Efatha Ministry Kigoma

Efatha Ministry Kigoma

Comments

Mungu anawapenda wale wampendao. Nao wamtafutao kwa bidii watamuona.
natafuta.mchumba.kama.yupo.tayar.nipo.radhi.hata.kuja.kusalia.anaposali
Wahi Usajili Wa Muhula Wa Masomo Kwa Mwaka 2019/2020 Kwa Ngazi Ya Cheti Na Diploma Ktk Kozi Ya Pharmaceutical Science Ktk Chuo Cha Western Tanganyika College Kigoma.(Chuo Chetu Ni Full Accredited by NACTE).Tupo Kigoma Mjini Lilipo Kanisa Katoliki Jimbo La Kigoma. Ada Yetu Kwa Mwaka Ni 1,400,000/=Unalipa Kwa Awamu 4. Ada Nafuu Kwa Kozi Hiyo.Mwombaji Anatakiwa Kuwa Na Ufaulu Wa D4 Tu,Ikiwemo Biology Na Chemistry.Kozi Ya Business Administration Na Kozi Ya Records,Archive's and information management Ada Kwa Mwaka Ni Laki 840 Utalipa Kwa Awamu 3.Piga au Sms 0713686812/0756708989
#Kibali cha Mungu wa kweli kiwe juu yetu nawatakia baraka njema ya Mungu wa kweli ikufungue katika vifungo vya kuzimu Mungu wa kweli uinuliwe juu kama una amini sema asante #YESU Amen
Nawapenda sana Efatha kigoma, songa mbele
Habari za utumishi uliotukuka nimekukumbuka sana baba yangu bensoni E mpele hakika mungu amekuagiza kgm naasie amini ato amini milele we we nibaba bora mafanikio yakukusikilza nayaona sasaivi japo ilifika hatua nikaanza kukupinga lakin wwe ni mtu ulie nifundisha kiroho na kimwili nanimefika mpaka hapa #NAKUPENDA_SANA_RATHER_BEN #NIPO_NJIANI_NAKUJA_KGM #mr_crown
TANGAZO KWA UMMA. Wahitimu Wa Kidato Cha 4 Waliopata Ufaulu Wa Kuanzia D 4 Wa Wahi Kujiunga Na Chuo Cha Western Tanganyika College Kigoma.Ktk Kozi Ya Famasia,Ukutubi Na Kozi Ya Usimamizi ktk Biashara kwa ngazi ya Cheti na Diploma. Usajili Wa CAS NACTE unafungwa Tarehe 26/02/2019. Tuma Sms au Piga 0713686812/0756708989 Karibuni.
Kwa Waombaji Wa Kozi Ya Pharmaceutical,Business Administration Na Records,Archive and Information Management Wahi Western Tanganyika College Kigoma Kabla Ya Usajili Wa Nacte haujafungwa Tarehe 05/02/2019.Fomu unaweza kupata kupitia Wasap 0713686812.
Efatha wore baba yetu mmoja!
Efatha
Kusanyiko hili la 2018 December 24-01 mambo yake ni MOTO haijawahitokea.

Healing and Deliverance By the Blood of Jesus

Mtumishi wa Mungu Mtume Mkuu Josephat Elias Mwingira anawakaribisha watu wote wanaompenda katika Ibada maalum ya kusheherekea maisha ya baba yake mpendwa Mzee Elias Mwingira, ibada hiyo itafanyika katika Kanisa la Efatha Precious Center Kibaha, Mkoa wa Pwani, Tanzania siku ya kesho Ijumaa kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni na siku ya Jumamosi saa nne asubuhi hadi saa 7:00 mchana; wote mnakaribishwa.

#Kumuaga Babu yetu kutaanza kuanzia Asubuhi, Ibada itaanza saa 7:00 Mchana.

Matangazo ya ibada hio yatawajia moja kwa moja kupia Trenet TV Na mitandao yetu yote ya kijamii FACEBOOK NA YOUTUBE

EFATHA KIGOMA –IBADA YA JUMAPILI TEREHE 16.02.2020
MTUMISHI EASTER HAMIS
MACHO YA HEKIMA

Kila mwanadamu chini ya jua ana macho . kwa sisi Efatha tupo mahali sahihi na salama kwa wokovu wetu . kwani tumepewa kutembea na roho zote saba ikiwemo hekima .

Hekima mara nyingi ana ndugu yake mmoja anaitwa IMANI . IMANI ina macho , vitu hivi viwili vinatenda kazi pamoja na kwa kufanana sana .

Kazi ya hekima inakupa kutenda mambo bila kukosea na bila maumivu wala majuto . HEKIMA inakupa kutenda kwa usahihi . Inakupa kufikia hicho unachotamani kufanya bila kuchoka , kujuta hata kama kuna maumivu .
Hekima inakupa kujua ufanye nini na wakati gani . Mwaka huu ni mwaka wa kufanya mambo kwa wepesi . Roho wa hekima atakujulisha .

Unapookoka Mungu huwa anaachilia hii Roho ili usikate tamaa.

Waefeso 2:10 , . Baada ya dhambi matendo yetu mema yalinyamazishwa na kuibuka matendo ambayo hatukupaswa kuenenda nayo . Tunahitaji sana hekima ili tuenende katika njia hii tuliyo nayo ya wokovu , kwani tuliandaliwa kwa ajili ya kutenda mema .

Zaburi 119:1 , . ukishika sana sheria ya Bwana ni hakika utapokea vya BWANA . huwezi kupokea vile unavyotaka kupokea kama huwezi kufanya matendo mema uliyokusudiwa . Tuliumbwa ili tumtii Mungu .

Hata sasa tumeambiwa tuondoe GIZA mbele yetu , lakini ukipata macho ya hekima . utaweza kuona mambo katika uhalisia wake na hata kufikia kuona mbali na hatimaye unakuwa na mwisho mema.

Unapopata kuona unajenga jambo ,lakini usipopata kuona unaharibu jambo . HEKIMA hujenga .
HEKIMA ,IMANI vikiwepo katika utumishi wako unakuwa si wa kawaida .

IBADA YA JUMAPILI
TAREHE 16/02/2020
Kanisa likisifu na kumwabudu MUNGU.

EFATHA KIGOMA IBADA YA JUMAPILI TAREHE 09.02.2020
MTUMISHI ; EASTHER KHAMIS
SOMO: IMANI YENYE NGUVU .

Imani yenye nguvu hukaa ndani ya mtu mwenye imani .Huyo mtu anakuwa na nguvu kwa kila anachokifanya . kwa sababu ya kuwa na imani hiyo hupokea vitu .

IMANI hutoka kwa Mungu . imani ni Mungu mwenyewe . Mtu wa imani huwa hashindwi na chochote na hupokea zawadi .

Zaburi 119:50, huyu mtu wa imani hupitia mazingira magumu . Mara nyingi huwa anahitaji usaidizi, kwa sababu huwa anasubiria vitu visivyoonekana . Anahitaji kupewa faraja , Mungu huachilia faraja ndani yake ili kutokata tamaa.

Watu hawa wa imani hupokea zawadi na huwa si wa kawaida . Wanafanya mambo makubwa na kushinda kwao ni kwa imani .

Tunao mfano wa watumishi katika biblia waliopita kwa imani .Ibrahim alikuwa mtu wa imani . Ayoub alikuwa mtu wa imani ,ingawa hakuitwa baba wa imani kama Ibrahim . daudi, Mussa wote hawa walitembea kwa imani.

Kuna wengine walisimama ,hata mali zao kuharibika wakishikilia imani . Ayoub maradhi yalimshambulia hata kushinda . daudi alipigana na dubu ,simba na Goliath hata kushinda .Hawa wote waliamini yanawezekana .

Ili IMANI iweze kuthibitika kwako kuna mambo ya msingi kuzingatia

1. USIWE KATIKA KUNDI LA MIZAHA NA UISHIKE SHERIA YA BWANA –Zaburi 1:1-3, ukishika sheria yake yeye anakupa nguvu
2. ACHA DHAMBI NA UWE MKWELI – kweli iwe ndani yako , usiwe muongo ,mnafiki kwani wewe ni mpakwa mafuta .
3. UWE MTU WA TOBA –Hii ndiyo njia pekee itakayoweza kukufanya upokee na wala usijihesabie haki . Daud alikuwa mtu wa toba
4. KUWA MTU WA KUSOMA NENO- imani itakapoenda kudhihirika hata neno litakuwa na nguvu .kwani Neno ni upanga ,nyundo ,moto na maji .

Zaburi 107:20 . Mwaka huu tumepewa Roho atakayetuongoza . Yeye atatufunulia yale yajayo na yale yaliyopo . Yapi ya kufanya na kutofanya . dhumuni ni kutoingia kunako maangamizo .

IBADA YA JUMAPILI
TAREHE 09/02/2020.
Mass choir kigoma wakiongoza ibada ya kumsifu na kumwabudu MUNGU

EFATHA KIGOMA TAREHE 02.02.2020
SOMO: NGUVU YA MSALABA
MTUMISHI EASTER HAMIS

Msalaba kwa sisi tunaoamini au tuliokoka ni nguvu kwetu ya ushindi. Nguvu hii hubeba kila aina kushindwa kwetu hapa duniani . Katika kila kitu ili uweze kutenda lazima uwe na nguvu , aidha inaweza kuwa ya upande wa giza au wa nuru .

Bila nguvu mwanadamu hawezi kutenda sawa sawa. Mungu pia humtegemea mwanadamu anapokuwa ameipokea hiyo nguvu kutoka kwake .

Nguvu ya uovu ipo ndani ya ulimwengu . Nguvu ya msalaba ipo ndani ya waaminio au waliookoka. Nguvu hii inatenda kazi kwa mtu yeyote anayemwamini Yesu kristo kuwa Bwana na muokozi wa maisha yake . Nguvu hii anapokutana nayo mtu anayemwamini yesu kuna ushindi kwake .

1Yohana 5:4 , Nguvu inayokuja lazima ujue kuwa Yesu kristo alizaliwa na Mungu . Kwa kuamini tu hata kuzaliwa kwa yesu kulikuwa kimaajabu .Ujue hata wewe umeshinda tayari.

Ukiilewa maana ya msalaba na kuzaliwa kwako mara ya pili , tambua kuwa yale aliyopitia Yesu kwa namna moja au nyingine na wewe utapitia .

Kufikia nguvu ya msalaba ili ifanye kazi kuna mapito lazima upitie .
I. DAMU lazima imwagike.
II. PENDO lazima liwepo kwako .
III. IMANI iwe thabiti na lazima ithibitishwe.
Mambo haya yanakupelekea kuwa mtu wa huzuni kama Yesu alivyokuwa . Unakuwa ni mtu wa

I. KUVULIWA NGUO.
II. MAUTI /KIFO
III. KUTEMEWA MATE
IV. MIIBA KUKUSONGA
V. KIU NA NJAA.

Haya yanawezaje kutenda kazi kwetu sisi kwa sasa . Katika nguvu ya adui kuna mambo ambayo wanafanya ,hata katika biashara zao wanaweza hata kuua mtu . Duniani pasina nguvu hakuna kinachoenda . Kwa sisi ili tushindane na hii nguvu tunapeleka kweli .

Ukiwa umeokoka na unaona unapitia haya ni kwa ajili ya kuimarishwa. Vipengele hivyo ndivyo vinakufanya kuthibitika mbinguni na hata ibilisi kukusujudia . IMANI yako inakuwa na nguvu baada ya nguvu hii kukuthibitisha .

Ukiweza kupita unaenda kupata zawadi .kwa nguvu hii ya msalaba tunapewa mamlaka ya kuvunja na kuondoa uharibifu wote

Untitled Album

IBADA YA JUMAPILI
TAREHE 02/02/2020
KANISA LIKISIFU NA KUMWABUDU MUNGU.

IBADA YA JUMAPILI
TAREHE 02/02/2020
KANISA LIKISIFU NA KUMWABUDU MUNGU.

Kwenda nyumbani kwenu kwa kiroho ni jambo Muhimu iwe ni usiku au mchana yapende mazingira hayo na uyaheshimu maana Mungu anakuwa mahali hapo kila wakati. Kanisa la Efatha kigoma Mahali hapa pameandaliwa na kufanyika baraka kwa kila anaepasogelea,
Hakika Mungu anaenda kututambulisha kwa namna ya Ajabu mwaka huu 2020.
MUNGU ANATENDA MAAJABU NA ATADUMU AKITENDA MAAJABU.

EFATHA KIGOMA

MTUMISHI: EASTER HAMIS

SOMO: NGUVU YA MUNGU

Nguvu ya pendo la Mungu kwetu lilimfanya amtoe mwanae wa pekee .Mungu wetu ni mwenye nguvu . Pendo lina nguvu ya kushinda dhambi . Dhambi pia ina nguvu , ila ndani ya kristo yesu kuna nguvu ya ushindi .

Ukiwa katika pendo huwezi kufa milele , pendo linafufua . kwani dhambi inaua .
Matendo 3:1-2 , sisi katika maisha yetu kuna vitu vilishafanyika ni vilemavu . Kuna ndoa zina ulemavu , biashara ,nk . Ukiwa huna ukiwete unaweza kumtumikia Mungu vizuri . Ukisoma biblia hapo Yule kiwete alitoka katika ukiwete kwa sababu ya pendo la Mungu . Sisi tulitolewa huko tulipokuwa kupitia pendo .
Pendo likishaingia ndani ya mtu kila kitu kinabadilika . Kwani ndani ya pendo kuna ujasiri , hukumu , kurejeshwa ,kubarikiwa na kuinuliwa hata kuondoa ushindani wowote uliopo.Pendo linapokupa ujasiri maana yake upo pamoja na Yeye kupitia Roho yake .Mungu alimtoa mwanae , maana yake na sisi inabidi tufanye maamuzi na tuwe na uthubutu.
1 Yohana 4:17 , hapo ulipo wewe ni kristo . Mungu anakutarajia ushinde . Yeye alivyo ndivyo na sisi tulivyo , ni vyema tuendelee kuwasikiliza watumishi wetu mara zote ili tutende kama kristo .Penda kufanya mambo kwa Mungu kwa gharama zote na hapo utakuwa umeachilia pendo kwake . Kama Yesu alijitoa na wewe lazima ujitoe .
Ili uweze kukubaliana na pendo lazima tugeuke , tuziache njia zetu mbaya , huku tukikubali Yesu alipopita ya kuwa na sisi tutapita kwa kipimo chetu .

Ndani ya pendo kuna mamlaka ya ajabu kuna uwezo wa kuamrisha kitu chochote na kuweza kuwa. Kutiisha na kutii yale yaliyoshindikana kutii . Hapo ndipo utaona uzuri wa pendo la kristo lenye nguvu

1 Yohana 5:4 , Kwa kupitia pendo hili ni lazima tuushinde ulimwengu na tabia zake. Katika hilo pendo kuna uwezo kubomoa na kushinda .

IBADA YA JUMAPILI.
Tarehe.19/01/2020.
Mass choir Kigoma Ikiongoza Ibada kwa Nyimbo za Kuabudu,
Kila aliezaliwa na Mungu anakila sababu ya kumuabudu Mungu Halleluyaa!

EFATHA KIGOMA
MTUMISHI: EASTER HAMIS MASOUD
SOMO :TUPO NDANI YA AGANO LA USHINDI
Katika hili agano kuna mtu ambaye amepewa . tupo ili tushinde . Mwanzo 1:26-28.

Ukisoma biblia , ametupa zile Baraka za kutiisha . leo hii unakuta mtakatifu badala ya kutiisha ndiyo anatiishwa .mke ana mtiisha mume , fedha ina mtiisha mtakatifu , afya inamtiisha nk . Mimi nilipoweza kumsikia mtumishi BENSON magonjwa yaliondoka kwangu . leo ni mwaka wa 11 mpaka sasa sina maradhi .

Nilipofika hapa nilikuwa na vidonda vya tumbo na magonjwa mbali mbali . Mtumishi aliniambia , ‘’ Wewe umeokoka magonjwa si sehemu yako tena “’.
Kuna watu wamepewa kuwa viongozi ,watawala lazima wakawe . Lazima uende huko ulipokusudiwa . hakuna cha kukuzuia .

Ukisoma vizuri biblia , tumepewa kumiliki vyote . Huko tulipokuwa kuna wengine walikuwa hawaruhusiwi kula nyama , wali nk . kila kitu kwao kimetiisha maisha yao , walitishwa . leo tunamshukuru Mungu kwa kutuokoa .

Agano hili tulilopewa lina nguvu ya ushindi . Tumepewa pia utiisho siyo ushindi tu .kutawala na kumiliki. Umiliki biashara , afya yako nk . Hivyo kama kuna maradhi yamepanga kwako lazima yatiishwe siyo kwenda kuyanunulia dawa.

Huu umiliki ni agano tulilopewa na baba yetu wa Mbinguni . tulikwisha pewa . Jambo tunalotakiwa kufanya ni kutembea katika NENO tuliloagizwa tu . Wengi hatutaki kukemewa kuambiwa na kuelekezwa . UKITII UNAWEZA KUTIISHA .

Zaburi 2:8-9 . inasema Mniombe ,siyo ukasome . Hapa ni kuomba tu .Mungu anataka aone mtakatifu yupo tayari ili yeye afanye kitu kwako . Miisho umepewa , na si tu umepewa ila ni URITHI wako .

Kitu chochote kisichotaka utawale katika eneo lako lazima ukipige , iwe ni kufarakana katika ndoa lazima ukipige . Hakikisha tu usilete ugomvi na Mungu .

Tupo katika kipindi cha marajesho na katika hayo marejesho kuna utaratibu wake ambao ni UTAKATIFU .

Hakikisha unashinda dhambi ya MWILI . Daudi alitenda dhambi hii hata kupelekea mtoto aliyezaliwa kufa . dhambi hii inaua .dhambi ya uzinzi ni vita vya mwili . tumefundishwa kuwa mwili nao unasema , vita hii inahitaji rehema ya Bwana .

Mwaka huu 2020 , tumeamriwa kushinda . Hivyo usisikilize amri za mwili . tujitahidi sana kushinda vita hizi ,NAFSI, MWILI, na ROHO . Vita hizi zinahitaji maamuzi si maombi pekee.

Dhambi ya mwili ni mbaya sana ina mtindo wa kujihalalisha maeneo ya GIZA .Mungu akiona umedhamiria atakutoa . Lipa gharama , Mungu atakutia nguvu . daud alitenda lakini alitubu na maisha yake siku zote yalikuwa ni TOBA .

IBADA YA J PILI.
TRH.12/01/2020.
Kanisa likimuabudu Mungu.

USHUHUDA

Mimi naitwa mariam Hussein au kwa jina lingine naitwa grace . Napenda kumshukuru Mungu katika , NDOA na FAMILIA .

Mimi nilikuwa muislam na nilikuwa ni mtoto pekee katika familia yetu kuokoka . mume wangu alikuwa ni mkristo mlutheri .

Nilipoingia Efatha na kuokoka ndugu zangu walinitenga na kunichukia . Mama yangu aliwahi kusema hata akifa nisiweze kumuosha . Mahari yangu walikataa hata kupokea ilibidi nile mwenyewe mahari yangu . Mimi ni mtoto wa nje ya ndoa , lakini baba yangu wa kufika aliweza kufika katika harusi yangu .

Nashukuru Mungu leo hii , wamenikubali hata bibi yangu ameweza kuchukua KIKOI chake kama sehemu ya taratibu za mahari . Hapo mwanzo alikataa.

KWA UPANDE WA NDOA . Nashukuru kwa Upendo wa baba yangu BENSON na mama yangu safina . Ningekuwa nipo katika uislam ndoa hii sidhani kama ingekuwepo . Mume wangu ndiye aliyeniweka katika ukristo , lakini yeye hajatulia katika WOKOVU . Mume wangu ni mwanajeshi lakini mshahara wake mume wangu nilikuwa , SIUPATI . Ashukuriwe Mungu tulimaliza nyumba yetu na kuhamia .

Jambo lingine naloweza kumshukuru Mungu . Nilipitiliza kujifungua lakini mtumishi BENSON alitamka neno nikajifungua salama huku nikiwa na damu 7 , ambayo ni hali si ya kawaida . Mtumishi alisema sitaongezewa damu , mpaka leo sijaongezewa.

Nilihisi kushindwa kufika kusanyiko hata kumfahamisha mtumishi .Lakini shauku yangu ilikuwa ni kutaka kufika kusanyiko aidha na mama mkwe wangu au mume wangu . Mungu ni mwema , Mume wangu alitupa nauli na kufika kusanyiko mimi na mama mkwe wangu. Mama mkwe alimpokea yesu na kuokoka sasa hivi ni mwana efatha mzuri huko karagwe.

USHUHUDA .

Naitwa mtumishi Lazaro , nasimama mbele zenu nikija kumshukuru kwa matendo makuu aliyotutendea mimi na famila yangu . kwanza nashukuru kwa mimi kupata WOKOVU na kuzaliwa sehemu sahihi yaani EFATHA .

Niliwahi kusikiliza somo la mtumishi benson , kuwa chanzo cha kusikilizishwa kwetu kiliharibiwa . Mimi nilishika hicho kuwa chanzo changu cha kusikilizishwa kwangu ambaye ni mtumishi wangu hakitaharibiwa . Nashukuru kwa hayo hakuna cha kunitenganisha na mtumishi . Namshughulika shetani ipasavyo .

Namshukuru Mungu kuweza kuwepo katika Kusanyiko letu la December . haikuwa kazi rahisi hata kidogo . Mungu aliniambia kuhusu baba yangu aliyekuwa anaumwa , kuwa atakufa muda si mrefu . Nilimuomba Mungu asije akafariki kipindi cha kusanyiko letu la wana kigoma , amchukue baada ya kusanyiko .Kusanyiko letu lilimalizaika tarehe 31 december 2019 . tarehe 01/01/2020 , baba yangu aliaga dunia . Namshukuru Mungu wa efatha kwa kunisikiliza .

mkewangu nae analo lakusema

Naitwa MTUMISHI HILDA LAZARO namshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyonitendea .kabla sijaokoka nilitamani sana nimuabudu sana Mungu wa kweli . Niliokoka mwaka 2006. Kabla ya hapo nilikuwa muislam.

Nilikuja EFATHA kutokana na matatizo . Kuna mtu alinishuhudia kwa kuniambia kutokana na matatizo uliyo nayo nenda mahali Fulani utatatuliwa matatizo yako uliyo nayo . Nilifika kanisani EFATHA kimiujiza. Niliingia kanisanai kwa kugoma yaani watu wananivuta , hata kuokoka nilijikuta nipo mbele , pasipo kujua nilifika vipi.

Nilikuwa ni muhudhuriaji wa mihadhara ya kiislamu huku nikichambua Biblia na vifungu vyake. Yale tulivyokuwa tunafundishwa na walimu wa kiislamu. Nilikuja kubaini vifungu wanavyotuambia katika mihadhara ya kiislamu haiendani na jinsi ninavyosoma biblia mimi mwenyewe, Nilikuja kujua ukweli .Huku katika uislam ukweli ulifichwa . Nikawa nataka nione kanisa la kweli ni lipi . Yote niliona kama si ya kweli , mpaka nilipofika EFATHA .

Namshukuru Mungu familia yangu , wanangu wameokoka . Namshukuru Mungu kwa kuolewa ingawa umri ulikuwa umeenda na hata kujiwazia vibaya . Niliona wanaume ni washenzi tu na niliapa sitaolewa. Nilijidharau hata kutoona wa kunioa kanisani .Ashukuriwe mtumishi BENSON , aliyekuwa anahubiri kila mara kanisani kuwa hapa hakuna masister , kila mtu ataolewa tu. Haijalishi ana umri gani .

Nilipata nguvu ya kujikumbuka , nikaomba kwa Mungu kuwa kama ninafaa kuolewa niolewe na mtu ambaye ana hofu ya Mungu . Sasa ninaye na nipo vizuri tu . Tunaishi kwa upendo mkuu na wanangu wanampenda baba yao wa kufikia.

Niliwahi kuomba Mungu anipe watoto wachungaji na sasa imekuwa , Namshukuru Mungu kwa matendo yake .

USHUHUDA

Naitwa mtumishi ELIAS MAGONGO au baba safina .Namshukuru mtumishi wa Mungu baba yetu mtumishi BENSON MPELE , kwani tunaye baba atakayetufikisha mbinguni .

Nilifunga Ndoa mwaka 2018 nawashukuru nyote mliokuwa pamoja na mimi . Kuna ambao waligeuka kuwa baba zangu na mama zangu katika ndoa yangu . kwani baba yangu mzazi alikataa kufika katika ndoa yangu , kwa kuwa ilikuwa inafungiwa kigoma . Mimi nilipenda ndoa yangu ifungiwe katika madhabahu ya kigoma .

Kwangu ndoa ni ya kwangu na si ya baba yangu nilisimamiwa na watakatifu washirika wenzangu na hata kulipa mahari na kufunga ndoa .

Mama yangu mzazi nilikuwa simjui kwani sikuwahi kumuona . Namshukuru Mungu katika harakati za ndoa na kwa msaada wa mtumishi BENSON niliweza kukukutana na mama . aliweza kufika katika harusi yangu , huku akinishangaa kuwa ana mtoto mkubwa ambaye alimuacha kwa muda mrefu . kwani mimi nililelewa na baba kuanzia nikiwa mdogo.

Namshukuru Mungu Mama yangu na ndugu zangu walipofika katika harusi yangu waliokoka na kumpokea Yesu.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Kigoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Kusanyiko la NNe kigoma
TAREHE 22/12/2019
MAPOKEZI KIBONDO
MPANDA
Ibada ya Mkesha tare 31.05.2019
HIVI NDIVYO MFUNGO WETU ULIVYOISHA
UFUNUO WOWOTE UNANGUVU NDANI YAKE. Kamwe ufunuo hauwezi kukuacha kama ulivyokuwa
Mwezi wa mfungo (TUMEUNGANA MUBASHARA KUTOKA MWENGE)Kuimba sifa na Kucheza

Location

Telephone

Address

Kigoma
Other Religious Organizations in Kigoma (show all)
Hope Katumbi Orphanage Hope Katumbi Orphanage
Katumbi Village
Kigoma, 255

Church Orphanage Center

BrockMinistries BrockMinistries
Kigoma
Kigoma, 47309

Daniel and Susan Brock