AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania

AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania

Injili, Ibada, Mafundisho ya Neno la Mungu, Maombezi na Utumishi wa Kweli.

Karibu sana katika Kanisa la AICT Nyangulugulu upate fursa ya kuokoka, kujifunza Neno na kumfahamu Mungu kwa ufasaha au kama u mtumishi wa Mungu, unaweza kupata fursa ya kumtumikia Mungu.

Mission: Kuwafikia watu wote ulimwenguni ili kuwapelekea habari njema ya Injili, ubatizo mafundisho na wokovu wa Bwana wetu Yesu Kristo. (Mathayo 28:18-20, Yohana 3:5)

[12/12/19]   Naomba kujua eti Mungu ni jina au cheo?

Sisi na vijana tuko mahali Fulani amazing tukimfurahia Yesu Kristo. Amina sana vijana wa AICT NYANGULUGULU.

Leo Tumetoka out na vijana wetu tuwapendao huku wameogelea, wamekunywa tani yao na vitafunwa kibao picha kwa wingi. Karibuni AICT NYANGULUGULU MAHINA.

Kanisa linalokua kasi sana hapa jijini Mwanza. Karibuni tumwabudu Mungu kwa viwango vingine. Amina,

Tunaendelea kujenga maliwato safi ya kisasa kwa ajili ya wana wa Mungu kabla ya kuezeka kanisa ! Toa maoni juu ya hatua hii tafadhali.

[07/06/19]   Yesu Kristo yuko Karibu kurudi jitakaseni!

[07/06/19]   Karibu kwa ibada ya kesho
Hapa Nyangulugulu.

[07/08/18]   Tunawapenda wote mliolike page yetu! Mungu awaangazie nuru ya uso wake na kuwalinda amen!

Welcome at AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania FOR THE REAL WORSHIP concentration! Tumetulia mbele za Mungu tunakula na kunywa mezani pake!!

Naona kama maono! Huyu Yesu Kristo Amekaribia kurudi lakini kwa kweli atatukuta bado tunashangaashangaa! Tena tunakutwa tunapambana na kuumanaumana tu. Mara manabii wa uongo, Mara Huyu ni MTUMISHI fake. Tukumbuke kuwa safari ya mbinguni ni ya MTU moja wala si kikundi cha wanakanisa wote. Halafu Yesu wa Nazareth alisema Sikh za mwisho hata wateule watadanganywa wasipokuwa makini? Kaa chonjo!
Tengeneza uhusiano wako na Mungu bado mapema.

Pasaka ni bomba sana hapa kanisani kwetu

Ibada zenu za pasaka ni bomba sana hapa kanisani kwetu.

Tunatafuta fundi mzuri wa kuezeka kanisa letu kwa vyuma! Tutamlipa vizuri! Tupo AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania KARIBU NA MLIMA WA NYANGULUGULU! Karibuni Mafundi Ujenzi!

Baada ya kuukaribisha mwaka sasa kila mkristo anatakiwa kuzaa matunda yapasayo toba! Kutubu kwako kwaongeza utakatifu. Ukiwa nao utakatifu tampendeza Mungu! Tueni eatakatifu au vipi jamani?

Tumefanikiwa kuvuka ng'ambo mwaka huu! Tumeanzisha kazi huko kanindo, tumewahudumia watoto wajane, tumelilisha kanisa la Bwana kwa chakula, tumekamilisha boma LA kanisa letu jipya lakini tumehuburi injili kwa wingi hasa ile ya nymba kwa nyumba! Yote ni kwa kuwezeshwa na Mungu Mwenye UTUKUFU NI WAKE!

AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania's cover photo

AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania's cover photo

Huduma za jamii Ni lazima kwa kanisa

Ibada iliyojaa Baraka za Bwana. Watoto wetu wakihitimisha ibada za kempu hapa AIC Nyangulugulu Leo 23/7/2017.

Hawa no wenyeji wetu huku kanindo!
Sehemu mpya ya utume mkuu!
Asanteni kuukaribisha!!
Tarehe 2julai 2017.

Tayari sana. Tuna mkutano wa injili huku AICT MHANDU! Tumepiga injili tangu jumatano hadi Leo Tarehe 25/6/2017. Wengi wamemwamini Yesu Kristo!! Sema AMINA.

AICT NYANGULUGULU Tuafurahia kupata mafundisho bora us nenola Mungu kutoka kwa mchungaji Zephaniah Masaga wa Nyakato Pastorate.

Sisi tunapoomba wachawi huwa wanakuta na na nguvu za Mungu .nguvu hizi huwapiga na kuwaacha peupe! Kazana kuomba ili tuwe na ulinzi wa Mungu!¡!!

This is the holy Sunday service at AICT Nyangulugulu. We worship preach and teach the oracles of Jehovah ADONAI. We are located at mahina nyangulugulu! welcome!

[05/15/17]   Sisi tu warith pamoja na kristo katika ufalme was mwanakondoo.

[04/30/17]   Yesu asema anataka kwetu rehema na si sadaka. Rehema ni huruma na matendo mema kwa wengine pamoja na moyo wa kumpendeza Mungu.

[02/24/17]   Ikiwa wewe ni mtu mwombaji yaani mwanamaombi au mpenzi wa AIC Nyakato Choir, tafadhali omba rehema kwa Mungu kwa ajili ya hii kwaya ili Mungu awapatie nguvu ya Roho Mtakatifu na haki zao zote zilizopotea na wapate nafasi ya kupendwa na kutetewa na Mungu kama watoto na watumishi wake. Wanaomba na wanahitaji maombi yako sana. Ni muhimu ukafanya hivyo sasa (hata moyoni) kwa dakika chache au nyingi bila kujali uko katika mazingira gani. Tumia damu na Jina la Yesu katika maombi yako. Kisha "share" na uwashirikishe wengine.

[02/21/17]   Mwili na damu ya Yesu ni uzima. Aulaye mwili wake na kuinywa damu yake hataonja mauti milele. Je, unaamini maneno hayo?

Yesu hajatuagiza kuhitaji wingi wa mali, bali ametuagiza kuomba "Riziki yetu" ya kila siku tu na vitu vingine anajua mwenyewe namna atakavyotupatia ikiwa vitahitajika kwetu maana aliaibishwa, aliteswa na kusulibiwa msalabani, alikufa, akafufuka na yu hai milele kwa ajili yetu sote. Tusiogope, maana hata kama tukifa tutafufuka naye (Mathayo 6:9-11).

Shughuli ya uzinduzi wa Albamu ya Video ya "Yesu Nitetee" ya mwinjilisti Yusuph M. Nghumba imekamilika leo hapa kanisani kwetu. Watu wameponywa na kubarikiwa kwa nyimbo zake. Yusuph ni baba wa familia na mlemavu wa macho (kipofu), hivyo tunamwombea Mungu azidi kumpa neema na kumtumia. Kama hujanunua DVD yake, tafadhali fanya hivyo sasa. Amen.

Tumsifu MUNGU

Kwa Wana Muziki wa nyimbo za Injili, Wanakwaya, Bendi ambao tayari wamesharekodi Nyimbo zao, STAR Religion, STAR MUZIK inakupa/inawapa nafasi ya kuwachezea nyimbo zenu, Tumeni DVD zenu, ama fika Ilemela ofisini, Wanakwaya wote mnakaribishwa kuleta nyimbo zenu.

Tumsifu MUNGU

Tumsifu MUNGU

Mwinjilisti Paulo Sengerema wa AIC Nyakato (Local Church).

Mchungaji Zephania Masaga wa AIC Nyakato (Pastorate).

Melkizedeki Hope International

An orphaned and widowed family in Mhandu Mwanza Tanzania. Right is Laurencia. She is an orphan waiting for her Standard 7 primary education national examination results. Sitting is her orphaned grandmother with her sister. Little kid is Laurencia's sister's daughter who is also abandoned by his father. This fatherless and motherless family needs support for making a significant change in their lives. Please, could you help? Contact us for more information about this support.
Update: (13/12/2016) Laurencia has passed her primary school national examinations to join new class of Form One in a day and secondary school. Her family is unable to finance for her educational needs. All are left alone, poor and needy. She needs education sponsorship to enable her continue with school.

Mungu akikubariki kiuchumi, usipandishe kiwango chako cha maisha. Pandisha kiwango chako cha UTOAJI sadaka kwa wahitaji na maskini. Fanya hivyo sirini maana Mungu akuonaye yuko sirini.
(Mathayo 6:1,4)
Like & Share

Hakikisha unachukua Biblia yako kila ulipo, iwe ni kanisani au mahali pengine popote kwani Mungu anaweza kuhitaji kuzungumza na wewe kupitia maandiko yake usiyoyajua.

Zaburi 35

1 Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.

2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie.

3 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.

4 Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.

5 Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.

6 Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia.

Nyakato Revival Band - Yohana A. Gomgo

Nunua DVD original kwa faida yako. Epuka bidhaa zilizochakachuliwa na kupunguziwa ubora. "Wewe ni Bwana" ni albamu yetu ya video yenye nyimbo 8 ukiwemo wimbo wa 'Wewe ni Bwana' na 'Misukosuko'.

Nyakato Revival Band - Yohana A. Gomgo

Nyakato Revival Band ni bendi ya Kikristo. Tunatoa huduma za uimbaji katika makanisa, mikutano ya Injili, ibada, semina n.k. (LIVE/VIDEO/AUDIO).

Timeline Photos

Ibada ni pamoja na kujiona mdogo kwa Mungu na kukubali kujitia chini ya ghadhabu yake kwa dhambi ulizonazo. Shetani hatajiinua tena katika maisha yako kwa jina la Yesu. Sema amina.

Zaburi 35

1 Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.

2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie.

3 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.

4 Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.

5 Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.

6 Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia.

Leo tarehe 9/10/2016 Mch. Zephania Masaga pamoja na AIC Nyakato Choir wamehudhuria na kuhudumu katika kanisa la FPCT Nyakato kwenye ibada ya Jumapili kama ishara ya upendo, kudumisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya makanisa haya mawili yaliyo jirani. Uhusiano huu umetokana na kuwa na ushirikiano katika mikutano ya Injili. Shukrani kwa Askofu Elias Simoni, viongozi wa kanisa, mashemasi, Amani Choir na waumini wote wa kanisa la FPCT Nyakato kwa mapokezi mazuri.
(1 Kor. 12:26,27)

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


Nyangulugulu Mlimani
Mwanza
S.L.P. 7508
Other Evangelical Churches in Mwanza (show all)
Ukombozi church Ministries Ukombozi church Ministries
P.O.Box 10568 Nyamagana
Mwanza, +255

This is An Official Account, we want to show the world extra ordinary Miracles that Lord Jesus is doing through our Ministry. Web: www.ukombozichurch.org