Tanzania Baptist Youth Ministry

Tanzania Baptist Youth Ministry

To provide a KNOWLEDGE of Jesus Christ HOPE for the future PEACE of mind and an assurance ETERNAL LIFE for the Youth.

[06/16/17]   Msiwalipe watu ovu kwa ovu au tusi kwa tusi:Bali watakieni baraka,maana ninyi mliitwa na MUNGU mpate kupokea baraka. 1PETRO 3:8-9

Nawatakia cku njema yenye baraka tele

[05/21/17]   Good Morning all
6 Ewe mvivu, mwendee chungu,Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana akida,Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9 Ewe mvivu, utalala hata lini?Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi,Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Mithali 6:6-11

Nawatakia ibaada njema na Jumapili yenye baraka!

[05/19/17]   Good Morning!!

16 Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu.

ZABURI 59:16
Amen Mungu akubariki!

[04/26/17]   TABIA YA KUIGA HAIDUMU

Mtu mmoja mfugaji wa kondoo alikuwa anavuka mpaka na mifugo yake .Pamoja na kondoo alikuwa na mbw a mmoja. Sasa katika nchi aliyokuwa akiiendea Iilikuwa hairuhusiwi kuvuka na mbwa,.
Kwa vile Mtu huyu alimpenda sana mbwa wake akaamua kumvisha ngozi ya kondoo. Yule mbwa akavaa akaonekana kama kondoo,

Walipofika mpakani Iilikuwa ni lazima kondoo wote wachomwe sindano ya chanjo. Hapo Sasa kawaida ya kondoo ni wapole na wavumilivu wakawa wanachomwa sindano wanapita wanavuka Sasa ikafika zamu ya mbwa aliyevalishwa ngozi ya kondoo hata kabla sindano akabweeeka ikajulikana sio kondoo ni mbwa ,dog, ni popi,

Wapo wengi maishani wamejificha kama watu wemaa lakini ndani yao ni Mbwa wakali dawa ni sindano ya chanjo ichomwe.

Ni maombi yangu Kwako msomaji na Rafiki yangu MUNGU apitishe sindano ya chanjo Kwa wote wanakuzunguka ili uwujue walio mbwa mwitu na walio kondoo.
Barikiwa na Bwana pia uwe na cku njema.

[12/27/16]   FROM MY SEEKING HEART...Dear heavenly Father, Please help us to always remember where we would be if it were not for You. Open our hearts to be aware of the needs of others. Open our eyes to see ways of helping and our ears to listen and respond. Teach us to love others as You love them and to accept the privilege of reaching out to them. Lord, we want to be Your ambassadors. Most of all, Father, increase our openness to Your leading in our daily lives. In the name of JESUS CHRIST, our Savior, we pray...Amen

[12/11/16]   Mithali 20:4
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi;
Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.
Mchana mwema

[12/06/16]   Ukiona Mchungaji wako au Mwinjilisiti wako kwenye mahubiri yake hagusi dhambi yoyote anayoitenda mwanadamu katika maisha yake ya kila cku, yawezekana kabisa na yeye ni mwana Chama wa Chama hicho, Anza kumchunguza Mchungaji wako au Mwinjilisiti wako ili uanze kuchukua hatua bado mapema usije ukaikosa Mbingu! 🏇

[11/29/16]   Morning glory; Majira ya mwisho wa mwaka kama haya mikono ya wanaokupinga na kutaka uaribikiwe huongezeka lakini Usiogope, kwa jina la YESU aliye hai kila mkono utakao inuka kwa ajiri yko kukupinga utavunja kama ulivyo vunjwa wa farao alipopinga Israel kutoka misri, EZE 30:21.

[11/18/16]   Kuwa hodari na mwenye moyo mkuu, usiogope wala usifadhaike kwa ajili ya wanaokupiga vita maana yupo Mungu mkuu pamoja nawe; 2NYA 32:7
Nawatakia asubuhi na cku njema!

[11/17/16]   Bwana Yesu asifiwe wapendwaaaaaaa.
Macho ya Bwana yanakimbia kimbia kuhakikisha uko salama ww na mambo yko dhidi ya nguvu na hali yakutisha inayokukabili; 2NYAKAT 16:9. asubuhi na cku njema.

[11/16/16]   Morning glory; Hakuna atakaye weza fupisha maisha yko au mafanikio yko maana Bwana ameahidi kukushibisha siku nyingi za kuishi, ZABURI 91:16.

[11/12/16]   Bwana Yesu asifiwe wapendwaaaaaaa
Uwapo mbele za Bwana omba kwa ajiri yako na kwenu, watoto wko pamoja na malizako ili mafanikio yako yawe yenye kishindo kisicho na misiba,hasara,magonjwa na chuki; EZRA 8:21

[11/10/16]   Morning glory; Bwana akutie nuru ktk macho yko ya rohoni uweze kuona utajiri wa urithi wa Ibrahimu ulipo mbele yko; EFESO 1:18. Ongeza bidii mafanikio yalio mbele yko sio ya kawaida ni makubwa mno.

[11/08/16]   Bwana Yesu asifiwe wapendwaaaaaaa katika Bwana!
Iko roho ya konokono ya kuchelewesha mambo, inatesa watu wengi, kazi yke nikuhakikisha kila unacho anzisha kisifikie malengo au kishie njiani kama konokono avukapo barabara taratibu na kugongwa kabla hajafika safari yke; ZAB 58:8, KWA JINA LA YESU roho hio iyeyuke na kutoweka kwako.
Mkue na cku njema

[11/05/16]   CONFESSION OF SIN. if we confess our sins to Him, be is faithful and just to forgive us and to cleanse us from every wrong. 1 John 1:9
Have a good Saturday dearest!

[11/02/16]   MAOMBI YA YAFAA KWA MUDA MUAFAKA.
Biblia inasema panapo usiku wa manane PAULO na SILA walikuwa wakiomumba MUNGU NA na kusifu PAULO na SILA walitambua nguvu ya maombi ya uck wa manane.Minyororo yote ikafunguka.Kama unataka tetemeko la roho Mtakatifu litikisike na ksambaratisha misng mibaya ya ukoo,lazima uanze na maombi ya usiku wa manane.Hata Daudi alifahamu siri ya maombi ya usiku wa ma8 ZABURI 119:62 Na YAKOBO ukisoma MWANZO 32:24_30 Utaona historia ya YAKOBO kuwa alianza maombi saa 10 jion mpaka saa 11 UKIAMKA USIKU WA MANANE LAZIMA SIKU IWE NJEMA
Nakutakia asubuhi njema!

[10/31/16]   je? ni nani awezaye kujiokoa ktk midomo ya simba wakali? NI YESu TU NDIE JIBU. usikate tamaa kwa chochote yupo wa kukushindia
Have a good night!!

[09/16/16]   Kama bado hujapata mume/mke!
Una vigezo gani ambavyo umemwambia Mungu akupe mke mwema?
Tafadhali share na cc asante sana

[08/26/16]   When you love someone wanna you die for her?
God loves you all the time

[08/24/16]   Unapotaka kuoa/ kuolewa kijana mwenzangu unachagua mwanamke/mwanaume wa maana gani?
Tujadili pamoja wapendwa
#SirEliman
Wishing ya all a gud day

[08/17/16]   Habari ya asubuhi vijana wenzangu!
Tujadili pamoja

Kwanini vijana wengi huwaogopa mabinti waliowazidi elimu na kipato?; wakati mabinti wengi huwakubali kwa ujasiri vijana wanaowazidi kiwango cha elimu na kipato???
Mjadala Mwema asante sana!
#SirEliman

[08/16/16]   Habari ya asubuhi kijana mwenzangu!
Leo kuna mada ya kuchangia inayosema;

Una fikiri nini chanzo cha mahusiano kuvunjika SKU hizi kwa vijana ,walosema ni wachumba au wapenzi baada ya muda wanakuta wameachana tatizo ni nn na tufanye nn?
Nawatakia maoni mema
#SirEliman

[08/11/16]   Mungu atawafanya maadui zako waishiwe nguvu za kukudhuru wiki hii na kukupa ulinzi wa kutosha mbele zako katika jina la Yesu Kristo Amen.
Tafadhali andika "Amen" kama uniamini Mungu anashughulika na adui zako!.
#SirEliman

[08/08/16]   Friend, if you are one of the people who believe, that you must pay the price of suffering, in order for you to be happy, or in order for God to approve of, or favour you, then today is the day, for you to kick that idea and persuasion, to the curb. Reject it, and along with it, reject any kind of suffering or difficulty, which tries to justify its presence in your life, with the excuse, that you must suffer to be happy or that God justly requires it of you. It is My just decree, that in order for any just individual, to live a good and happy life, all you need to do, is understand, that happiness in the Kingdom of Righteousness, is without cost and without price. And if any requires a price of you, whether it be man, spirit, or any force or power, tell them:

“For the LORD God is a sun and shield; the LORD bestows favour and honour; no good thing does He withhold from those whose walk is blameless.” (Psalm 84:11)
#SirEliman

[08/04/16]   Bwana Yesu Asifiwe!
Tafakari juu ya hekima ya kibiblia kwa kiongozi wa ngazi yoyote;
"Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu" (1Petro 5:6-7)
Alhamis njema!
#Eliman #John

[07/19/16]   Utunze ujana wako ili Mungu akuandalie aliye mwema amen

[07/04/16]   GOD is LOVE. But we cannot reach Him or feel His Love towards us without FAITH for the scripture read Without FAITH it is impossible to please God. FAITH is the currency of God's Kingdom, it is the confidence of what we HOPE for and assurance about what we do not see. #Sir #Eliman
Wishing you a great week

[06/21/16]   Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Bwana tutafakari neno la cku hii ya leo ndo nguzo katika imani tuliyonayo!
''Kwa IMANI wakapita kati ya bahari ya shamu, kama nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya hivyo WAKATOSWA" Kwa IMANI, pito, jaribu, shida, tatizo, magumu, mateso. Amini mpendwa ukiwa kama mwana wa Israel wa leo katika Jina la Yesu na wewe utayavuka na kuelekea USHINDI WAKO. Tatizo lolote litakalo kufuata Nyuma MUNGU ATALISETA kama alivyomseta Farao. Kama unaamini like au sema Amen!
Nawatakia cku njema na yenye baraka tele Amen
#Sir Eliman

[06/15/16]   Wengi wao wanafikiri kubarikiwa na Mungu ni kuwa na magari, majumba, nk.
Mimi ninavyojua baraka halali itokayo kwa Mungu ni watoto.

Mwanzo 1:27-28a
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mungu akawabarikia, akawaambia zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha;
Ninaumia sana ninapoona watoto wanapotupwa majalalani, watoto wanapotelekezwa na kufanyiwa vitu vibaya kweli inasikitisha.
Watoto ni zawadi kubwa mno kutoka kwa Mungu.
Tumuombe Mungu atuokoe na haya majanga ya ulimwengu huu!
#Sir Eliman

[06/02/16]   Mungu atafanya nyia pasipo na njia, atakuonesha njia ya mafanikio, pale adui yako alipojaribu kukufungia ndipo hapohapo Mungu atakufanishishia!
Sema #Amen kwakua Mungu ni mtetezi wako kila iitwapo leo!
Nakutakia cku njema yenye baraka tele Amen

[05/31/16]   Habari ya asubuhi wapendwa katika Bwana!
Mungu watu ni mwaminifu kamwe hawezi tuacha bila ulinzi wake mwamini yeye na mtumaini Jehova kwa kila mipango na mambo yako nae atafanya kwa uaminifu amen!
Nawatakia cku njema na Mungu wa mbinguni awabariki wote

[05/27/16]   "Mwenyezi Mungu alimpa karama kila mwanadamu, waliobahatika kutambua karama zao walizitendea haki na Mungu akaweka baraka zake na sasa wanaishi maisha ya furaha na faraja sababu hakuna faraja kama kufanya kazi katika kitu unachokipenda, hauwezi choka kufanya kazi katika eneo la kipaji chako."

🙋�🙋�🙋�🙋�🙋�🙋�🙋�🙋�🙋�

Habari za asubuhi.

[05/20/16]   SOMO: LEO NI SIKU YA KUPATA MAJIBU YAKO
Leo ni siku ya kupata majibu yako;
Yoshua 6:1
Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Isareli, hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia, Bwana akamwambia Yoshua, tazama nimeutia Yericho katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake, nanyi mtauzunguka mji huu watu wote wa vita mkiuzunguka mji huu mara moja, fanya hivi siku sita.
Mji ulikuwa umefungwa kwa ajili ya hofu ya wana wa israeli, hamna mtu aliyekuwa anatoka wala kuingia, lakini akatokea mtu shujaa, wa kipekee haijapata kutokea kuingoza israeli, taifa lililoachwa na Musa
Biblia inasema, mji ule ulifungwa - ni kama biashara zako, shughuli zakko, hakuna kiachoendelea, hata meza na viti vyako nyumbani unaona kuwa havitamaniki.
Biblia inasema Yoshua akiwa katika hali ya kutafakari , jinsi gani ataukabili huo mji, kama ambavyo unatafakari mda huu, namna gani utakabiliana na matatizo, inawezekana ya ndoa, ada za watoto, mambo ya kazini kwako, jinsi biashara inavyoyumba, na hata kufikiria mpango wa kuhama mji, jibu lako liko sasa.
Bibia inasema Joshua alipopata ujumbe huo kutoka kwa Mungu, ambaye hata hakubabaisha - wala hakujaribisha kumwambia kwa uwazi kuwa "mji huu nimekupa", hapohapo ulipo umepewa, vyote unavyovitamani, huyu Joshua alipewa wakati mji umefungwa, watu wanaogopa kuingia na kutoka nje, lakini kauli ya Mungu ilivunja viambaza vyote.
Katika Jina la YESU KRISTO, lile linalokutesa linaenda kuyeyuka, kwa sababu Mungu ndiye aliyekupa, kilichosimama kwako ni ukungu tu ambao unayeyuka mbele za Bwana.
Lakini haikuwa rahisi kama unavyodhani Yoshua kuchukua ile nchi, haikuwa rahisi kuuchukua ule mji, haikuwa rahisi kuchukua ile baraka ambayo Mungu ameipanga, haikiuwa rahisi. watu wengi wameokoka, wanamtaja Kristo, lakini wanakosa kwenye maelekezo ambayo Mungu anataka wayapitie ili kupata baraka.
Yoshua akiwa wakati huo anazunguka-zung
uka, na Bwana amemuambia 'mji umepewa', akamuagiza maagizo makubwa, lakiniYoshua akawaendea wana wa Israeli akawaambia ili wauteke mji ilwapasa wadamke asubuhi sana na mapema,
Yoshua 6:15 Akawaamuru waanze kuondoka asubuhi na mapema, ili kuukabili mji.
Ndugu, ni kweli unahitaji muujiza, wengi wanapenda muujiza dezo, wanapenda kuombewa, na hata kwenye radio utawasikia 'niombee, niombee' lakini wao hawataki kuomba. Sasa hivi nikuambie kuwa SIRI ya kujibiwa, ni kuanza siku yako asubuhi na mapema, hata wachawi wanaologa, hawalogi saa nne usiku wala saa moja asubuhi - wanaaza asubuhi na mapema, saa tisa, kumi, kumi na moja. wanaovunja nazi na mayai viza njiapanda hawavunji saa tatu - saa nne, wanavunja kukiwa na giza bado - asubuhi na mapema, hakuna asiyejua maana ya asubuhi na mapema, asubuhi inaeleweka, na mapema yake ni asubuhi zaidi ya asubuhi.
Maana yake kila mtu anayemwamini Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi, kama ewe unayetaka majibu yako kwa njia ya maombi, hutaki majibu yako kwenda kuaguliwa, ama kwa njia ya ramli kwa kuwa unamwamini Mungu, basi jibu lako lazima lianze asubuhi na mapema kabla wachawi hawajaloga, unaamka mapema na kuanza kumsifu Bwana na kuiombea siku yako, unaiweka kwa Bwana biashara yako,
Nakupoa siri ya kufanikiwa kwako, maana mara nyingi umelalamika kuwa pamoja na maombi mambo yako hayaendi sawa, yako vilevile - jibu lako huanzi siku yako asubuhi na mapema, watu wote wa Mungu, hata Yesu Kristo mwenyewe Biblia inasema alikuwa anajiangua katikati ya watu anaenda mahali pa peke yake kuiweka siku sawasawa, halafu anakutana na wanafunzi wake siku inayofata.
Kwa hiyo siri ya kwanza ya tunayoisoma ya Yoshua kufanikiwa au kuangusha ukuta wa Jericho ilikuwa ni kuanza siku mapema, mstari wa kumi na tano unaeleza hivyo, ni vizuri uelewe kuwa hata wale wanaomuabudu shetani, hawamuabudu saa tatu.
Utakuta mtu anasema ameokokoka anamuamini Mungu, lakini kuamka kwake ni saa moja, saa moja na nusu ndo ananyoosha mikono anasema 'Bwana unajua jana mimi njilichoka', anapiga na mihayo ya hasarahasara, amka asubuhi na mapema saa kumi, saa kumi na moja, ombea biashara yako, ombea kuamka kwako, mitaa yote unayopitia, wateja wote, waamuru waje kwa jina la Yesu, kabla wachawi hawajaloga.
Lakini watu wengi mijini, wanaamka wakati watu tayari wameloga, wamemkanyagia mlangoni kwenye chumba alichopanga, wamemwaga maji ya maiti tayari ameshalogeka, yeye anapita tu kwenda kazini, na anakuta mambo hayako sawa, na hata akivuka njia panda hana maombi, hana nguvu yoyote, wachawi wameshatangulia ndio maana unakuwa mtu wa kushindwa mara kwa mara.
Siri ya kuvunja ukuta wa Yericho, Yoshua alisema 'tutaanza kuzunguka asubuhi na mapema' kwa hiyo hata kama wewe ni mgumu kuamka, katika Jina la Yesu kuanzia leo uanze kuamka asubuhi na mapema. Ili mradi umeamua kumuamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako, ukweli utakuweka huru.
Nitakupa mfano, kanisani kwangu nilikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri, na baadae biashara zake zikaanguka kabisa, nilipokuwa namuuliza siri ya biashara yake kabla hajaokoka, akasema, ilikuwa ni asubuhi saa tisa au saa kumi ni lazima afanye matambiko fulani fulani, aende kuzikwa makaburini na kichwa cha kondoo - kwenye kaburi la mtu fulani saa tisa au saa kumi. Kwa hiyo ushirikina wote unafanywa asubuhi, wakati wewe unakoroma. Mtakatifu - haiendi hivyo., amka asubuhi na mapema uizungukie siku yako.
Huyu mtu anasema baada ya hapo akienda kwenye shughuli zake, biashara zake zinavuta watu maelfu na maelfu, kumbe siri yake na shetani wake, alikuwa anaifanya saa tisa mpaka kumi, kumi na moja. Hivyo siri ya watakatifu nao wanatakiwa wajue kuwa, kufanikiwa kwao ni kuamka asubuhi na mapema.
Yeremia 29:10 Mungu anasema ni vizuri uamke asubuhi na mapema
Unapoamka asubuhi na mapema, ina maana majibu yako yapo tayari, na hapo ndipo utajua kuwa huna haja ya kulaumu wahubiri wala wachungaji - ni wewe mwenyewe wa kujilaumu kwa kuwa huanzi siku asubuhi na mapema.
Nakutakia cku njema yenye baraka tele Amen

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


P.O.BOX 11794
Mwanza
Other Mwanza places of worship (show all)
Deliverance Church Int'l Mwanza Deliverance Church Int'l Mwanza
Mwanza, MWANZA

Located at Buzuruga, Mwanza, Tanzania. Welcome

Huduma ya Maandiko Huduma ya Maandiko
P.O. Box 2017
Mwanza, 25528

Worlds Largest Christian Bible Study site. All available as a free download .

Efatha Ministry Mwanza Efatha Ministry Mwanza
P.o.box
Mwanza, 11626

The Official Efatha Ministry MWANZA page. You tube: https://youtu.be/vb7qVVxIfO8 http://www.instagram.com/efathamwanza

Melkizedeki Hope International Melkizedeki Hope International
Plot No. 114 Block "B" Nyakato National, P.O. Box 1844
Mwanza, 25528

We support orphans and offer access to basic needs to the poor. Please give food, clothes, shoes, bedding or education to the needy.

AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania
Nyangulugulu Mlimani
Mwanza, S.L.P. 7508

Injili, Ibada, Mafundisho ya Neno la Mungu, Maombezi na Utumishi wa Kweli.

New Vine Church-HQ New Vine Church-HQ
Mwanza

NVC is a Church committed to see the raising of great Godly generation with the aim of making impact, changing lives and influence the World.

Peter Mbajije victory - Angaza Gospel Peter Mbajije victory - Angaza Gospel
Tanzania
Mwanza, 83

Utukufu una yeye aliyezifanya mbingu na Nchi.What'sp no (+255) 752 107 183 Email:[email protected]

Ukombozi church Ministries Ukombozi church Ministries
P.O.Box 10568 Nyamagana
Mwanza, +255

This is An Official Account, we want to show the world extra ordinary Miracles that Lord Jesus is doing through our Ministry. Web: www.ukombozichurch.org

Bujora Sukuma Museum Bujora Sukuma Museum
Bujora Cultural Centre (Sukuma Museum)
Mwanza, 76

Visit us and discover the traditional and contemporary life of the Sukuma people. Tour the museum and join us for the annual Bulabo Dance Festival in June!

Africa Inland Church Tanzania - AICT Africa Inland Church Tanzania - AICT
P.O Box 905 Makongoro Street, Plot No 66
Mwanza

Kanisa linalothubutu katika kutimiza utume kamili kwa utukufu wa Mungu (a daring church that carries out a holistic mission to the Glory of God).

Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania
Mbeya
Mwanza, DODOMA, DAR-ES-SALAAM

Lengo ni kumtumikia Mungu bila kujari madhebu yetu kama Vijana. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu. Zaburi 60:12

About   Privacy   Login C