Ukombozi church Ministries

Ukombozi church Ministries

Comments

Mungu waukombozi anatenda maajabu sana
ALIYEKUPA UHAI SIKU YA LEO MWAMBIE ASANTE kabla haujatoka online
Bwana Yesu Asifiwe, Wapendwa katika Bwana, Mimi ninamatatizo makubwa, nimefukuzwa nyumbani bila hata kosa, ninaumri wa miaka 24. Naombeni msaada wenu jamani. Namba yangu ni +255783307817 kwa aliye tayari.
Let's bless our sunday guys
MUNGU AKUPE NGUVU KULIKO MAADUI MUNGU AKUPE NGUVU KULIKO MAADUI ZAKO.
Mungu ni Mwema.Nabii GB MALISA ni Nabii WA MUNGU ALIYE HAI
Happy birthday,I am praying you
asate mungu wa ukombozi kwa kunificha adui zangu wasinione
hakika mungu wa ukombozi anajibu kwa moto
Matendoo makuu ya MFALUME ZUMARIDI mkomboozi wa dunia

This is An Official Account, we want to show the world extra ordinary Miracles that Lord Jesus is doing through our Ministry. Web: www.ukombozichurch.org

Mission: To preach the Gospel of Jesus Christ to all four corners of the word by manifesting the power of our lord Jesus Christ through the presence of Holy Spirit

MUNGU AKUPE ROHO YA KUJI- AMINI
KWAAJILI YA KUFANYA MAMBO MAKUBWA !.

Kuna Wakati Kwenye MAISHA unaweza kupitia vipindi VIGUMU sana.Na ukakata tamaa kabisa hasa Pale Ambapo MAONO YAKO HAYALINGANI NA HALI HALISI unayo Ipitia ! Yaani Unacho Kiona kwenye Roho Yako Ni kikubwa, MAFANIKIO makubwa Lakini una lala njaa.! Usikate TAMAA! WEWE ANGALIA MAONO YAKO USIANGALIE HALI HIYO MBAYA!. NI MAPITO TU! UTAFIKA!.USIFANYE MAAMUZI MABAYA KWA HALI YA KUPITA!.

Somo:VITA DHIDI YA MADHABAHU ZA UKOO
▪Matendo ya Mitume 16:16-ff
▪Matendo ya Mitume 19:23-ff
▪Matendo ya Mitume 14:19

Kuna vita nyingi hutokea kwa watu wengi leo kwa sababu ya wokovu.
Unapookoka unakuwa umemtangazia shetani vita.
Unapookoka unatangaza vita dhidi ya madhabahu za ukoo.

Mtu wa Mungu Nabii B.G Malisa amesimama madhabahuni kuhudumia maelfu ya watu waliohudhuria kwenye Ibada ya leo.

NENO LA KINABII
1.Watoto wako wataitwa waliobarikiwa sana.
2.Maombi yako ya leo yainue KIZAZI chako chote kwa jina la Yesu.
3Watoto wako waitwe waliobarikiwa kwa jina la Yesu.
4.Mwaka huu upate vitu vizuri ulivyovisubiri kwa miaka mingi kwa jina la Yesu.

Mtumishi wa Mungu,baba yake Mzazi na Nabii B.G Malisa, MCHUNGAJI GODFREY F. MALISA
akitoa salamu za neema kwenye madhabahu ya UKOMBOZI siku ya leo.

▪Mwanzo 1:26-28
Mapenzi ya Mungu kwa watoto wake ni wafanikiwe katika kila eneo la maisha yako.
Mungu amepandikiza mbegu ya mafanikio ndani ya kila mtoto wake.
Ni huzuni kusema wewe ni mtoto wa Mungu na huku huongezeki.
Maana ya KUZAA inatokana na neno PERU ikimaanisha KUZAA MATUNDA(TO BE FRUITFUL)
Kama hutaelewa kuwa una mbegu njema ndani yako shetani atakukandamiza sana.

Pili kama mtoto wa Mungu, ni lazima uwe na uwezo wa kutiisha mambo kwenye ulimwengu wa roho na wa mwili pia.

Kuna nguvu katika kumsifu Mungu...Mungu anaposifiwa kisahihi hushuka mwenyewe kwa nguvu na kujibu maombi yetu.
▪Zaburi 29:1-11

Karibu katika Ibada maalum ya UPENYO inayoendelea kwenye madhabahu ya UKOMBOZI MINISTRIES FOR ALL NATIONS-MWANZA.
▪Zaburi 84:1-12
▪Zaburi 51

Unapoendelea kufuatilia Ibada hii mubashara kwa njia ya YouTube UKOMBOZI TV au UKOMBOZI FM 104.1MHz ni maombi yangu Mungu akukumbuke mwaka huu kwa jina la Yesu.

BABA YANGU ALINI AMBIA,UKIINULIWA NA MUNGU JUU USIUACHE UNYENYEKEVU CHINI!.NA WEWE CHUKUA SIRI HII.

Hata Kama Ukiitupa DHAHABU kwenye JALALA BADO THAMANI YAKE ITABAKIA VILE-VILE.
HUENDA UMEDHARAULIWA UNAPITIA MAISHA MABAYA,USIJIDHARAU IPO SIKU WATU WATA JUA THAMANI YAKO TU!.

WEWE ni MBUYU,HaijaLishi Bado Unaonekana Bado MDOGO, IPO SIKU UTAKUWA MKUBWA! kwani MBUYU Huanza kama MCHICHA.Ni SUALA LA MUDA TU! JIPE MUDA!. BIASHARA ZAKO ZITAKUWA TU! HUDUMA YAKO ITAKUWA TU! MWAKA HUU -- 2020!!

Kila nguvu za giza zinazotaka mimi niendelee kuwa na maisha ya vile vile mwaka huu NINAZIVUNJA kwa DAMU YA YESU...!!

KESHO Yako ITANG'AA KULIKO
JANA YAKO !!

Ikiwa leo ni siku ya tatu ya maombi ya kufunga, tunakuombea MUNGU AKUONGOZEE UWEZO WA KIUNGU WA KUFANYA MAMBO MAKUBWA MWAKA HUU KWA JINA LA YESU...🙏!

Ungana nasi sasa katika Kambi ya KUFUNGA KWA AJILI YA KUPOKEA NGUVU MPYA KWA AJILI YA MWAKA HUU 2020

Tafadhali fuatilia maombi haya kwa njia ya YouTube UKOMBOZI TV au UKOMBOZI FM 104.1MHz dakika chache kuanzia sasa.

BARIKIWA NA BWANA YESU!!

Tafadhali mjulishe na mwingine kwa ku-share tangazo hili au mpigie simu mwingine ili ajiunganishe na maombi haya

Ungana nasi sasa kufuatilia Maombi haya ya kufunga ya siku 3 yanayoendelea kwenye madhabahu ya Ukombozi sasa hivi.
Tafadhali fuatilia maombi haya kwa njia ya youtube UKOMBOZI TV au Ukombozi Fm redio 104.1MHz

SHUHUDA

Ninamshukuru sana Mungu wa madhabahu hii ya Ukombozi kwa kunifanikisha kwenye mtihani wangu wa kidato cha nne.
Kwenye ukoo wetu,watu huwa hawafaulu kwenye mitihani na hasa huishia njiani.
Dada yangu alikuwa akiabudu mahali hapa, alinitumia niki kitabu cha MAOMBI YA UPENYO KWA WANAFUNZI." Nilianza kukisoma kitabu hiki kwa bidii na kufuatisha maombi yaliyoandikwa humu.
Ninamshukuru Mungu nimekosa pointi moja tu kupata DIVISION 2.Kwangu ni muujiza na kwenye ukoo wetu kutokana na historia mbaya ya elimu kwenye ukoo.
Jina la Yesu libarikiwe sana.

SHUHUDA
Nilikuja kanisani hapa nikiwa na matatizo makubwa sana.Ini langu lilikuwa na matundu,figo zangu zilikuwa na uchafu na pia mapafu yalikuwa yamevimba.
Mwonekano wa tumbo langu ulikuwa zaidi ya mwanamke mjamzito kwani tumbo lilikuwa limejaa na kuvimba sana.Nilikuwa siwezi kukaa, nilikuwa nakula kwa shida sana na hata nilikuwa siwezi kuvaa nguo zangu, bali nilikuwa navaa lubega kama Mmasai.
Nilipitia maumivu makali sana.
Wakati wa kambi ya Patmo, kulikuwa na ufunuo wa maji ya hatari.Mtu wa Mungu Nabii B.G Malisa akasema haya maji yamekuwa damu ya Yesu.Kunywa kwa imani na Mungu atakuponya.
Nilitumia maji hayo na ndani ya siku mbili tu,tumbo lilinyauka kabisa kama mnavyo niona.
Sasa hivi naweza kuvaa nguo zangu vizuri,naweza kula na ninaweza kukimbia.

Hakika Yesu Kristo anaponya...Jina la Yesu libarikiwe sana.

SHUHUDA
Nilikuwa mlevi wa kupindukia; ni ulevi wa kurithi, nilianza kulambishwa pombe nikiwa hata sijajitambua vizuri.Nimekua na hali hiyo ya ulevi, na hata nimeolewa nikiwa ni mlevi tena wa kupindukia. Nilikuwa siwezi kulala bila ya kunywa pombe.
Mume wangu alikuwa hapendi hali hii ya ulevi maana nilikuwa nikilewa tu naharibu vitu ndani na kuongea maneno yasiyofaa.
Tulikuwa hatuabudu mahali hapa, lakini mume wangu alinilazimisha Nije naye.Tulipokuja tukakuta Luna Ufunuo wa maji ya madhabahuni...Kila wiki nikawa nachukua chupa tatu na ninapeleka nyumbani.Ile kiu ikiamka tu, nakunywa maji.
Cha kushangaza kila kiu ikianza nilikuwa naona picha ya babu yangu aliyekufa akiwa na kibuyu cha pombe.
Kila mara kiu ilipokuwa ikija nakunywa maji ya madhabahu na kutamkwa,"Nakunywa damu ya Yesu. "
Leo nimekuja kumshukuru Mungu wa Ukombozi kwa kunifungua kabisa maana sina kiu tena ya pombe tena.
Jina la Yesu libarikiwe sana kwa muujiza huu mkubwa alionitendea mimi na familia yangu maana ulevi ulikuwa unaathiri hata familia yangu.

Somo:MKABIDHI BWANA MALENGO YAKO YA MWAKA 2020
▪Zaburi 37:5
▪Mithali 16:3
▪Luka 1:53
Ukitaka uone mwaka huu ukikwendea vizuri ni lazima umkabidhi Bwana MALENGO yako ya mwaka huu.
Usipange chochote bila kumshirikisha Mungu.
Mara nyingi tunateseka sana kwenye maisha yetu kwa sababu hatumpi Mungu nafasi ya kwanza.

Pata nakala yako ya Vipengele 100 vya maombi na maneno ya kinabii kwa herufi...Kitabu kimebeba ufunuo mzito wa Mungu utakaoufanya mwaka wako huu uwe na Upenyo mkubwa.

Kupata nakala hii; Wasiliana nasi kwa namba;
+255754088938
+255763710426

BARIKIWA

Neno la KINABII
1.Yeyote anayekupeleleza mwaka huu kuona unaendeleaje, ATASHANGAA KUONA UNAENDELEA VIZURI MWAKA HUU WOTE KWA JINA LA YESU.
2.BWANA YESU, ATAKUTHIBITISHA KUWA UMEOKOKA KWELI KWA MAMBO MAKUBWA ATAKAYOKUTENDEA MWAKA HUU KWA JINA LA YESU.

Mwaka huu wa 2020, MUNGU AKUPE KICHEKO kwa jina la Yesu!
Unaposifu Mungu mbingu zako zifunguke mwaka huu kwa jina la Yesu!
Unapoabudu, milango ya baraka ifunguke kwa ajili yako kwa jina la Yesu.

Karibu katika Ibada maalum ya UPENYO inayoendelea katika kanisa la UKOMBOZI MINISTRIES FOR ALL NATIONS-MWANZA
▪Zaburi 29:1-11
▪Zaburi 24:1-4
▪Zaburi 28:1-2

Unapoendelea kufuatilia Ibada hii mubashara kwa njia ya YouTube UKOMBOZI TV au UKOMBOZI FM 104.1MHz, MUNGU AUFANYE MWAKA HUU UWE MZURI KWAKO KWA JINA LA YESU!

2020 !! NI MWAKA WA KUTIMIZWA KWA NDOTO ZAKO ZA MIAKA MINGI,MALENGO YA MIAKA MINGI!.
WALIO KUCHEKA WATAONA MAMBO YAKITOKEA
WATAKIRI HAKIKA UNA MUNGU!

Simba anavyokua mdogo,anafanana na paka...na ni rahisi kuishi naye maana kwa wakati ule anakuwa hana madhara kwako na wanaokuzunguka...Kadiri anavyozidi kukua, ndivyo anaanza kudhihirisha makucha au tabia yake halisi...Ndiyo maana hafugwi nyumbani...Vivyo ilivyo na dhambi.Dhambi yoyote unayoifanya huanza taratibu, lakini kadiri inavyokua inaanza kukuletea madhara makubwa...madhara haya yanaweza kusambaa na hata kudhuru wengine wasio na hatia...Dhambi hufungua mlango wa huzuni, mateso, magonjwa, mafarakano yasiyoisha kwenye familia, ugomvi, mapepo kunishambulia, hasira zisizo na sababu, chuki...Dhambi hufunga malango ya mbingu ya baraka,...dhambi huondoa ujasiri...
Dhambi moja unayoiendekeza hufanyika sumaku ya kuvuta dhambi nyingine na mwisho huleta mauti...Mauti kwenye biashara, mauti kwenye kazi, mauti kwenye huduma, mauti mashamba na mifugo, mauti kwenye afya, Mauti kwenye ndoa, mauti kwenye mahusiano na wanaokuzunguka...n.k

Ni vizuri tuanze mwaka huu 2020 kwa toba na hakika tutamwona Mungu akisaidia maisha yetu.
▪Danieli 9:5
▪Maombolezo 5:7

[01/11/20]   DHAMBI NI KAMA MCHWA NDANI YA MTI...
Kama vile mchwa unavyotafuna mti taratibu na kuuharibu kabisa na kuleta madhara katika kila sehemu ya mti, vivyo ilivyo na dhambi.
Dhambi siyo tu huleta madhara kwako binafsi bali huleta madhara hata kwa wanaokuzunguka...iwe ni mke, mume, watoto,ndugu, jamaa na hata marafiki, kazi, wito, huduma, mashamba na hata mifugo yako pia.

Ni vizuri mwaka huu tuwe watu wa toba na kukubali kubadilika katika maneno, matendo na hata mawazo yetu.

▪Zaburi 51
▪2 Nyakati 7:14
▪Zaburi 25:6-7

#Tuanze mwaka kwa toba#
#Katika mlima wa BWANA itapatikana#
#2020#

Hata katikati Ya matatizo makubwa, Tusi zisahau nyakati za Furaha tulizo wahi kuzipata! Hata kama Huyo mtu Amekukwaza sana Leo, Usije Ukasahau Wema Alio wahi Kukufanyia.

NILIPO AMKA TU! NILIANZA KUSIKIA SAUTI IKISEMA! " NITAKUFANYA UWE TAIFA KUBWA!! NA WEWE JIUNGANISHE NA UNABII HUU MWAKA HUU! ANZA KUPANGA MIPANGO MIKUBWA! ILA USIWATEGEE WANADAMU! WATAKUANGUSHA.WEKA TEGEMEO LAKO KWA MUNGU!.

Hiki sio cha kukosa

Ule UNABII wa
MATHAYO 24: 10}
UTAANZA KUTIMIZWA sana mwaka huu, tuombe sana isitokee kwetu,.

Somo:JINSI YA KUFANIKISHA MWAKA 2020

1.Lazima ukusudie ni wapi unataka ubadilike au ni vitu gani unahitaji kubadilisha.
Pangilia mambo yako vizuri.Simamia ulichokusudia.
Ayubu 22:28

2.Anzisha jambo jipya kwa nguvu.Unapokubali kuanza upya,Mungu Naye ataanza upya na wewe.
Mambo ya Walawi 26:23

3.Jitie nguvu.Jipe moyo. USIOGOPE.
Endelea mbele bila kukata tamaa.

4.Shinda tabia ya kuhairisha mambo
5.Ishinde tabia ya kufanya mambo rahisi rahisi.
6.Ishi kwa kusudi.Usiishi bila lengo.

Neno la Kinabii
1.Kila matatizo ya muda mrefu yaishe mwaka huu kwa jina la Yesu.
2.Kila mateso ya mwaka jana yaishe kwa jina la Yesu.
3.Kama ulishinda mwaka jana,mwaka huu UTASHINDA zaidi kwa jina la Yesu.
4.Mwaka huu hutatoka mikono mitupu kwa jina la Yesu.
5.Kama mwaka jana ulipata fedha, mwaka huu utapata fedha nyingi zaidi kwa jina la Yesu.

Ikiwa ni Jumapili ya kwanza ya mwaka 2020, ninakuombea
Mwaka huu Mungu akuinulie msaada mahali ambapo hutarajii kwa jina la Yesu.
Mungu abariki kazi za mikono yako sawa sawa na Kumbukumbu la torati 30:9
Mungu aandike kwa upya historia ya ukoo wenu kwa jina la Yesu.

Kama WALIKUSHINDWA MWAKA JANA 2019
HAWATA KUWEZA KABISA MWAKA huu 2020.
Kama UNA AMINI Sema, Fire!!!!!

KITU KIKUBWA kina kwenda KUZALIWA NDANI
YAKO! MWAKA huu Wa 2020.!

Ombea maji ya Tanzania
Ombea Rais Donald Trump
Ombea Rais wetu wa Tanzania(ombea afya, ulinzi,maadui zake wafichuliwe kabla hawajamshambulia)
Ombea majirani zetu Kenya(ombea ulinzi)

Mwaka 2020 wa Yehova Yire, Mungu atainua watumishi wa Mungu wakubwa kati yetu watakaoitikisa dunia.

Mwaka 2020 wa Yehova Yire, Kuna vitu vizuri vitaanza kugunduliwa ndani ya nchi.
Kuna vitu vizuri vitaanza kujifunua kwenye maisha yako binafsi pia.

Mwaka 2020 wa Yehova Yire ni mwaka wa kufunguliwa ufahamu na akili ya kiroho.
Ni mwaka wa kuamshwa kutoka katika usingizi wa kiroho sawa sawa na Zekaria 4:1.

Iwe unataka au hutaki ninaamuru akili yako iamke mwaka huu kwa jina la Yesu!

Mwaka 2020,wa Yehova Yire ni mwaka wa kukamilishiwa muujiza wako.
Mungu atakamilisha miujiza yote kwenye maisha yako kwa jina la Yesu.

Mwaka 2020 wa Yehova Yire watu wakuu na vitu vikuu vinakwenda kuzaliwa kwa jina la Yesu...🙏🙏!

Mwaka 2020,wa Yehova Yire ni mwaka wa FIDIA...Mungu anakwenda kufidia ulichopoteza kwenye maisha yako kwa jina la Yesu!!

Ukombozi church Ministries

Mwaka huu wa 2020,wa Yehovah Yire ni mwaka wa mavuno kwa waliovumilia taabu za miaka mingi kwa jina la Yesu...🙏!!
▪Mwanzo 22:14

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

NENO LA FARAJA KWAAJILI YA MAISHA YAKO

Location

Telephone

Address


P.O.Box 10568 Nyamagana
Mwanza
+255
Other Evangelical Churches in Mwanza (show all)
AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania AICT Nyangulugulu Church - Mwanza Tanzania
Nyangulugulu Mlimani
Mwanza, S.L.P. 7508

Injili, Ibada, Mafundisho ya Neno la Mungu, Maombezi na Utumishi wa Kweli.