Press and Publicity Team- New Vine Church

Press and Publicity Team- New Vine Church

Ukurasa huu una dhamira ya kufikisha mafundisho ya Neno la MUNGU na kusababisha matokeo ya kazi ya MUNGU kujulikana kwenye jamii kubwa ya watu.

New Vine Church is locacted in Nyegezi, Mwanza Tanzania under Senior Pastor Goodluck Kyara. P.O Box 10098, Nyegezi, Mwanza, Tanzania For advice and prayer call +255754435951 Press and publicity team-New Vine Church was established by Senior Pastor Goodluck Kyara for the aim of reaching huge community with the Biblical Truth Teachings and making the fruits of God's work being known by such community all over the world. This page will offer teachings, testimonies, quotes and other church updates for God's Glory.

Operating as usual

Siku zimekaribia mkutano Mkubwa Wa Injili kati Jiji la Mwanza. Mwanza Inuka majira.ya kujiliwa kwako ni haya

Ni mkutano Mkubwa wa Inijli utakaofanyika katika jiji la Mwanza. Tunza tarehe na usipange kukosa.

It is a big crusade that will be held in Mwanza, save the date and miss not.

Ibada ni Hekima ya Mungu kuhifadhi watu wake hata siku ile ya Kristo(Waebrania 10:25).

Karibu katika ibada itakayosababisha mgeuko kwenye maisha yako kwa Nguvu za Roho Mtakatifu na kwa Jina pekee la Yesu Kristo.

Usipange kukosa.

Turning around service.

Kwa AJILI YA USHINDI NA BARAKA ZAKO KILA ENEO LA MAISHA YAKO MWEZI HUU MPYA WA TANO.

Karibu na usikose

SIKU 3 MAALUMU ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA KWA AJILI YAKO MWEZI HUU. tar 3-5/5/2016 ni Kesho jtano-ijumaa. Tunakutana saa 10:00 jioni. NVC

"Hata walipokwisha KUMUOMBA MUNGU, mahali pale walipokusanyika PAKATIKISWA..."

MTU WA MUNGU MCHUNGAJI GOODLUCK KYARA ATAKUONGOZA KATIKA MAOMBI HAYA.

KARIBU KATIKA MWEZI WAKO WA "USHINDI"

⛪Ibada ya Jumapili (23/4/2017), NVC-NYEGEZI (Tema Hotel).
📖SOMO: *AGANO LA MAFANIKIO NA UTELE*
📣MNENAJI: Pastor Goodluck Kyara (Snr pastor of NVC)
☎NVC Pastoral Contact: +255754435951
==================================

*-----UTANGULIZI------*
》Hili ni somo ambalo limelenga katika kulifunua Agano baina ya Mungu na watu wake, ambalo lilikuja kwa njia ya Ibrahimu. Katika msimu huu, Mungu ametujalia kulitazama Agano hilo katika mlengo unao tuonesha namna ambavyo Agano husika limekusudiwa kuwaingiza watu wake, katika viwango vya mafanikio ya kiungu na utele wa hali ya juu.

》Ni muhimu kufahamu kuwa, hakuna Agano ambalo halina vigezo na masharti ambayo hayana budi kuzingatiwa na wana agano husika. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kupata ufahamu utakao tusaidia kuyafunua na kuyazingatia hayo, ili ahadi za Agano hilo ziwe thabiti maishani mwetu.

*-------SOMO-------*
📖Kumb.8:18
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

》Utajiri sio dhambi kwasababu dhambi haitoki kwa Mungu.
》Ikiwa umeokoka, lipo Agano la mafanikio na utele ndani yako.
》Ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe kifedha.
》Kutajirika ni mapenzi ya Mungu.

📖3Yohana 3:2
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

》Mafanikio ya roho yako.
》Mafanikio ya afya yako.
》Mafanikio katika mambo yote.
》Ni muhimu kufahamu kuwa, ili ufanikiwe ni lazima ubadilishe mfumo wako wa kufikiri.
》Mafanikio na utele ni fungu lako.
》Ili ufanikiwe ni lazima usikie kuhusu mafanikio Mara kwa mara,kwasababu IMANI huja kwa kusikia.

📖Mwanzo 13:2
2 Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.

📖Mwanzo 26
13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.
14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.

》Moja ya furushi la wokovu ni mafanikio na utele.
》Umaskini siyo unyenyekevu.

NINI MAANA YA AGANO
》Tafsiri ya kawaida;-
Agano ni mkataba/makubaliano au kifungo cha makubaliano/mkataba.

》Tafsiri ya kiungu;-
Ni kifungo baina ya Mungu muumba mbingu na nchi na kiumbe alicho kiumba Yeye mwenyewe, ambacho ni mwanadamu.
>Agano hili ni la kipekee sana, kwasababu panafanyika makubaliano baina ya pande mbili ambazo zinatofautiana sana kimamlaka.
>Na panapotokea mtu mwingine anakusudia kumwaribu mwenye Agano na Mungu, Mungu humshughulikia mtu huyo, hata uharibifu wake usifanikiwe ama kumrudia mtu aleye ubuni.
>Ikumbukwe kuwa Agano ni zaidi ya ahadi, ijapokuwa ndani ya Agano kuna ahadi au alama ya agano, kama upinde wa mvua ulivyo salia kuwa ni alama baina ya agano la Mungu na Nuhu.
>Agano la Mungu halijali jangwa,ukame wala kipingamizi chochote, cha kimtaa,kitaifa wala kiulimwengu.

》Aina za maagano makuu yaliyopata kufanyika baina ya Mungu na wanadamu, kwakupitia watu mbalimbali:-
1. Baina ya Mungu na Nuhu
2. Baina ya Mungu na Ibrahim.
(Mwanzo 5:17-21)
3. Baina ya Mungu na Musa.
4. Baina ya Mungu na Daudi
5. Baina ya Mungu na watu wake, kwa njia ya Yesu Kristo.

》Katika maagano yaliyopita, yapo ambayo Mungu aliyahamisha na kuyaboresha katika nyakati hizi za Agano jipya, ambapo hata sisi (wa mataifa) tumeingizwa katika urithi wa maagano hayo, kwa imani iliyo ktk Kristo Yesu Bwana wetu. Miongoni mwa maagano hayo ni hilo la Ibrahimu.

📖Wagalatia 3
16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.

》Ikiwa umeokoka na Yesu Kristo ni Bwana na mwokozi wa maisha yako, uwe na uhakika kuwa, urithi wote wa ahadi zote, zitokanazo na Agano la Ibrahimu ni fungu lako HAKIKA.

------*HITIMISHO*------
Hongera kwa kushiriki pamoja nasi katika utangulizi/msingi wa somo hili. Tafadhali usikose kuungana nasi katika mfululizo wa somo hili katika ibada ya Jumapili ijayo (Tar 30/4/2017). Mahali ni Tema hotel-NYEGEZI.

Siku hiyo tutapata neema ya kujifunza Mambo sita au zaidi, ambayo yatakuwezesha kulifanya Agano la mafanikio na utele liwe hai na halisi katika Maisha yako ya kila siku. Kumbuka kuwa Agano la Mungu likihuwika ndani yako, mtikisiko wa kiuchumi na misukosuko mingine inayoikumba jamii yako, haitafanikiwa kukuyumbisha wewe.

》 *KWA MSAADA NA MAELEZO ZAIDI, WASILIANA NASI KWA ANUANI TAJWA HAPO JUU.* Asante.

==================================
NVC - PRESS AND PUBLICITY DEPARTMENT
🌐April 2017

Karibu katika IBADA YA KESHO JUMAPILI, UPOKEE NEEMA NA MSAADA WA BWANA JUU YAKO WAKUKUSAIDIA KUENDELEA MBELE KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YAKO. (utapokea Neema kwa MAOMBI NA MAFUNDISHO).

Ibada ni saa 3:00 [email protected] New Vine Church(HOME OF IMPACT)

Mahali: Nyegezi, Tema hotel, Ukumbi Mkubwa

Welcome to Easter Service

Time: 9:00 a.m Tomorrow

Location: NVC-Tema Hotel , Main Hall Nyegezi, Mwanza.

We love guest.

Karibu kwenye Ibada ya Pasaka

Muda: Saa 3:00 Asubuhi, Kesho

Mahali:NVC-Tema Hotel, Ukumbi mkubwa, Nyegezi, Mwanza.

Tunapenda wageni.

Viewers all over the world we LOVE YOU and INVITE YOU TO WORSHIP WITH US @ New Vine Church ''A home of Impact"

-A place where God is real and Jesus is the centre of our massage.
-The place where will deepen your person walk/relationship with God
-The place where church is a FAMILY
-The place where real u in Christ Jesus will show up
-The place where rises winners and changers
-The place where reigners are risen
-The place where you will connect with your miracle

Join us:Sunday service 9:00 am

Pastor Goodluck Kyara

JESUS IS LORD

Ile siku tuliyokua tukiisubiri, sasa imefika, ni siku ya SIFA KUU kwa Mungu wetu, JEHOVA.

Boaz Danken Ester Nyanda Kabula Noel Mlabwa Lugano Isaiah kelvin webber na Eliya kutoka Arusha watahudumu wakisibdikizwa na MICC praise team na BMCC praise team ukishereheshwa na MC Masanja Mkandamizaji.

Karibu, mualike na rafiki yako.

Mwanza kaa mkao wa kubarikiwa, ni leo saa 9:00 alasiri pale Tema hotel.

Umezaliwa kushinda. Masanja Mkandamizaji tayari ndani nyumba kuendesha semina na kuimba na timu yake.

==================================
⛪Ibada ya Jumapili (02/4/2017), NVC-NYEGEZI (Tema Hotel).
📖SOMO: *UNACHOPASWA KUJUA ILI UWEZE KUISHI MAISHA YENYE MATOKEO*
📣MNENAJI: Mwalimu Victor Deogratius
☎NVC Pastoral Contact: 0754435951
==================================

Utangulizi
*-------*
Isaya 35:1-10
》Soma sura hiyo na upate muda wa kufakari, ili upate kujua Mungu yu ataka kukufunulia siri gani, kutoka mistari hiyo.
*-------*

*YAFUATAYO NI BADHI YA MAMBO YAKUPASAYO KUYAJUA.*
📌1. Jua yakwamba Mungu wako, Yeye ni mwenye nguvu/uweza wote.
》Uweza na nguvu hizo ziliachiliwa juu ya Yesu (mabegani mwake), ili kwa njia ya kumwamini zitufikie sisi tulio fananishwa naye , kwa njia ya kuzaliwa mara ya pili.
📖Isaya 43:15-16
15 Mimi ni Bwana, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.
16 Bwana asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;

📖Luka 1 :37
37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

📖Yeremia 32 : 27
Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?

📌2. Jua kwamba, Mungu ameweka ndani yako; mamlaka, sheria na nguvu ya kuzalisha matokeo unayoyataka.
》Ukisimama katika nafasi yako ya ukuhani, unayo haki ya kutunga sheria yoyote, itoshayo kutoa hukumu kwa hali yoyote inayotokea maishani mwako, na sheria hiyo ndiyo itakayo amua matokeo ya hali yako. Ikiwa hautasimama kwenye nafasi yako, utajikuta unatawaliwa na sheria za ulimwengu huu, ili hali ndani yako una uwezo wa kutunga sheria ambazo ulimwengu utazifuata.

📖Efeso 3:20
20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

📖1Petro 2:9
9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

📖Ufunuo 5:9-10
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

📖Malaki 2:7 (Mika 2:7 sifa za kuhani).
7 Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi.

📌3. Jua kwamba, unatakiwa kuwajibika kwa kila kinachotokea maishani mwako.
》Usimtafute aliyesababisha mazingira usiyoyataka, bali tumia uwezo ambao Mungu amekupa, kubadilisha mazingira husika, Ili yawe kama vile utakavyo wewe.
》Ili Mungu akuinulie watu wa kushiriki ktk utimilifu wa kusudi lako, ni lazima ufike mahali pa kutambua kuwa jambo husika ni la kwako wewe na wewe ndiwe unayetakiwa kulikamilisha. Baada ya kujitambua kihivyo, ndiposa Mungu huinua watu wa kukufikisha katika hatima ya jambo husika.
》Mungu hutafuta watu wawajibikaji.
》Mungu havutiwi na watu walalamishi tu, ambao mioyoni mwao hawako tayari kuwajibika bali kulalamika tu na kutafuta watu wa kuwalaumu kuhusu hali fulani.

📖Ezra 10:4
4 Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.

📖Ezekiel 22:30
30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.

📌4. Usikumbuke hasara, Mungu ana suluhisho ktk njia panda yako.
》Mara nyingi watu husalia ktk hali za kukwama kwao, kwasababu hupoteza muda mwingi ktk kutafakari kuhusu namna walivyo anguka/kwama na matokeo yake, badala ya kutumia muda huo ktk kutafakari kuhusu namna ya kupata suluhu ya kuuepuka/kuchomoka kutoka ktk mkwamo/hasara/anguko lako.

📖Isaya 43:18-21
15 Mimi ni Bwana, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.
16 Bwana asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu.

📌5. Jua kuwa, Mungu anaweza kukujenga Mara ya pili na kurejeza ustawi wako.
》Mungu yu aweza kujenga kwa upya, kitu chochote kinachokuhusu, ambacho kina hali ya kubomoka au kupoteza mwelekeo.

📖Yeremia 31:3-5
3 Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
4 Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.
5 Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake.

📖Yoeli 2:25-27 (1:4)
25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
>>>>>>>>>>>>>>>

The days are countable now, siku 2 zimebaki kuanza semina siku ya Ijumaa na Mchungaji Goodluck Kyara na mchungaji Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji.

Semina hii itafuatiwa na tamasha kubwa la kusifu na kuabudu likiongozwa na waimbani kutoka Arusha( Jiji la Sifa) na Mwanza( Jiji la maarifa).

Kabula Noel Mlabwa atakuwepo kuhudumu. Karibu sana.

Anaitwa Kelvin Weber kutoka Arusha maarufu kama Jiji la sifa( city of Praise)huyu naye atakuwepo kwenye Tamasha la sifa kuu. Karibu uhudumiwe na Roho Mtakatifu kupitia chombo hiki kilichoaminiwa(trusted vessel).

Ikitanguliwa na semina kuanzia tarehe 7-8

Hutabaki ulivyokua. Mkaribishe na rafiki yako. Maelezo zaidi yako.

Habari Njema watu wa Mwanza na wilaya zake, Kanisa la New Vine linakuletea tamasha linalojulikana kama" Sifa Kuu"

Mwimbaji Ester Nyanda kutoka Mwanza atahudumu na kukusogeza Enzini pa Mungu huku ukivunjwa mbavu na mchungaji Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji.

Yaani itakua Sifa na kicheko na furaha.

==================================
⛪Ibada ya Jumapili (19/3/2017), NVC-NYEGEZI (Tema Hotel).
📖SOMO: *FAIDA ZA KUMTUMIKIA MUNGU*
📣MNENAJI: Pastor Goodluck Kyara (Snr pastor of NVC)
☎NVC Pastoral Contact: 0754435951
==================================

*-----UTANGULIZI-----*
》Mtembeo wa nguvu za Mungu umekuwa dhahiri sana ktk ibada yetu ya leo, mtu wa Mungu Pastor Goodluck aliianza huduma ya madhabahu kwa kuiachilia hiyo nguvu kubwa ili iweze kuwaponya na kuwafungua watu, hakika tumemuona Bwana akiwafungua watu wengi walio hudhuria ibadani ambao walionewa na mwovu kwa namna mbalimbali.
》Ushuhuda wa namna ambavyo Mungu alihusika kuifanikisha safari ya Pastor Goodluck pamoja na timu teule kutoka Mwanza ambao walipata neema ya kuteuliwa kwenda kushiriki mazishi ya mama mzazi wa mtumishi Mwakasege.
==================================

》Ktk somo lililopita tuliangalia namna ambavyo hatujaokolewa hivihivi tu, bali tumeokolewa kwa kusudi maalumu. Ijapokuwa lengo la utumishi ni kuujenga ufalme, lakini kila mtu ana kusudi tofauti na mtu mwingine.
》Kusudi la Mungu kukuona na kukuacha uendelee kuishi na kukuepusha na mabaya mengi, ni kwasababu Mungu anataka kukutumia/kukuagiza umtumikie.
》Ni muhimu kufahamu kuwa kila mtu ni wa kipekee sana, kama vile ambavyo alama za vidole vyetu zinavyo tofautiana, vivyo hivyo makusudi yetu hayafanani.

*SOMO LENYEWE:*
*-------------*
》Je Mungu ana mtazamo gani kumuelekea mtu anaye mtumikia Yeye/ Je kuna faida gani ktk kumtumikia Mungu?

📖Mathayo 10:9-10
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake.

》Mungu yuko kinyume na kutumika bure/pasipo malipo stahiki.
》Maandiko yanatanabaisha kuwa: Mungu aliwambia wana wa Israel kuwa
> *"sikuwaita mkanitumikie bure"*
> *"nanyi mtamtumikia Mungu wenu naye atakibarikia chakula chenu"*
> *"kila mtendakazi anastahili posho lake"*

》Ni muhimu kufahamu kuwa posho ya Bwana ni zaidi ya mshahara wako, hiyo inatosha/inaweza kufanya mambo makubwa ambayo hayawezi kufanyika kwa mshahara ambao wengi wanautegemea kuendeshea maisha ya kila leo. Kwasababu hiyo, mtu amtumikiaye Mungu, daima huwa na mafanikio makubwa kuliko watu wa aina yake, kwasababu yeye hataishi kwa kutegemea mshahara kama wengine.

*FAIDA ZA KUMTUMIKIA BWANA*
1. Mbingu zinakufungukia na baraka (nguvu ya kukuwezesha kufanikiwa ) ya Bwana inakuwa juu yako na kusababisha mafanikio ya kipekee.

📖Kumb 11:13-15
13 Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote,
14 ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako.
15 Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.

》Kumtumikia Mungu kunafungua mbingu ili iachilie mafanikio kukujia, kuto mtumikia Mungu/ kutumikia miungu mingine kunasababisha mbingu kufungwa juu yako.

2. Bwana huzidi kukutengeneza ili uzidi kuzaa zaidi.
📖Yohana 15:1-2
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

3. Uwepo wa Bwana hutembea nawe na kutenda kazi/hudhihirika ktk maisha yako.

Marko 16:20
📖20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]

》Kila kumtumikia Mungu, kunafungua mtembeo wa nguvu zake.

4. Unapokea neema ya kuinuliwa na kutukuzwa

📖Isaya 52:13
13 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.

5. Kila silaha na hila za adui dhidi yako, haziwezi kufanikiwa kwako.

📖Isaya 54 :17
17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.

6. Kumtumikia Bwana hufanya maombi yako kujibiwa.

📖Yohana 15:16
16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

》Nguvu iliyoko ktk kumtumikia Bwana ndiyo iliyo sababisha maombi ya Hezekia kukataa kufa yasikiwe na yajibike bila pingamizi lolote. (2 Wafalme 20 : 1-)

7. Kumtumikia Mungu husababisha huduma ya malaika kuambatana nawe.

》Zipi habari nyingi sana kwenye maandiko ambazo zina ainisha namna ambavyo watu mbalimbali waliomtumikia Bwana waliweza kuachilia au kupokea huduma ya utendaji kazi wa malaika ktk nyakati tofautitofauti.

*HITIMISHO:*
Vigezo vya utumishi unaokubalika mbele za Bwana ni:-
*1. Kumtumikia Mungu sio wanadamu*
*2. Kutumika kwa moyo wote na bidii kuu.*
*3. Tumika kwa furaha bila manung'uniko.*

》Ni muhimu kufahamu kuwa faida hizi hazimuhusu kila mtu aliye ndani ya kanisa, bali wale wanaomtumikia Mungu tu.
》Ni mapenzi ya Mungu kuwa kila aliye muokoa awe katika fungu la kunufaika na faida hizi. Kwasababu hiyo, ni jambo la muhimu sana kwa kila mtu ndani ya kanisa, kuuelekeza moyo wake ktk kumtumikia Mungu kwa namna yoyote ambayo moyo wako wakusukuma kuanza nayo.
》Ni ukweli usiopingika kuwa, hakuna mtu ambaye atathubutu kumtumikia Mungu na akabaki kuwa mtu wa kawaida.

*ANGALIZO:*
》Chunga sana utumishi wako, ikiwa unatumika ili mchungaji wako akuone au washirika wenzio, tambua kuwa utumishi wako hautapata posho kutoka kwa Bwana, kwasababu Bwana hutoa posho kwa wanaomtumikia Yeye, na sio wanaotumika ili watazamwe na watu.
==================================
NVC - PRESS AND PUBLICITY DEPARTMENT
🌐 *March 2017*

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


NYEGEZI
Mwanza
1345

Opening Hours

Thursday 16:30 - 18:30
Sunday 09:00 - 12:00
Other Religious Organizations in Mwanza (show all)
Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania
Mbeya
Mwanza, DODOMA, DAR-ES-SALAAM

Lengo ni kumtumikia Mungu bila kujari madhebu yetu kama Vijana. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu. Zaburi 60:12

Africa Inland Church Tanzania-AICT Africa Inland Church Tanzania-AICT
Mwanza

This is an official page of Africa Inland Church-Tanzania[AICT]

ELVD - ELCT ELVD - ELCT
P.O. Box 423
Mwanza

East of Lake Victoria Diocese (ELVD) is part of the Lutheran Church in Tanzania (ELCT). Our home base is Mwanza, next to Lake Victoria.

Lumala Seventh-Day Adventist Church Lumala Seventh-Day Adventist Church
Lumala
Mwanza, 1724

Tumeitwa kuwa wajumbe wa Mungu duniani. Karibu tumwabudu na kumtumikia Mungu kwa kicho.

Efatha Ministry Mwanza Efatha Ministry Mwanza
P.o.box
Mwanza, 11626

The Official Efatha Ministry MWANZA page. You tube: https://youtu.be/vb7qVVxIfO8 http://www.instagram.com/efathamwanza

Efatha-Mwanza Efatha-Mwanza
Mwanza
Mwanza, P.O.BOX 11626

Efatha mwanza is located at nyakato nundu B in we are among the church which are growing very fast. We are running the vision and mission of Apostle J.E.M

Bujora Sukuma Museum Bujora Sukuma Museum
Bujora Cultural Centre (Sukuma Museum)
Mwanza, 76

Visit us and discover the traditional and contemporary life of the Sukuma people. Tour the museum and join us for the annual Bulabo Dance Festival in June!

USCF SAUT Mwanza USCF SAUT Mwanza
St. Augustine University
Mwanza

USCF SAUT ni Umoja/ Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ujulikanao kama UKWATA kwa shule za sekondari na vyuo vya kati (colleges).

Huduma ya Maandiko Huduma ya Maandiko
P.O. Box 2017
Mwanza, 25528

Worlds Largest Christian Bible Study site. All available as a free download .

New Vine Church New Vine Church
Gloryland,Nyanembe-Buhongwa
Mwanza, +255

NVC is a Church committed to see the raising of great Godly generation with the aim of making impact, changing lives and influence the World.

Jesus Restoration Centre - JRC Church Jesus Restoration Centre - JRC Church
Kirumba
Mwanza, 255

Jesus Restoration Centre ni kanisa la kipentekoste lililopo chini ya uongozi wa Mchungaji George Mukabwa. Kanisa hili lilianza Novemba, 2011.

UHURU UHURU
ISAMILO
Mwanza

Uhuru wa mawazo fikra.kira mtu ana uhuru wa point ispokuwa usiende kinyume na sheri.

About   Privacy   Login C