliti au Yuda na kusababisha mambo ya Mungu kukwama. Tumekatazwa kuwa wazinzi, wachawi na kama kunawatu wanatenda hayo ni wasaliti kama yuda maana wanafanya kinyume na neno la Mungu. Kufanya sawa na neno husababisha baraka tele.
Mubarikiwe nyote.

[03/01/16]   It is a new week God has given us. welcome all to our church there Is a seminar for the whole week from yesterday up to sunday this week. Wanawake wa kanisa hili wameandaa semina nzuri kwa kuwaarika watumishi mbalimbali ambao watatupa mafundisho mazuri. Njoo wew mualike na yule tuhudumiwe na Mungu.

[02/29/16]   Tumtumikie Mungu maadam ni mchana, maana usiku waja ambapo hatutaweza kufanya kazi.

[11/06/14]   CURRENT NEWS:
JEHOVA NISS CHOIR HAS RECENTLY INAUGURATED THEIR SECOND GOSPEL MUSIC ALBUM GOES BY NAME "BADO UNALIA?" THIS COMES AFTER THEIR FIRST ANNOINTED ALBUM GONE BY NAME "USILIE,NYAMAZA". THE FIRST WAS GOOD, THE SECOND BETTER, THE COMING WILL BE THE BEST,EXCELLENT, BRAVO............TILL ALL GLORY. CONGS JEHOVA NISS. DONT MISS THE COPY FOUND IN DVD AND AUDIO CD.

[10/30/13]   CURRENT NEWS:
MEN'S CHRISTIAN FELLOWSHIP (CMF) HAVE STARTED THEIR WEEK THAT WILL EXTEND TO SUNDAY. MEN CONDUCTS SEMINAR FOR ALL CHURCH. YOUR INVITED TO ATTEND AND SHARE WHAT GOD HAS PREPARED FOR YOU THROUGH MEN. DONT MISS.

Untitled Album

Untitled Album

Calvary Christian Centretunduma TAG's cover photo

[10/21/13]   God created you number one, don't accept number two.

[10/19/13]   WELCOME ALL PEOPLES WHO LOVE GOD.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Tunduma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


Left Side Along Sumbawanga Road Majengo Mapya Near Mwaka Area
Tunduma
Other Religious Organizations in Tunduma (show all)
Shalom International Ministries - Tunduma Shalom International Ministries - Tunduma
BOX 136 TUNDUMA
Tunduma, +255

Shalom International Ministries Tunduma Shalom International Ministries Tunduma
P.O.BOX 8
Tunduma, +255

KWAAJILI YA KUIUBILI INJILI YA YESU KRISTO NA MATENDO YAKE