Efatha Ministry Mbinga

Efatha Ministry Mbinga

Comments

SIMBA
Karibu kufuatilia Ibada ya Jumapili (26 JAN 2019) inayorushwa moja kwa moja katika vituo vyetu vyote vya EFATHA. Fuatilia Ibada hii inayoongozwa na Mch. Betson Kikoti kupitia TRENET TV Youtube: https://youtu.be/3vW1Ih4ZN7o Online Radio: www.mixlr.com/efatha-ministry
karibu sana ibadani efatha Mbinga
Masumbuko
Wewe jinsi ulivyo tu ni muujiza, MTU ASIKUDHARAU, Wewe ni kazi ya mikono mitakatifu ya Mungu. Karibu Efatha mbinga tumsifu MUNGU
Halelluyah wanaefathawote ninamtukuza yesuwa efatha mana ndiye anayeni2nza mpaka hapa nilipofikia.
HALELUYA: Ukimpa MUNGU moyo wako atasamehe dhambi zako zote na atakupa uzima na kurejesha ujana wako upya. Maisha ya umilele sio kuokoka tu kama watu wengine wanavyodhani, la hasha! Bali ni namna unavyoutoa uhai wako kwa Mungu. Yohana 17:3"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Unapotoa moyo wako kwake unakuwa umejitoa mwenyewe mzima na vyote ulivyo navyo kwenye mwili na maisha yako, ikiwemo wazazi, mke, mume, watoto wako na mali zako. Unatoa wazazi wako kwa sababu wamekuzaa. Vile vile mke au mume kwa sababu ni wako. Kwa hiyo ukitoa moyo wako kwa Mungu, unakuwa umetoa kilakitu ulicho nacho, naye hukusanya kila kitu kinachohitajika kwenye maisha yako kuwa karibu nawe, ikiwemo familia yako, kipato chako, marafiki zako na kila kitu. Atahakikisha unapata hivyo vyote na maisha yako hayatakuwa ya kawaida.
SOMO: NGUVU YA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO. Uzima unatoka kwa Mungu, watu wengi wanatembea lakini ndani yao kuna ufu na ndiyo sababu unaweza kuona hata gari linaweza kuwaua, gari lipo ili kukusafirisha na si kukuangamiza, lakini kwa sababu unatembea na ufu ndio maana linaweza kukuangamiza. Unapo tembea na ufu ndani yako chochote kinaweza kukuangamiza, lakini ukitembea na uzima hakuna cha kukumaliza. Isaya 43:1-6 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.” Mungu hajakuumba tu lakini pia alikukomboa na kukuchagua, usiishi kama mtu yeyote tu bali ishi kama mtu aliye kombolewa au aliyeitwa. Mungu ametuumba wote lakini kuna wale ambao aliwachagua na amewaita kwa jina lake ili wawe wake. Isaya 43:2 “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.” Unapopita kwenye maji mengi hayawezi kukwambia kuwa kipindi hiki hutaishi kwa maana nitakuangamiza, utakapo pita katika moto uunguzao hauta unguzwa kwa sababu wewe umechaguliwa na aliye kuchagua ni MOTO ULAO hivyo moto hautaweza kukuangamiza. Roho wa Mungu ni maji yaliyo hai hivyo ukiwa naye maji hayataweza kukuangamiza kwa sababu maji yaliyo hai yako ndani yako.
welcome
Asante Mungu Kwa Neema Zako , Miss You Efatha,
Ni ukurasa unaofanya vizuri, unapotembelea hukosi cha kujifunza...!

Welcome to mbinga

NENO EFATHA LILITAMKWA MARA MOJA TU NA BWANA YESU KATIKA KITABU CHA MARKO 7:34. MBINGA FUNGUKA. Saa imefika ya kuileta injili halisi ya YESU KRISTO wilayani Mbinga. Mungu alipomuita Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa kazi ya kuliandaa kanisa lenye NGUVU ili hatimaye Injili iwaokoe waliokusudiwa, kwa wakati na majira yake sasa tumefika Mbinga. Nini kinafanyika? Kuikomboa Mbinga na watu wake Kutoka madhalimu yote ya shetani Kupitia mahubiri ya Neno la Imani, kama Biblia isemavyo "Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo" WARUMI 10:17. Kwa kuwa wengi wanampenda Yesu Kristo hivyo tunafundisha mafundisho maalum ya kukulia wokovu, na jinsi ya kuishi na Nguvu ya ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye chanzo cha Hekima, maarifa na Mafinikio Yote ya Mwanadamu. Huduma ya Efatha ni maono aliyopewa Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira ambayo ndani yake kuna kusudi la Kiungu. Ili kufanikisha kusudi hilo, MUNGU alimpa Mtume na Nabii vipengele 10 vya kutekeleza ambavyo kwa pamoja ndivyo vinavyoumba Huduma ya Efatha. 1. Kuikomboa Tanzania ili iweze kusimama mbele za kiti cha hukumu na kupokea baraka za MUNGU. 2. Kuliandaa kanisa la YESU KRISTO kwa ajili ya kunyakuliwa lisilo na mawaa wala makunyazi. 3. Kufanya Kanisa la YESU KRISTO liwe na Mamlaka. 4. Kudhihirisha uweza katika KRISTO YESU, kwa Ishara, Miujiza, Uponyaji na Ukombozi wa Roho, Nafsi na Mwili. 5. Kuwafanya watakatifu wawe na umoja. 6. Kumzalia BWANA matunda yaani kuwaleta watu kwa YESU. 7. Kupokea vipawa vya MUNGU kama mahitaji yetu, ROHO MTAKATIFU, lugha mpya na kuvigawa. 8. Kusimamia kazi ya MUNGU na kuruhusu maongozi ya ROHO MTAKATIFU yaweze kutenda kazi. 9. Kuhakikisha kuwa malango ya kuzimu yananyamazishwa. 10. Kuwa tayari wakati unaofaa na usiofaa kuhubiri NENO la MUNGU Usisite, njoo ukutane na Neno lenye kukutoa shimoni yaani dhambini. MBINGA MBINGUNI NI KUWA NA YESU. HALELUYA!

Mission: Kuileta Mbinga kwa Yesu. Kuikomboa jamii kutoka vifungo vya ibilisi kwa DAMU YA YESU na kuiponya jamii ya Mbinga ili iishi sawasawa na kusudi la Mungu kwa watu wake.

TABIA ZA KIONGOZI.
1.kujitambua yeye ni nani?
2.Atmbue mamlaka inayotenda kazi ndani yake ni ipi?
3. Ajitathimini.
4.Atambue haki za kila mtu

SIFA ZA KIONGOZI BORA
-Anafanya majukumu kwa usahihi
-Anafanya mambo kwa ukamilifu
-Anafanya majukumu kwa uaminifu
-Ananguvu ya Mungu
-Anafanya bila kutaka sifa
-Anakubali changamoto na anadhunghulika kuzitatua
-Anajikagua na kujihukumu

Mchungaji David A. Kaywanga
SOMO;Kiongozi ni nani?
Kiongozi ni mtu anaesababisha watu wafanye
kulingana na yeye anafanya nini.
-kiongozi mzuri ni yule amabaye anakutana na matatizo na anakuwa na majibu ya matatizo ayo.
-kiongozi anaweza akawa anadharauliwa na viongozi wenzie kutokana na umri wake lakini anaweza kuwa ndiye kiongozi bora kwani anakuwa na majibu ya matatizo mbalimbali (mfano Daudi alidharauliwa kulingana na umri na udogo wake wa mwili lakini alimshinda Goliathi)
-Kiongozi mzuri ni mkweli na mwaminifu pia anakuwa na hofu ya Mungu.
TABIA ZA KIONGOZI.
1.kujitambua yeye ni nani?
2.Atmbue mamlaka inayotenda kazi ndani yake ni ipi?
3. Ajitathimini.
4.Atambue haki za kila mtu
KIONGOZI BORA
-Anafanya majukumu kwa usahihi
-Anafanya mambo kwa ukamilifu
-Anafanya majukumu kwa uaminifu(mithali 12:14)

Ibada ya jumapili tarehe 16/02/2020 katika kanisa la efatha Mbinga waimbaji wakimsifu Mungu

We bring Mbinga to Jesus

Karibu katika kanisa la Efatha mbinga lililopo eneo la uwanja wa ndege.

Karibu ibada inayoendelea Katika kanisa la Efatha Mbinga.

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26/1/2020 KANISA LA EFATHA MWENGE.
MTUME MKUU NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

SOMO: JE KUNA NENO GANI LILILO GUMU KUMSHINDA MUNGU?

Ibilisi anaweza kutengeneza mazingira magumu ila Mungu anatengeneza mlango wa kutokea. Ni kweli hali unayopitia ni ngumu ila si kwamba haiwezekani kwa sababu hakuna jambo gumu kwa Mungu.

Toa macho yako kusiko wezekana na uangalie uwezekano.

1. Ruhusu macho yako yaone uwezekano, unapoona uwezekano basi inakuwa ni rahisi kupata kile unacho kihitaji.
Kama kila jambo lingekuwa ni rahisi katika maisha yako basi usinge muhitaji Mungu, kwa nini tunamuhitaji Mungu? Ni kwa sababu maisha tunayoishi huku Duniani yana mipaka hivyo tunamuhitaji yule ambaye hana mipaka ili atuondoe kunako vizuizi vyetu.
Mara zote vizuizi havifanani bali kusudi la kuzaliwa kwa mtu ndilo litakuonyesha unazuiwa na nini, ruhusu macho yako yaone uwezekano na si vizuizi. Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”

a. Siyo kila mtu unayemuona anabeba msaada wako la! tambua ni nani anabeba msaada wako, kuna watu wako ili kukuchosha lakini wengine wapo ili kukusababisha wewe ufurahi na utimilize hatima yako hivyo unapaswa kuwafahamu.
Anayeweza kukuzuilia anaweza kuwa ni mumeo/ mkeo, baba au mama yako hata wafanyakazi wenzako hivyo usiseme kwa sababu huyu ni baba yangu la! Jifunze kutambua ni nani atakuonyesha njia ya kutokea.
Anayeweza kuwa msaada wako muda mwingine unaweza ukawa haumpendi kabisa au ukampuuza.

b. Usifanye matatizo yako kuwa magumu zaidi, jifunze kufanya mambo kuwa mepesi.
c. Mara zote uwe na malengo na fahamu unachokihitaji usichukue mambo yote kana kwamba haujui unacho kihitaji.
d. Jifunze kuzingatia.

JE KUNA NENO GANI LILILO GUMU KUMSHINDA MUNGU?

Mwanzo 18:14 “Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.”

Je! kuna neno gumu kwa Mungu? Linaweza likawa ni gumu kwako ila si kwa Mungu, ni kwa nini Mungu aseme hivyo? Sara na Ibrahimu walikaa miaka mingi pasipo kupata mtoto na ikafika mahali Sara akawa amevuka umri wa mwanamke kupata mtoto hivyo ilikuwa ni ngumu kwake kupata mtoto.

Hali ambayo unapitia leo hii inaweza ikawa ngumu lakini si kwamba haiwezekani, ni kweli inaweza kuwa ni ngumu kwako lakini si kwa Mungu hivyo mtumaini Mungu. Ukiona mambo ni magumu usiseme haiwezekani kwa sababu jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote, Mungu hajawahi kushindwa.

Katika maisha yako kunaweza kukawa na jambo gumu kwako lakini si kwamba haliwezekani, magumu yanaweza yakatokea, haijalishi umezaliwa mara ya pili au la! Kwamba ni mwema au mbaya, mtakatifu au mwovu, hali inaweza kuwa ngumu lakini si kwamba haiwezekani mbele za Mungu.

SHUKRANI

Baadhi tu wazazi na walezi wa watoto waliomaliza kidato cha nne mwaka 2019 katika shule ya Efatha Seminary. Tunapenda kumshukuru Mungu sana kwa ajili ya watoto wetu waliyomaliza kidato cha nne katika shule ya Efatha Seminary, Kipekee kabisa tunamshukuru Mungu kwani Watoto wetu wameweza kufanya vizuri katika mitihani yao, sisi kama wazazi na walezi tulikubaliana tukaunda umoja wetu na kila siku usiku tukawa tunaomba kwa ajili ya watoto wetu, hii ilisaidia hata wale watoto ambao uwezo wao wa kuelewa ulikuwa mdogo Bwana aliwasaidia hata wao wamefanya vizuri katika mitihani yao.

Tunawashukuru pia waalimu wa Efatha Seminary kwani wamekua karibu na sisi tulisimama kwa pamoja tukasema tunataka kuona watoto wetu wakifanya vizuri, tuliazimia kuwainua watoto wetu na wameweza kufanya vizuri katika masomo yao. Wazazi wote tunafuraha kwa maana tumeona watoto wetu wakifanya vizuri kiroho na kitaaluma, Mungu awabariki walimu kwa kuwa bega kwa bega na sisi wazazi pamoja na Watoto wetu.

Tunawashauri wazazi kuwapeleka watoto wao Efatha Seminary kwa sababu ni mahali salama, ni mahali ambapo mtoto anakuwa kiroho na kiakili.

Never giveup .

USHUHUDA

Naitwa Simaiton Patson napenda kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyotenda maishani mwangu, nilihukumiwa kifungo cha maisha gerezani, lakini baada ya kukaa gerezani kwa miaka kumi ndipo nilipopata neema ya kukutana na watumishi wa Mungu kutoka hapa Kanisa la Efatha wanaokuja kule gerezani Ukonga kutufundisha habari za wokovu na kututia moyo kwamba liko tumaini na Mungu anaweza.

Nilipompokea Yesu (kuokoka) na kuendelea kumwamini, nilikata rufaa mara kadhaa sikufanikiwa lakini sikukata tamaa niliendelea kuishika imani, ndipo Bwana alinikumbuka na ilipofika tarehe 6/1/2020 niliachiwa huru kabisa.

Namshukuru Mungu sana kwa huruma zake kwangu, pia nawashukuru watumishi wa Mungu wanaotembelea wafungwa gerezani na kuwafundisha Neno la Mungu, jamani Mungu yupo mimi kuwa hapa leo ni muujiza sikujua kama nitawaona ndugu zangu tena; ilifika wakati nikakata tamaa lakini baada ya kukutana na huyu Mungu amenisaidia leo niko hapa.

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26/1/2020 KANISA LA EFATHA MWENGE.
MTUME MKUU NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Mungu alimtoa mwanaye wa pekee kwa ajili yetu ili awe dhabihu na kwa sababu hiyo tumekombolewa, kwa sababu ya dhabihu ambayo Mungu aliitoa kwa ajili yetu ibilisi hana nguvu juu yetu tena kwani tumekwisha kombolewa, vivyo hivyo tunapo jitoa kwa Mungu na vyote tulivyonavyo ndipo Mungu anaachilia kile alichonacho kwa ajili yetu.

Haupokei kile ambacho ni stahiki yako kutoka Mungu kwa sababu haujitoi mwenyewe na vile ulivyonavyo.

Matoleo ni nini? Ni kuonyesha Upendo, itaonesha ni kwa jinsi gani unampenda Mungu kupitia matoleo yako maana pasipo Pendo kamwe hauwezi kutoa.

Je! Unampa nini Mungu? Yeye alitoa uhai wake kwa ajili yetu sasa je! Wewe unatoa nini kwa ajili yake? Mimi niliamua kutoa maisha yangu kwake, maisha yangu si yangu tena bali ni maisha yake, kama maisha uliyonayo si yako yaani umeyatoa kwa Mungu inamaana kuwa si wewe tena unaye ishi bali ni YEYE ndani yako kwa maana hiyo hakuna kitakacho kusumbua tena.

Kutoa kunaponya, kupitia matoleo yako unaweza kufukuza magonjwa mbali na wewe.

Zaburi 32:11 "Mfurahieni Bwana; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo"

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26/1/2020 KANISA LA EFATHA MWENGE.

Yesu alikufa kwa ajili yetu, na huu ni mwaka wa utambulisho wako, nguvu ya Roho Mtakatifu itakuchukua popote ulipo na kukuleta karibu na Mungu, Mungu tumtumikiaye ni Mungu wa kusudi na ni Mungu ajuaye mwanzo na mwisho wako, anajua wapi pa kuanza na wapi pa kumaliza, jinsi gani ya kuingia na kutoka, katika yeye hakuna mashaka, wala giza.

Mungu anajua vyema kuhusu wewe, mazingira ya pale unapoishi, unapofanya kazi au pale ulipo zaliwa yanaweza kukudanganya na kukwambia mambo hasi na ukiyatazama unaweza ukasema hakuna namna ya kutoka tena. Mazingira yanaweza kukuhubiria kwamba umekwisha, inaweza ikawa hivyo lakini tambua mazingira hayana jibu wala neno la mwisho kuhusu wewe bali yuko Mungu mwenye jibu na neno la mwisho kuhusiana na wewe. Kwa sasa inaonekana kwamba hakuna njia ya kutoka lakini sio kweli, huo ni uongo, hayo unayo yaona, uliyo yafahamu yanazungumza uongo siyo ukweli kukuhusu wewe, aliye na ukweli kuhusu wewe ni yule anayejua mwanzo na mwisho wako naye ni Mungu.

Kuna nguvu katika Yesu na Jina lake lina nguvu, ni kweli wewe peke yako hauna nguvu lakini katika YEYE unazo nguvu tele. Ni kweli wewe ni mdogo lakini katika YEYE wewe ni mkuu, kwa sababu anayeishi ndani yako ni mkuu.

© MTUME MKUU NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

MTUME MKUU NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Ayubu 33:27-28 “Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo; Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.”

Unapaswa kuzingatia matendo yako, ni wakati gani Mungu anakuokoa? Ni wakati unapo zingatia matendo yako na kuamua kumgeukia Mungu ndipo anaweza kukuokoa, leo ni siku yako ya ukombozi, Mungu anajua yale uliyopitia katika maisha yako na leo atakukomboa; lakini unachopaswa kufanya ni kuzingazia matendo yako, amua kubadilika na kisha utubu ili upate kukombolewa.

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26/1/2020 KANISA LA EFATHA MWENGE
MTUME MKUU NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Ayubu 33:14-15 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”.

Siyo tatizo la Mungu bali ni tatizo la mtu ni jinsi gani unavyoona na kuzingatia Mungu anapo nena na yeye, ingawa hatuelewi anachosema tulalapo lakini inatupasa kuzingatia kile ulichokiota. Unapo lala takasa kitanda chako kisha ulale, Mungu anapokuja na kusema na wewe msikilize kwa umakini, unapoamka asubuhi chukua muda wa kutafakari hiyo ndoto na kisha uombe kwa ajili ya hiyo ndoto.

Ayubu 33:16-18 “Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”

Mungu anasema na kutoa maelekezo kwa mwanadamu ni kwa jinsi gani anapaswa kuishi hapa duniani, haupaswi kuishi kwa jinsi unavyotaka wewe bali unatakiwa kuishi sawa sawa na maelekezo yake.
Siku zote kusudi la mtu litampeleka shimoni na kumsababisha aangamie, ndipo Mungu humtuma mjumbe wake ili kumuokoa mwanadamu kuondokana na mawazo yake kwa sababu kama ukizingatia mawazo yako na kuyatekeleza utaishia shimoni na kuangamia.

Ayubu 33:19-20 “Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;” Kama hautakuwa tayari kumsikiliza Mungu yeye ataruhusu maumivu na mateso katika mwili wako ili upate kumsikia Yeye ili aweze kukugeuza.

Efatha Ministry Mbinga

Efatha Ministry Mbinga

Efatha Church

SUNDAY SERVICE - EFATHA MWENGE

mixlr.com

EFATHA CHURCH on Mixlr

Haleluya Mwana wa Mungu, hakika mimi na wewe tuna kila sababu ya kumrudishia Mungu SIFA na SHUKRANI zetu kwa yale aliyotutendea wiki hii yote mpaka kufikia Jumapili hii ya leo, napenda nikukaribishe katika Ibada ya Jumapili ya leo hapa Kanisa la Efatha Mwenge Dar es salaam Tanzania na katika Vituo vyote vya Kanisa la Efatha ndani na nje ya nchi.

Kama upo mbali unaweza kufuatilia Ibada hii mubashara (Live) kupitia Trenet TV, na mitandao yetu ya kijamii kama Facebook, Online Radio ambayo ni http://mixlr.com/efatha-church/ na Instagram ni www.instagram.com/efatha.church.

Nakutakia Ibada njema; Mungu Akubariki.
He looked up to heaven and with a deep sigh said to him, "EFATHA!!!" (which means "Be opened!") - MARK 7:34

About this website
MIXLR.COM
EFATHA CHURCH on Mixlr
He looked up to heaven and with a deep sigh said to him, "EFATHA!!!" (which means "Be opened!") - MARK 7:34

He looked up to heaven and with a deep sigh said to him, "EFATHA!!!" (which means "Be opened!") - MARK 7:34

Ibada ya neno
Mchungaji Upendo Mapunda
Somo: PENDO LA KRISTO
(Luka19:1-9)kupitia injili hii inatufundisha jinsi gani Yesu anatutazama, Zakayo alionesha kuling'ang'ania pendo la kristo
Kamba za kuzimu zimetuzunguka kutokana na kuzaliwa kwetu na kupelekea tusilijuwe pendo la kristo. Kamba yeyote inayoficha maisha yako leo lazima ikakatike lakini kwa kusimama tu katika imani. Vile vyote vinavyotuzuilia ndio kamba zinazotushikilia mfano.kutojiamini
Yatupasa kutii maelekezo na maagizo ili kuzishinda kamba za kuzimu. Mtu mwenye pendo la kristo anaishi maisha yake halisi. Zakayo aliishi maisha halisi akuangalia kimo chake wala umati unaomzunguka yeye alitafuta pendo la kristu. Watumishi wa Mungu atupaswi kuangalia umati unaotuzunguka katika wokovu wetu. Katika utumishi wetu na nafasi zetu ndipo yesu atakapopitia kutuletea baraka zetu mfano. Waimbaji inapaswa wasimame katika uwimbaji wao
Watumishi wa mungu atupaswi kujidharau kutukana na mazingira ya utumishi wetu,kwani Mungu anachotaka kutoka kwetu ni kumheshimu na kumpenda hivyo watumishi wa Mungu tunapaswa kutafuta pendo la Mungu na sio kufurahisha wanadamu. Mungu siku zote anaangalia haki haangalii watu wanasema nini juu yako.
Wokovu ni neema hivyo tumshukuru Mungu kwa wokovu tulionao na tutamani watu wengine pia wapate neema hii ya wokovu

Waimbaji wakiongoza sifa katika jumapili ya leo

Mtumishi Evaristo Komba akiongoza kipindi cha matoleo katika jumapili ya leo. (Malaki 3:10-11)
Faida za matoleo
1.Matoleo huondoa hofu na mashaka katika maisha yetu
2.matoleo huondoa giza katika maisha yetu
3.matoleo yanatupa kibali cha kuona mbali katika maisha yetu na kuona ubadae katika maisha yetu
4.matoleo yanatupa kuwa na mwisho mwema wenye furaha na mashangilio

USHUHUDA
Mtumishi Magreth Ndambo anamshukuru Mungu na kumshangaa kwa matendo yake makuu kwani ameweza kufunga siku 3 kavu mara mbili.Haikuwa jambo rahisi kwake lakini ni kwa kibali na neema ya Mungu wa mbinguni.

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 19/01/2020
Mtumishi wa Mungu Felisiana Ndimbo akifungua kipindi katika ibada ya Jumapili ya leo.

Waimbaji wakiongoza sifa katika ibada ya jumapili

IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 12/1/2020
Mtumishi Felisiana Ndimbo Askofu wa zone ya Gezaulole dar es salaam
Somo: Imani
Imani inapoumbika tunapokea kile tulichoahidiwa na mwenyezi Mungu.(mathayo14:29-31) Imani iliyokamili ni kuamini kitu moja kwa moja. Yatupata tusiwe na mashaka kwenye imani yetu. Tunaposikia jambo na kulitii na kulifanyia kazi tunajenga imani madhubuti, Imani madhubuti inajengeka ndani yetu kupitia maombi. Imani ni roho hivyo mambo ya imani ni mambo ya kiroho zaidi, ili kuwa na imani madhubuti yatubidi kuwa watu wa rohoni. Mashaka Yanafanya imani kutetereka (waraka wa kwanza wa mtume petro2:1) mashaka na visingizio vinafanya imani kutetereka hivyo baraka na neema nyingi zinatupita. Maovu yanamfanya Mungu asiweze kukaa ndani yetu kwani Mungu hawezi kukaa hekalu lenye dhambi.(matendo ya mitume 3:1-4)mategemeo ya mtu yanamfanya Mungu kukutendea kupitia hayo mategemeo kwani imani ni mategemeo

Ibada ya matoleo
Mtumishi Happy Isaya akiongoza ibada ya matoleo na maombi kwa ajili ya matoleo

Ibada ya jumapili tarehe 12/01/2020
Mtumishi Evalista Benja akifungua ibada

IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 12/1/2020
ASKOFU FELISIANA NDIMBO
SOMO:IMANI

DARASA LA JUMATATU YA TAREHE. 30/12/2019.
MCHUNGAJI: DEVID ALEX
SOMO: TABIA ZA WANA WA MUNGU WA ISRAELI NA MADHARA YAKE.
1. Tabia ya kunung'unika na kudharau
Kutoka 14:11
2.Tabia za kutangaza habari mbaya
Hesabu 13:27-33
3.Tabia ya uwoga na utumwa.

USHUHUDA

Naitwa Emmanuel Charles namshukuru Mungu kupitia semina ya Mtumishi wa Mungu Mtume mkuu na Nabii Josephat Elias Mwingira, iliyofanyika mwezi wa sita katika semina hiyo Mtumishi wa Mungu alitufundisha yeye ni kama gari au ukuta linalomsaidia mtoto kutembea.

Nililishika hili Neno na wakati huo nilikuwa nimefunga biashara yangu na nyumbani nilikuwa na akiba ya shilingi elfu kumi tu, niliichukua pesa ile na kuanzisha biashara ya maziwa ambapo nilianza na lita kumi lakini Mungu aliendelea kuniinua sasa nauza hadi lita thelathini kwa siku.

Namshukuru Mungu nilikuwa sina pesa lakini sasa ninapesa za kutosha, ninapouza maziwa yangu siiti wateja kwa kupiga kelele Maziwa maziwa la! ila huwa nanena kwa lugha tu na wateja huja wenyewe, nikipita nawakuta wananisubiri kwenye mageti yao, namrudishia Mungu sifa na utukufu wote.

USHUHUDA:

Naitwa Grace Kwetukia, namshukuru Mungu kwa kunisaidia kumaliza shahada yangu ya kwanza, kuna siku Mtumishi wa Mungu Mtume Mkuu na Nabii Josephat Elias Mwingira alitamka neno akasema “nenda kafanikishe kumaliza elimu yako katika mwaka huu wa ushindi” mimi nililipokea na kulisimamia hilo Neno na Mungu alinitetea na kunifanya kuwa mmoja wa wahitimu. Namshukuru Mungu sana maana pasipo Yeye nisingeweza kufika hapa nilipofika.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mbinga?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


Precious Area, Kihaha Street, P. O. Box 299
Mbinga
TZA