LIFE Givers Ministries International

LIFE Givers Ministries International

Comments

Bwana Yesu Asifiweee.Mm Nauliza Yesu Ktk Wanafunzi Wake Hakuweka Wanawake Mbona Siku Hizi Wanaweka Wazee wa Kanisa Wanawake Hata Wachungaji Wapo Wanawake ?

Our vision is to win the lost souls back to Christ and prepare the church for the rapture.

Operating as usual

Tukiwa na Rosi Muhando " Mwanamke usilie tena "

fireee

Life Givers Ministry Mwanza

Timeline Photos

[12/06/16]   '' TUMIA ULICHONACHO KUPATA UNACHOTAKA''
Katika kitabu cha 2 Wafalme 4:1-7 ni habari ya mwanamke mjane ambaye watoto wake wawili walitaka kuchukuliwa kuwa watumwa kwasababu ya deni ambalo mama yao hakuweza kulilipa.
Inavyoonekana deni lilikuwa ni kubwa sana ndio maana mdai alithaminisha hilo deni kwa kutaka kuchukua hao vijana wawili wa mama mjane ili wafidie deni hilo.
Mwanamke huyo mjane hakukubali watoto wake wachukuliwe kuwa watumwa, alichukua hatua ya kwenda kwa nabii Elisha kumweleza changamoto hiyo. Nabii Elisha akamuuliza mama mjane ''NIKUFANYIE NINI? NIAMBIE UNA KITU GANI NYUMBANI? naye mwanamke mjane akamjibu nabii Elisha kuwa '' MIMI MJAKAZI WAKO SINA KITU NYUMBANI, ILA CHUPA YA MAFUTA"
Nabii Elisha akamwambia akaombe vyombo vitupu huko nje kwa majirani zake wote, tena vyombo vingi, kisha aingie ndani ajifungie na watoto wake na akavimiminie mafuta vile vyombo.
Mwanamke huyu alifanya kama nabii Elisha alivyomwagiza, alivimiminia vile vyombo mafuta kupitia kale kachupa kadogo navyo vikajaa vyote kisiwepo hata chombo kimoja kilichokosa mafuta, naye mwanamke mjane akayauza yale mafuta na kulipia lile deni na watoto wake wakawa salama.

NINI MAANA YA UJUMBE HUU?
Kila binadamu amepewa kitu cha ki mungu ndani yake mbacho anatakiwa kukitumia ili afike mahali ambapo Mungu amemkusudi afike. Mwanamke mjane alikuwa hana kitu zaidi ya ile chupa ndogo ya mafuta ambayo hakika ilimtoa kwenye umaskini, WEWE UNANINI? Inawezekana una elimu ambayo wewe unaiona ni ndogo, inawezekana una hela ambayo unaona ni ndogo sana, inawezekana una kipaji labda cha kuimba au kipaji chochote cha kutumia mikono yako kutengeneza vitu vya ubunifu, inawezekana pia una kitu lakini hukioni au hujui ukitumieje ili kikuondoe sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine,'' MUNGU AKUPE NEEMA YA KUJUA UNA KITU GANI KITAKACHOKUSAIDIA KUBADILISHA MAISHA YAKO''.
Lakini nakusihi leo, WAKATI WATU WANALALAMIKA UCHUMI NI MBAYA BASI WEWE TUMIA ULICHONACHO KUPATA UNACHOTAKA. Hata kama ni talent ndogo tu au skills ndogo tu, au knowledge ndogo tu, ila tumia hichohicho kidogo ulichonacho ili ufike mahali pa juu sana ambapo ndipo Mungu alipokukusudia. Usikae chini na kulia hali ni ngumu, fanya kwa bidii kile kitu ambacho Mungu amekupa, na kumbuka Mungu hawezi kuubariki mkono mlegevu, fanya kwa bidii na hakika utauona mkono wa Mungu. Mimi sijui Mungu amekupa nini ninachojua ni kwamba kila mtu amepewa kitu na Mungu ambacho ukikitambua na kukifanyia kazi basi kitakutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine.
''NI MAOMBI YANGU KWAMBA KAMA MAMA MJANE ALIVYOTUMIA KICHUPA KIDOGO KUTOKA KATIKA UMASKINI, NA WEWE PIA MUNGU AKUPE NEEMA YA KUTAMBUA KICHUPA CHAKO KIDOGO NA KIKUONDOE KWENYE HALI NGUMU UNAYOPITIA''
''BARIKIWA NA BWANA''

Untitled Album

NGUVU YA ROHO MTAKATIFU

NGUVU YA ROHO MTAKATIFU

Untitled Album

PASTOR Godfrey Fungo AKIWEKA WAKFU NA KUTOA VYETI VYA UONGOZI KWA VIONGOZI WA HUDUMA YA LIFE GIVERS." VIONGOZI WAMEAPA KUMTUMIKIA MUNGU NA KUTOMUASI MTUMISHI WAKE.

PASTOR Godfrey Fungo AKIWEKA WAKFU NA KUTOA VYETI VYA UONGOZI KWA VIONGOZI WA HUDUMA YA LIFE GIVERS." VIONGOZI WAMEAPA KUMTUMIKIA MUNGU NA KUTOMUASI MTUMISHI WAKE.

Untitled Album

ZAIDI YA WATU SABINI WAMEFUNDISHWA NENO LA MUNGU NA KUBATIZWA

ZAIDI YA WATU SABINI WAMEFUNDISHWA NENO LA MUNGU NA KUBATIZWA

Untitled Album

KONGAMANO LA KUPOKEA BARAKA

KONGAMANO LA KUPOKEA BARAKA

Pastor Godfrey Fungo delivering a woman possessed with evil spirits.

Pastor Godfrey Fungo akimfungua mwanamke aliyefungwa na nguvu za giza, nyota yake ilikuwa imeibiwa kichawi na ametolewa kafara na mume wake kwa miaka kumi na mitano. Mwanamke huyu alikuwa amefungwa uchumi wake, kila alichokifanya alikuwa hafanikiwi. Huwenda na wewe kuna biashara unayofanya ama kazi yoyote unayofanya lakini kwa muda mrefu haufanikiwi, napenda kukutia moyo kwamba Mungu anaweza kukuondolea shida hiyo, karibu kanisani ujue ni nini chanzo cha matatizo hayo yanayokupata na ukawekwe huru. Barikiwa.

UBATIZO WA MAJI MENGI
Kwa mkristo, ili kutimiza haki yote ni lazima ubatizwe kwa maji mengi kama BWANA wetu Yesu kristo alivyobatizwa na Yohana mbatizaji kwenye mto Yordan. YOHANA 3:23

KESHO JUMAPILI TAREHE 6/11/2016 KUTAKUWA NA UBATIZO WA MAJI MENGI NA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU KWA WALIOOKOKA KWENYE KONGAMANO NA WENGINE WOTE AMBAO BADO HAWAJABATIZWA KWA MAJI MENGI. Usikubali neema hiyo ikupite, mahali ni katika hema ya mguso Ilemela kanisani barabara ya kuelekea airport Mwanza, kituo kinaitwa Kanisani. KWA MAWASILIANO PIGA 0755211061. BARIKIWA!

HAPPY BIRTHDAY MBEBA MAONO, Apostle Godfrey Fungo "THE DISTINCT"

SIRI YA KANISA LENYE MADHABAHU YA KICHAWI MWANZA YAFUCHUKA!
Mungu anamtumia Mchungaji Godfrey Fungo kumfungua dada ambaye alikuwa akiabudu kwenye kanisa lenye madhabahu ya kichawi jijini Mwanza; Mapepo yametoa siri za jinsi mchungaji huyo anavyowatoa washirika wake sadaka kwa mapepo ili wanywe damu. Mapepo yamemwekea dada huyo alama mguuni. Angalia video hii...

Pastor Godfrey Fungo akishughulikia vyanzo vya matatizo ya muda mrefu katika ibada ya Jumapili iliyofanyika kanisani kwake Life Givers prayer Centre, Ilemela, Mwanza, barabara ya kuelekea Airport, Kituo cha daladala cha Kanisani.

Pastor Godfrey Fungo delivering a woman who was initiated to Idols. (Mchungaji Godfrey Fungo akimfungua mwanamke aliyekuwa ametolewa sadaka kwenye madhabahu ya kichawi).

USISHUGHULIKIE TATIZO, SHUGHULIKA NA CHANZO CHA TATIZO

Ibada ya kesho itakuwa ni ya muhimu sana na ya kihistoria katika maisha yako huenda usipate nafasi kama hiyo tena kwani tutashughulikia vyanzo vyote vya matatizo uliyonayo. Watu wengi wanahangaika kutatua matokeo ya tatizo badala ya kushughulikia chanzo cha tatizo na baada ya muda matatizo yao yanarudi palepale. Shughulikia chanzo cha tatizo na tatizo hilo litanyauka maramoja na kufa kabisa. 
Kwanini uteseke wakati MUNGU anakuwazia mema? Wagonjwa wote wenye magonjwa sugu kama Kisukari, presha, Ukimwi na Kansa kupitia jina la YESU KRISTO hakika watapokea uponyaji katika ibada ya kesho.

KARIBU UKUTANE NA MTUMISHI WA MUNGU APOSTLE GODFREY FUNGO ANAYETUMIWA NA MUNGU KWA NAMNA YA KIPEKEE NA KWA KIWANGO CHA JUU SANA KUWAFUNGUA WENYE SHIDA NA MATATIZO MBALIMBALI.

NAKUKARIBISHA KATIKA IBADA YA KESHO JUMAPILI, KWA WALIOKO MWANZA PANDA GARI ZA KUELEKEA AIRPORT SHUKIA KITUO KINAITWA ILEMELA KANISANI NA HATUA CHACHE MBELE UTAONA HEMA JEUPE (HEMA LA MGUSO) KARIBU.


[10/22/16]   Kanuni mojawapo ya kugundua nguvu iliyoko nyuma ya tatizo la muda mrefu ni '' USIACHE KWENDA KANISANI HATA KAMA KUNA KILA SABABU YA WEWE KUTOKWENDA KANISANI''.

Ukisoma LUKA 13:10 ni habari ya mwanamke aliyekuwa amepindana kwa miaka 18. Mwanamke huyo alienda katika sinagogi(kanisani) siku ya sabato kama ilivyo desturi yao. Mwanamke huyu biblia inasema alikuwa na "pepo" wa udhaifu na pepo huyo ndio aliyesababisha mwanamke huyu kupindana kwa miaka 18.

Hii inamaanisha kwamba, mwanamke huyu asingeenda kanisani basi asingepona ugonjwa wake hadi angekufa. Lakini alipokwenda kanisani ndipo alikutana na Yesu akawekewa mikono na akapona kabisa.

Usikubali kubaki nyumbani na kusali kupitia Television peke yake, Waebrania 10:25 unasema "wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine... na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia". LUKA 2:49... Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? Yesu mwenyewe alienda kanisani, kwanini sisi tusalie nyumbani?

Nakusihi katika jina la Yesu, usiache kwenda kanisani hata kama una sababu ya msingi sana ya kukufanya usiende kanisani, na MUNGU akakutane na maisha yako. Amen

Hivi ndivyo kongamano la kupokea baraka linavyoendelea.

Untitled Album

Semina ya kujifunza kanuni za kumtoa mtu  katika tatizo la muda mrefu katika Biblia.

Semina ya kujifunza kanuni za kumtoa mtu  katika tatizo la muda mrefu katika Biblia.

[10/20/16]   Kwenye kila tatizo linalotokea katika maisha yako, ipo nguvu nyuma yake inayosababisha tatizo hilo. Mungu akupe neema ya kugundua kila nguvu iliyopo nyuma ya tatizo lako na ukawekwe huru katika jina la Yesu!

Photos from LIFE Givers Ministries International's post

Photos from LIFE Givers Ministries International's post

Maombezi katika huduma ya Life Givers International Ministries ya

Maombezi katika huduma ya Life Givers International Ministries ya

Timeline Photos

Apostle Godfrey Fungo, Mama Apostle Godfrey Fungo, Christina Shusho na Martha Mwaipaja wakiwa mbele ya Mama Wajane wakiwatia Moyo na kugawa zawadi kwa Mama Wajane. Ilikuwa mwisho wa Kongamano la Mwanamke Usilie Tena.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye Kongamano la Mwanamke Usilie Tena. Watu walikuwa ni Wengi sana kama unavyoona kwenye picha hapo chini.

Betty Lukasi Akiimba kwenye Kongamano la Mwanamke Usilie Tena

Shusho akiimba

Christina Shusho Akiimba live kwenye Mkutano huo

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Address


Mwanza
Mwanza
30585
Other Religious Centers in Mwanza (show all)
EAGT Bethel Kisesa EAGT Bethel Kisesa
Kisesa
Mwanza

Jesus Restoration Centre - JRC Church Jesus Restoration Centre - JRC Church
Kirumba
Mwanza, 255

Jesus Restoration Centre ni kanisa la kipentekoste lililopo chini ya uongozi wa Mchungaji George Mukabwa. Kanisa hili lilianza Novemba, 2011.

Africa Inland Church Tanzania - AICT Africa Inland Church Tanzania - AICT
P.O Box 905 Makongoro Street, Plot No 66
Mwanza

Kanisa linalothubutu katika kutimiza utume kamili kwa utukufu wa Mungu (a daring church that carries out a holistic mission to the Glory of God).

Efatha-Mwanza Efatha-Mwanza
Mwanza
Mwanza, P.O.BOX 11626

Efatha mwanza is located at nyakato nundu B in we are among the church which are growing very fast. We are running the vision and mission of Apostle J.E.M

Ukombozi church Ministries Ukombozi church Ministries
P.O.Box 10568 Nyamagana
Mwanza, +255

This is An Official Account, we want to show the world extra ordinary Miracles that Lord Jesus is doing through our Ministry. Web: www.ukombozichurch.org

About   Privacy   Login C