New Vine Church

New Vine Church

NVC is a Church committed to see the raising of great Godly generation with the aim of making impact, changing lives and influence the World.

Mission: Rising of Godly generation

2020 MWAKA WANGU WA KUWEKWA MAHALI PANGU PA JUU

(Kwa NVC,wana NVC na yeyote aliyeunganishwa nasi na kuamini katika neema na utumishi huu tulioitwa na Bwana.BASI POKEA NEEMA YA KUWEKWA MAHALI PAKO PA JUU KTK JINA LA YESU)

Maandiko yafuatayo ni muhimu sana kuyasoma na kumuomba Roho mtakatifu akuonyeshe unachotakiwa kuona kwa Mwaka huu.kumbuka ndio maandiko ya Neno la Mwaka.(Yanaelezea neno la Mwaka)👇

ZABURI.18:31-33

31 Maana ni nani aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?
32 Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.
33 Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.

HAB.3:19.

19 YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.

2Sam 22:32-34.

MUNGU AWABARI,HAPPY NEW YEAR 2020.

KARIBU KATIKA MAJIRA YAKO YA "KUWEKWA MAHALI PAKO PA JUU"

Pst Goodluck Kyara
New Vine Church.

Ibada ya utukufu,jumapili iliyopita,hapa Kanisa la New Vine.Tunamshukuru Mungu kwa mkono wake juu ya huduma hii.

Glorious last sunday service @New Vine Church "A home of Impact".Gloryland-Nyanembe,Buhongwa-Mwanza.

We had Bishop Amos Hulilo and mama.It was great time to have this generals of Jesus in this house.Thank u sir and mama for accepting our invitation.

JESUS IS LORD.

#Myyeartoshine2019
#Gloryland

New Vine Church's cover photo

Pastor Goodluck Kyara

Last Sunday service/ibada ya jumapili iliyopita.

Karibu jumapili tunapoendelea na:-

Somo "VITA AINA I4 UNAZOPASWA KUZIPIGANA NA KUZISHINDA ILI UTHIBITIKE NA KUFANIKIWA KILA ENEO LA MAISHA YAKO MWAKA HUU 20I8"

KARIBU KANISANI,KILA:-

JUMAPILI SAA 3:00 asbh

TUNAPOENDELEA NA SOMO HILI katika VITA YA 6

@New Vine-Temahotel Nyegezi Mwanza.

[01/09/18]   MAOMBI YA KUATAMIA.
Mfululizo wa 1.

Karibu katika mfululizo wa somo hili nzuri la maombi ya "KUATAMIA".By Pastor Goodluck

andiko letu la msingi litakuwa ni: 1Falme 18:41-46

41 Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele.
42 Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.

Kabla sijaanza kuchambua maandiko hayo hapo juu kwa muktadha ya maombi ya kuatamia hebu kwanza nielezee kuhusu haya ni maombi ya namna gani.

-Maombi ya kuatamia, haya sio maombi ya kawaida kawaida bali ni maombi ya kusababisha jambo jipya kuzaliwa. Ni maombi ya kama vile kuku anapoatamia mayai yake huyaatamia mpaka atakapoona matokea yaani vifaranga.

-Ni maombi ya kusababisha jambo/mambo mapya kutokea katika maisha yako, familia yako, ukoo wako, watoto wako,masomo yako, biashara yako, katika mwaka wako wa 2018,katika hatima yako.

Ni aina ya maombi ya "kuatamia" kitu cha ki Mungu ndani yako mpaka kidhihirike katika ulimwengu unaonekana.

Ni maombi ya kuatamia kwa njia ya maombi ajenda ya ki Mungu katika familia yako, watoto wako, ndoa yako, huduma yako mpaka ajenda hiyo itokee/ithibitike.

Aina hii ya maombi au shule hii ya maombi inaonekana katika maeneo kadhaa ya biblia lakini tutachambua kidogo kidogo kadri Bwana Yesu anavyotupatia nafasi.

Sasa kwa maandiko tuliyoanza nayo hapo juu hebu tuanze kuangalia shule hii.

1.Eliya
Eliya kama Nabii wa Bwana ni mmoja wa watu walio ijua vizuri shule hii ya maombi ya kuatamia.

Maandiko tuliyosoma hapo juu ya kitabu cha 1 falme 18:41-46

Utaona siri kubwa ya mafanikio ya Eliya. Hii ni baada ya miaka mingi takribani mitatu na nusu mvua wala tone la mvua halikuonekana katika nchi ya Israel hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba watu walinunua na kula mavi ya njiwa, ilifika kipindi hata wanawake wakawachemsha watoto wao ili kuwala,mifugo ilikufa, uchumi ulianguka hali ilikuwa ya kukatisha tamaa. Katika hali hii mbaya Nabii wa Bwana akasikia sauti ya mvua tele. 1falme 18: 41 "Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele".

Hili ni neno la matumaini mapya lilikuja kupitia Mtu wa Mungu Eliya.

🤜Mpendwa mimi sijui nini unapitia katika maisha yako, lakini ninazo habari njema kwako kwamba unaweza kubadilisha jambo hilo kwa maombi ya kuatamia sauti ya Bwana katika maisha.

Tunaona baada ya Eliya kusema maneno yale ya kuwa anasikia sauti ya mvua tele. Hakuenda kulala bali biblia inasema:- "Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini".

Nini alichoenda kufanya?, ni "KUATAMIA" kwa maombi ile sauti ya mvua tele aliyoisikia katika ulimwengu wa roho,ili asiishie tu kubaki na sauti ya mvua bali mvua halisi inyeshe.

Utaona hilo biblia inaposema alipanda mlimani akajikunja mpaka nchi,uso wake ukakutana magoti yake.Mpendwa, Eliya alijua unaweza ukabaki tu na sauti ya ahadi ya Bwana na usione uhalisia wa ahadi hiyo katika maisha yako ya mwilini. Na Eliya hakuwa tayari kwa hilo.

Na hili ndio kosa watu wengi hufanya. Watu wengi wamebaki katika sauti ya mvua tele ila sio udhihirisho wa mvua halisi.sauti ya utukufu tele ila sio udhihirisho wa utukufu halisi, sauti ya ushindi tete ila sio udhihirisho wa ushindi halisi.

Sijui wewe umesikia sauti ya ushindi na hata baraka zipi kwenye maisha yako, ila kwa kipindi kirefu umebaki tu kushangilia sauti ya mvua tele bila kuona uhalisia wa mvua hiyo katika maisha yako?.Hebu mwaka huu 2018 iwe tofauti.

OMBI LA KUOMBA KWA AJILI YAKO:

Ee Mungu nipe Neema mwaka huu 2018,nione udhihirisho wa ahadi zako katika maisha yangu, ni siishie tu kushangilia sauti ya ahadi bila udhihirisho.

Endelea kufuatilia mfululizo unaofuata wa somo hili....

Pastor Goodluck Kyara
New Vine Church
"A home of Impact"
±255754435951

2018 "MWAKA WA KUTHIBITISHWA NA BWANA"
2018 "THE YEAR OF ESTABLISHMENTS"

Zab 89:20-21. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

Psalms 89:20-21. I have found David my servant; with my holy oil have I anointed him:
With whom my hand shall be established: mine arm also shall strengthen him.

New Vine Church

New Vine Church's cover photo

Sunday service @ New Vine Church

TO GOD BE ALL THE GLORY FOR THE GREAT HARVEST OF SOULS.
with Evangelist Kevin Greer and Pastor Goodluck Kyara
Great move of God,many soul where saved,healed and blessed with Jesus. Buhongwa,the southern part of Mwanza city will never remain the same.
I and entire family of New Vine Church were privileged to host this crusade

Photos from New Vine Church's post

New Vine Church's cover photo

New Vine Church's cover photo

We are humbled and honored for this great men of God in different times and from different places visit New Vine Church Construction.Pastor George & mama. My mama Mrs Joram Meena,Uncle Paul Meena.My neighbor Mr Reymond.Pastor Moses Hosea.

New Vine Church's cover photo

YESU NI BWANA /JESUS IS LORD.

Welcome this coming sunday
Karibu ibadani jumapili ,tutafurahi kukuona.Kumbuka Mungu anakusudi na maisha yako.

Timeline Photos

Sunday service 23/4/[email protected] New Vine Church

somo: AGANO LA MAFANIKIO NA UTELE

With pastor Goodluck Kyara

[04/24/17]   It is NORMAL to be challenged, but it is UNSCRIPTURAL to be defeated.
Psalm 34:19, Romans 8:35.

Dr David Oyedepo.

SUNDAY SERVICE 9/4/2017 @ New Vine Church with pastor Emanuel Mgaya

==================================
⛪Ibada ya Jumapili (02/4/2017), NVC-NYEGEZI (Tema Hotel).
📖SOMO: *UNACHOPASWA KUJUA ILI UWEZE KUISHI MAISHA YENYE MATOKEO*
📣MNENAJI: Mwalimu Victor Deogratius
☎NVC Pastoral Contact: 0754435951
==================================

Utangulizi
*-------*
Isaya 35:1-10
》Soma sura hiyo na upate muda wa kufakari, ili upate kujua Mungu yu ataka kukufunulia siri gani, kutoka mistari hiyo.
*-------*

*YAFUATAYO NI BADHI YA MAMBO YAKUPASAYO KUYAJUA.*
📌1. Jua yakwamba Mungu wako, Yeye ni mwenye nguvu/uweza wote.
》Uweza na nguvu hizo ziliachiliwa juu ya Yesu (mabegani mwake), ili kwa njia ya kumwamini zitufikie sisi tulio fananishwa naye , kwa njia ya kuzaliwa mara ya pili.
📖Isaya 43:15-16
15 Mimi ni Bwana, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.
16 Bwana asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;

📖Luka 1 :37
37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

📖Yeremia 32 : 27
Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?

📌2. Jua kwamba, Mungu ameweka ndani yako; mamlaka, sheria na nguvu ya kuzalisha matokeo unayoyataka.
》Ukisimama katika nafasi yako ya ukuhani, unayo haki ya kutunga sheria yoyote, itoshayo kutoa hukumu kwa hali yoyote inayotokea maishani mwako, na sheria hiyo ndiyo itakayo amua matokeo ya hali yako. Ikiwa hautasimama kwenye nafasi yako, utajikuta unatawaliwa na sheria za ulimwengu huu, ili hali ndani yako una uwezo wa kutunga sheria ambazo ulimwengu utazifuata.

📖Efeso 3:20
20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

📖1Petro 2:9
9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

📖Ufunuo 5:9-10
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

📖Malaki 2:7 (Mika 2:7 sifa za kuhani).
7 Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi.

📌3. Jua kwamba, unatakiwa kuwajibika kwa kila kinachotokea maishani mwako.
》Usimtafute aliyesababisha mazingira usiyoyataka, bali tumia uwezo ambao Mungu amekupa, kubadilisha mazingira husika, Ili yawe kama vile utakavyo wewe.
》Ili Mungu akuinulie watu wa kushiriki ktk utimilifu wa kusudi lako, ni lazima ufike mahali pa kutambua kuwa jambo husika ni la kwako wewe na wewe ndiwe unayetakiwa kulikamilisha. Baada ya kujitambua kihivyo, ndiposa Mungu huinua watu wa kukufikisha katika hatima ya jambo husika.
》Mungu hutafuta watu wawajibikaji.
》Mungu havutiwi na watu walalamishi tu, ambao mioyoni mwao hawako tayari kuwajibika bali kulalamika tu na kutafuta watu wa kuwalaumu kuhusu hali fulani.

📖Ezra 10:4
4 Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.

📖Ezekiel 22:30
30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.

📌4. Usikumbuke hasara, Mungu ana suluhisho ktk njia panda yako.
》Mara nyingi watu husalia ktk hali za kukwama kwao, kwasababu hupoteza muda mwingi ktk kutafakari kuhusu namna walivyo anguka/kwama na matokeo yake, badala ya kutumia muda huo ktk kutafakari kuhusu namna ya kupata suluhu ya kuuepuka/kuchomoka kutoka ktk mkwamo/hasara/anguko lako.

📖Isaya 43:18-21
15 Mimi ni Bwana, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.
16 Bwana asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu.

📌5. Jua kuwa, Mungu anaweza kukujenga Mara ya pili na kurejeza ustawi wako.
》Mungu yu aweza kujenga kwa upya, kitu chochote kinachokuhusu, ambacho kina hali ya kubomoka au kupoteza mwelekeo.

📖Yeremia 31:3-5
3 Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
4 Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.
5 Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake.

📖Yoeli 2:25-27 (1:4)
25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
>>>>>>>>>>>>>>>

Great sunday service 26/3/2017 @New Vine Church. With Mrs Pastor Goodluck Kyara(Ziada Kyara).

Sunday service @ New Vine Church

Timeline Photos

Sunday service @ New Vine Church.

Timeline Photos

Cell Leaders giving testimonies on reaching out campaign (OPERATION MAVUNO)

Viongozi wa cells wakitoa ushuhuda juu ya kampeni ya kuleta watu kwa Yesu.(OPARESHENI MAVUNO)

# Sunday service#ibada jumapili#
Somo:
"KUPIGANA NA WENYEJI WA NCHI" (vita vya pili unavyopaswa kivishinda)

@ New Vine Church

Sunday service @ New Vine Church

Timeline Photos

# FROM OUR LOVELY USHERS#

All things are possible with GOD.and possible to whom believes.
Join us this wonderful special Sunday morning as we wind up our 21 days of fasting and prayer.is going to be great day as we break the bread and share the cup of our Lord Jesus together.

SERMON:
3 BATTLES YOU SHOULD WIN IN LIFE

TIME: 9:00 am
New Vine-Temahotel-Nyegezi Mwanza.

Timeline Photos

==================================
⛪Ibada ya Jumapili (15/1/2017), NVC-NYEGEZI (Tema).
📖SOMO: *AINA TATU ZA VITA UNAZOPASWA KUZISHINDA ILI UFANIKIWE.*
📣MNENAJI: Pastor (Snr) Goodluck Kyara
☎NVC Pastoral Contact: 0754435951
==================================

*UTANGULIZI:*
*-------------*
♡Kuhusu mkakati wa maombi ya kufunga.
》Maombi ni muhimu sana katika maisha yetu, kwa sababu kwa njia hiyo, mambo mengi huumbika/husababishwa kutokea.

》Mambo huwa hayatokei tu bali husababishwa kutokea. (Kanuni ya kwanza ya mwanasayansi aitwaye Newton inasema kuwa; *"Daima vitu vyote husalia katika hali zake zilezile, hadi pale kani msukumo/nguvu nyingine itakapokuja na kukibadilishia uelekeo"*. Vivyo hivyo katika maisha hakuna mabadiliko yatakayotokea pasipo kusababishwa). Maombi ni miongoni mwa mambo makuu yanayozalisha nguvu ya mabadiliko, haiwezekani ukajitoa kuomba kwa imani katika jina la Yesu na mambo yako yakabaki vilevile.

》Kumbuka kuwa kuomba huvunja vifungo/nira za uovu maishani mwa muombaji. Kwasababu hiyo, sisi tumeamua kuanza mwaka huu kwa kumkabidhi Mungu mambo yetu ya mwaka huu kwa njia ya maombi. Tuna siku 21 za maombi ya mfungo, na leo tuko siku ya 8, bado unayo nafasi ya kujumuika pamoja nasi, kwahiyo tunakukaribisha sana. Karibu na Mungu akubariki sana.

*AINA TATU ZA VITA UNAZOPASWA KUZISHINDA ILI UFANIKIWE.*
1. Vita dhidi ya adui aitwaye mimi.
2. Vita dhidi ya Wenyeji wa nchi/mji.
3. Vita vizuri vya imani.

*1. VITA DHIDI YA ADUI AITWAYE MIMI*
》Vita dhidi ya adui aitwaye mimi, inalenga kupigana na mawazo au fikra alizo nazo mtu binafsi kujihusu yeye mwenyewe.

》Vita dhidi ya adui aitwaye mimi ni vita kuu kuliko zote, kwasababu *"aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo"* (mithali 23:7)

》Kwasababu hiyo basi, Mungu hawezi kufanya zaidi ya unavyowaza, maana Yeye hutazama nia zetu, yaani mawazo/nguvu ya imani iliyo ndani yetu. Hivyo husema kuwa, Yeye hutupa sawa na Imani zetu.

》Tunapo zungumza kuhusu mwanajeshi, hatuzungumzii kuhusu mtu tu, bali tunazungumza kuhusu mawazo ya kijeshi yaliyoingizwa ndani ya mtu husika. Mawazo yale ya kijeshi ndiyo humpatia mtu uwezo wa kuwa mwanajeshi na kumwacha mwingine akibaki kuwa raia wa kawaida tu. Vivyo hivyo kiongozi/dereva wa gari moshi, sio mtu tu, kwasababu hata wewe ni mtu pia, lakini ukipewa uliongoze lile, hutoweza. Kwahiyo muongoza gari moshi ni mawazo/fikra zilizomo ndani ya mtu mahususi aliyeandaliwa kwaajili ya kazi hiyo.

OMBI LA KINABII
*Mwaka huu Bwana akujalie mawazo chanya, yatakayotosha kukusaidia kuyaendesha mambo mbalimbali yaliyo mbele yako kwa mwaka huu, katika jina la Yesu.*
(pokea tamko hili kwa imani, na endelea kumsihi Mungu kuhusu ombi hili kwa wakati wako).

》 Neno linaposema *"tusinie makuu kuliko tuwezavyo"*. Kwa lugha nyingine hapa anamaanisha kuwa tusinie zaidi ya tunavyo amini. Kumbuka kuwa Imani ni jumla ya nguvu itokanayo na mawazo/kile mtu anachokiona kabla hakijatokea, kwasababu kila tukionacho leo kwa macho ya nyama, hapo awali kilikuwa ni wazo ndani ya mtu fulani. Kwahiyo tunapaswa kunia/kutaka/kuomba sawasawa na imani zetu. Kama tunahitaji zaidi, basi hatuna budi kuinua zaidi imani zetu.

》Ndugu yangu, ni muhimu kutambua kuwa, adui yako wa kwanza kabisa ni wewe mwenyewe, sio shetani, jirani au ndugu yako. Kumbuka kuwa ninapozungumza kuhusu wewe, namaanisha mtazamo wako. Mitazamo mibovu ndio imekusababishia matatizo mengi maishani mwako.

》Daima Mungu hushughulika na mitazamo ya watu anaotaka kuwatumia kabla hajaanza kuwatumia. Kielelezo cha Gidioni kinatupatia picha hiyo. Malaika alipomtokea Gidion akiwa kule mafichoni, alianza kumtengeneza Kwanza mtazamo wake, kwa kumbadilisha namna anavyojichukulia. Tazama akamwita kuwa *"YEYE NI SHUJAA"* , hapo ndipo shule ikaanza. (Waamuzi 6 :12)

》Tatizo sio shetani, bali ni mawazo/mitazamo tuliyonayo kuhusu sisi wenyewe. Kama hatuta shughulikia mitazamo yetu katika mwaka huu, tutaendelea kubaki vilevile kama mwaka jana. Ni Muhimu tupanie kumpa Mungu nafasi ya kubadilisha mitazamo yetu kwa njia ya neno lake ili tufanikiwe kuingia viwango vingine.
Rumi 12:2 (nia ni mtazamo/mawazo yako).

Kwa ufafanuzi wa ziada, naomba tujifunze kidogo kuhusu kanuni mbili za kivita ambazo zilibuniwa na mtu aitwaye SUN TZU, ambaye ni mwanadiplomasia wa masuala ya kivita mwenye asili ya uchina, ambaye kanuni zake hutumiwa na majeshi karibi yote ulimwenguni.

1. *"Sanaa kuu ya vita ni kumshinda adui pasipo kupambana naye."*
♡Uhalisia wa kanuni hii katika maisha yetu kwa kifupi uko kama ifuatavyo:

》Shetani maranyingi hutumia mbinu hii kama Cole Goliath alivyomshinda Sauli na jeshi lake. Sanaa hii maranyingi huvamia mawazo ya adui na kumfanya akose nguvu ya kupambana hata kushindwa vita.
》Watu wengi wameshindwa vita zao hata kabla hawajaanza kuzipigana.

2. *"Sanaa kubwa ya vita ni kumshinda adui kabla hujaingia kupambana naye"*.
♡Uhalisia wa kanuni hii katika maisha yetu kwa kifupi uko kama ifuatavyo:

》Mtazamo wako ukiwa hasi ( umejaa mashaka/hofu), unakuwa umeshindwa kabla ya kupambana, ukiwa chanya (umejaa imani) unakuwa umeshinda kabla ya kupambana.

》Hatuendi kwa kuona, bali tunaenda kwa imani. Huu ni mwaka wa kulitanguliza Neno la Bwana katika kila hali tunayoikabili. Neno ni Bwana hutupa kushinda hata kabla hatujaanza kupambana kwakuwa hutupa ujasili wa kushinda zaidi ya kushinda katika Kristo Yesu, yaani hutupa kujiona na kufanya kama mashujaa / wana wa aliye juu.

Kumbuka:
Mwana mpotevu aliendelea kula makombo ya mifugo hadi siku ile alipobadilisha mtazamo wake. Ni muhimu kubadilisha mitazamo yetu ndugu zangu. Changamoto hazitakoma kutujia, lakini zitakapokuja tunapaswa tuzikabili kwa mtazamo chanya kama alivyofanya Daudi wakati anamkabili Goliati.

NVC - PRESS AND PUBLICITY DEPARTMENT
🌐15 January 2017

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Address

Gloryland,Nyanembe-Buhongwa
Mwanza
+255
Other Religious Organizations in Mwanza (show all)
Melkizedeki Hope International Melkizedeki Hope International
Plot No. 114 Block "B" Nyakato National, P.O. Box 1844
Mwanza, 25528

We support orphans and offer access to basic needs to the poor. Please give food, clothes, shoes, bedding or education to the needy.

Peter Mbajije victory - Angaza Gospel Peter Mbajije victory - Angaza Gospel
Tanzania
Mwanza, 83

Utukufu una yeye aliyezifanya mbingu na Nchi.What'sp no (+255) 752 107 183 Email:[email protected]

Kyaruzi Tz Kyaruzi Tz
Ngara
Mwanza, 00000

If you don't have an alternative don't criticise

UHURU UHURU
ISAMILO
Mwanza

Uhuru wa mawazo fikra.kira mtu ana uhuru wa point ispokuwa usiende kinyume na sheri.

Nyakato Seventh Day Adventist Church Mwanza Tanzania. Nyakato Seventh Day Adventist Church Mwanza Tanzania.
Nyakato - Mwanza, Tanzania
Mwanza

St.dominic Pastoral Centre Archdiocise of Mwanza St.dominic Pastoral Centre Archdiocise of Mwanza
PO Box1527 MWANZA TANZANIA
Mwanza, +255

www.stdominicpastoral.or.tz

Africa Inland Church Tanzania - AICT Africa Inland Church Tanzania - AICT
P.O Box 905 Makongoro Street, Plot No 66
Mwanza

Kanisa linalothubutu katika kutimiza utume kamili kwa utukufu wa Mungu (a daring church that carries out a holistic mission to the Glory of God).

ELVD - ELCT ELVD - ELCT
P.O. Box 423
Mwanza

East of Lake Victoria Diocese (ELVD) is part of the Lutheran Church in Tanzania (ELCT). Our home base is Mwanza, next to Lake Victoria.

Efatha-Mwanza Efatha-Mwanza
Mwanza
Mwanza, P.O.BOX 11626

Efatha mwanza is located at nyakato nundu B in we are among the church which are growing very fast. We are running the vision and mission of Apostle J.E.M

Jesus Restoration Centre - JRC Church Jesus Restoration Centre - JRC Church
Kirumba
Mwanza, 255

Jesus Restoration Centre ni kanisa la kipentekoste lililopo chini ya uongozi wa Mchungaji George Mukabwa. Kanisa hili lilianza Novemba, 2011.