Efatha Ministry Kahama

Efatha Ministry Kahama

WE BRING THE WORLD TO JESUS

IJUMAA HII TAREHE 31.05.2019,
USIKU MTAMU USIKU WA KULA NA KUONGEA NA MUNGU KARIBUNI WAKAZI WOTE WA KAHAMA NA VITONGOJI VYAKE TUJE TUFURAHI NA MUNGU WETU KIMBILIA KWA YESU MAANA SAA YA WOKOVU NI SASA.

NAIBARIKI Jumamosi yangu, BABA Asante, Nakushukuru kwa PENDO LAKO, Asante kwa MAARIFA na UFAHAMU wako, SITAKUWA kama NILIVYOKUWA, MIMI NI MSHINDI, MIMI NI KICHWA, MIMI NI WA KWANZA, BABA Asante, NITAHESABU Mapato yangu huku NIKISHANGILIA, Maana PENDO LAKO LINANIPA YOTE MEMA, KWAKO BABA SITAPUNGUKIWA NA KITU, YOTE YANAWEZEKANA KWAKO BABA, Nakupenda, Nakufurahia BABA, Asante, Nakushukuru, NIMEBARIKIWA na Jumamosi yangu.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SABA.

Kijana ambaye unataka Kuoa au Kuolewa omba Mungu akupe MTU SAHIHI ambaye mtatembea naye katika Njia moja na siyo kufuata Pesa.
Usiingie mahali kwa tamaa au kwa sababu unataka kitu, Ndoa ni ya Muhimu sana na ni Mali ya Mungu acheni kudanganyana.

Oa au Olewa na mtu ambaye UNAMPENDA na Yeye ANAKUPENDA ili hata kama itatokea dhoruba ya aina gani katika Maisha yenu mtaweza kusimama pamoja.

MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA - EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SABA.

Katika Ndoa si kwamba ni bondeni kama watu wanavyofikiri kwamba hakuna changamoto, kuna milima, mabonde na changamoto na ni lazima ukubali kuzitatua, kama umekubali kufunga Ndoa na huyo mtu na ukasema Unampenda jipinde kupambana na hizo changamoto mpaka ushinde. Watu wengi inapofika mahali pa Kuoa au Kuolewa wanawaza kuwa kuna raha tu siku zote la! Kuna Kazi unatakiwa kuifanya.

- Wewe kijana kabla ya Kuoa au Kuolewa sikiliza kwanza Mafundisho huku ukimuomba Mungu, atakupa unachokitaka, Mungu si kama mwanadamu na Mungu hayupo mbali ukimuomba atakujibu.

- Usioe kwa sababu ya TAMAA au MUDA UMEENDA Muombe Mungu akupe wa Kufanana na Wewe.

Kuoa na Kuolewa ni MAISHA YA MILELE hivyo hakuna sababu yoyote ya kuachana, ingia kwenye Ndoa huku ukielewa hilo, kwani kwa wewe kuelewa hilo hakuna kitu ambacho kitakushinda, Oa au Olewa na mtu Unayempenda.

MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA - EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SABA.

Mwanzo 28:6-9 “Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani, na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu. Esau akaona ya kuwa binti za Kanaani hawakumpendeza ….”

Yakobo alikuwa mtii kwa wazazi wake na akafuata maagizo aliyopewa na wazazi wake hata kuhusu swala la kuoa, Yakobo alibarikiwa kwa sababu alikuwa mtii na msikivu. Esau nduguye Yakobo hakusikiliza mausia ya wazazi wake akajitwalia mke kutoka katika kabila ambalo wazazi wake hawakupenda, mwisho wa siku akaoa wanawake wengi sana, usiposikiliza mahusia unayopewa na wazazi wako au watumishi wa Mungu utaoa wanawake wengi sana.

Waamuzi 14:1-3 “Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko ……..”

Samsoni ni mtoto ambaye alipatikana kwa Neema ya Mungu na mama yake baada ya kupewa mtoto huyo akapewa masharti na Mungu ya kufanya ili Samsoni aje kuwa msaada kwa Taifa la Israel, lakini Samsoni hakutaka kuwasikiliza wazazi wake kwa habari ya kuoa hata aliposhauriwa.

Unapotaka Kuoa au Kuolewa angalia mtu atakayekufikisha katika Kusudi lako ambalo Mungu amekuwekea, Samsoni hakuliangalia hilo kwa sababu hakusikia alichokuwa anaambiwa, na Mungu akamuacha ndipo yakamkuta ya kumkuta.

Je! Kuhusu swala la Kuoa au Kuolewa unasikiliza Wazazi na Watumishi wa Mungu wanapo kuonya na kukuelekeza? Samsoni yeye alitobolewa MACHO kwa kutokusikia kwake na habari yake ikaishia hapo, vipi kuhusu wewe?.

Mzazi wako anapokuelekeza si kwamba hakupendi, la! bali anakutakia MEMA.

MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SABA.

Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”

Mungu akikupa mtoto inamaana kuwa amekuamini, na ukimlea huyo mtoto katika njia ipasavyo hataisahau hata atakapokuwa mtu mzima, atakumbuka kuwa mama au baba aliniambia hivi na vile.

Siku hizi tumekuwa tunaona ndoa nyingi zinavunjika, kwa nini? Kwa sababu vijana wetu hawana mafundisho sahihi wanayopokea kutoka kwa wazazi wao yatakayo wasaidia wao kuweza kusimama imara, ni jukumu letu sisi wazazi kuwaelekeza watoto wetu njia iwapasayo wao kuenenda ili waweze kuwa na ubaadae mzuri.

Ndoa si mahali pa kuingia na kutoka au kutembea na kurudi hivyo ni lazima maamuzi yawe sahihi ili usije kujutia baada ya kuingia.

MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SITA.

Baraka ni thawabu ambayo anapokea mtu baada ya kupitia maumivu kwa ajili ya Bwana, Mungu anapo kuona sasa umefikia kiwango cha kumpendeza Yeye ndipo sasa anakupa Baraka kama thawabu.

Huwezi kupokea Baraka kwa maombi, unaweza kupokea UPONYAJI au UKOMBOZI kwa maombi lakini si BARAKA, utapokea Baraka baada ya kupitia MACHOZI na Mungu anapotosheka na machozi yako ndipo sasa ANAKUBARIKI.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SITA.

Ili uweze kuwa na Baraka au ufikie Baraka nini kifanyike?

Zaburi 126:5 “Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.” Kamwe hautapata Baraka kama hukupanda kwa machozi, waangalie Isaka, Yakobo, Musa, Yusufu, Daudi waliweza kufikiaje Baraka zao. Kabla haujapata mbaraka kuna machozi na maumivu utakayo pitia, mfano kwa mama mjamzito kabla hajajifungua mtoto kuna maumivu tele anapitia inamgharimu maji na damu.

Kama unataka kuziona Baraka katika maisha yako kubali kulipa gharama.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SITA.

Kilicho Barikiwa hakina wingi bali kina UTELE, ukiwa umebarikiwa unaweza ukawa na milioni kumi lakini ukajenga nyumba ya milioni mia, ambaye hajabarikiwa hata akiwa na milioni mia moja akitaka kujenga ataanza kujenga lakini nyumba haitaisha ile pesa itakuwa imeisha.

- Baraka maana yake ni utoshelevu, kinacho kufanya utosheke na kile ulicho kuwa nacho hiyo ndiyo inaitwa Baraka.
- Baraka zipo ili kutosheleza uhitaji wako na si matakwa yako,
- Mafanikio hayawezi kutimiliza uhitaji wako bali ni Baraka pekee ndiyo inaweza kutimiliza uhitaji wako,
- Mafanikio hayawezi kutambua uhitaji wa mtu mwingine la! Siku zote mafanikio yanakuvuta wewe kutaka yaliyo juu zaidi na zaidi lakini Baraka zina kazi ya kukufanya wewe kufikia mahitaji yako na kwa kila mtu ambaye unatamani apokee yatamfikia; Kwa nini? kwa sababu Baraka huleta utoshelevu hivyo kila mtu aliye karibu na wewe uliye Barikiwa atatosheka.

Katika Baraka hakuna kitu kinachoitwa UVUMILIVU bali kuna KUPENDANA, KUHESHIMIANA, KUSAIDIANA na KUSONGA MBELE.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA SITA.

Baraka ni nini? Baraka maana yake ni kumcha Mungu, Zaburi 128:1 “Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.” Ukimcha Yeye basi unayo heri, kumcha Bwana ndiyo chanzo cha Baraka hivyo unapo mcha Mungu maana yake ni kuwa unampendeza na upo katika mapenzi na Yeye.

Unapo waambia watu mimi nimebarikiwa maana yake ni kuwa unamcha Mungu, tutajuaje kuwa unamcha Mungu? Tutaangalia namna ya maisha yako, tabia za mke wako na watoto zikoje na mazingira yako kwa ujumla.
Baraka ina mtembeo wake, mtu aliyeanza mtembeo wa Baraka anakuwaje? Zaburi 128:2 “ Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.” popote atakapo kwenda atakuwa heri na kwake kwema.

Ukiwa umebarikiwa hauhitajhi kujipigania yupo anaye kupigania.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA MINISTRY.

EFATHA MINISTRY

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
IBADA YA TAREHE 5/5/2019 EFATHA MINISTRY MWENGE.

Msamaha ni kwa faida yako wewe mwenyewe, kusamehe sio kwa sababu yule aliyekukosea amekufanyia mazuri la! Msamaha unatokana na wewe kuelewa kwamba unasamehe kwa faida yako, usiposamehe moyo unajaa uchungu na maumivu ambayo yanasababisha shinikizo la damu (high blood pressure).

Wa mama wengi wanashikwa na shinikizo la damu kwa sababu mume anachelewa kurudi nyumbani, inawezekana amechelewa amepita kwa ndugu na jamaa zake hii sio dhambi, hakuna mahali Biblia imeandikwa kuchelewa kurudi ni dhambi lakini wewe mama unakasirika na kuwa na uchungu moyoni mpaka unalala ukiwa hujasamehe hii ni dhambi, ndio maana nawaambia Neno la Mungu likae ndani yenu ili muweze kutofautisha nini ni dhambi na nini sio dhambi. Kukasirika mpaka ukawa na uchungu ni dhambi, Mwanamke usikasirike pale mume wako anapochelewa kurudi nyumbani na hajakuaga kwani si dhambi. Ili abadilike ni lazima anywe maziwa yasiyo ghoshiwa ambayo ni Neno la Mungu.

Hakikisha una badilika kupitia Neno.

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA (Siku ya 4)

Leo Mungu ataiviringisha aibu yako. Aibu yako yote ataiviringisha mbali na wewe. Na BWANA ameirejesha mamlaka yako.

Umesafiri safari ndefu bila ushindi, lakini leo ushindi umerejeshwa kwako. UTATEMBEA KWA USHINDI.

Ulikuwa mdogo lakini wewe sio mdogo tena. Wewe ni mtawala wa maisha yako, hakuna aliye juu yako bali Yesu peke yake.

Ulikuwa umekwama, lakini sasa una safari ya ushindi.

Ulikuwa na uhitaji, lakini sasa meza imeandaliwa kwa ajili yako.

Ulikuwa mfu, lakini sasa umefufuka.

HAKUNA KUSHINDWA TENA, HAKUNA KURUDI NYUMA, HAKUNA AIBU, KUOGOPA, KUPAMBANA, KUNG'ANG'ANA, MAGONJWA WALA UHITAJI KWAKO.

#SHANGILIA

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA - SIKU YA TATU.

Zaburi 45:11-12 “Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. Na binti Tiro analeta kipawa chake, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.” Unapojua namna ya KUJISALIMISHA na KUJITIISHA mfalme atautamani uzuri wako, vivyo hivyo kwa mabinti, mabinti wanao jua kujitiisha kwa waume zao wanapendwa zaidi, muda umewadia kwako wewe kujionyesha kwamba unaweza kuaminika.

Jifunze zaidi kuhusu MUNGU ndipo UTASTAWI, nimekuja kugundua kuwa USTAWI NI RAHISI MNO, huwezi kupata USTAWI kupitia jasho lako labda uwe umepata KIBALI kwa MUNGU, unahitaji nini ili USTAWI? Unacho hitaji ni KUJITIISHA kwa MUNGU, kwa wewe kufanya hivyo YEYE anakuwa MPAJI wako hivyo tu, na mwishoni unaishia kuwa mtu ALIYESTAWI.

Ayubu alipoteza kila kitu lakini ALIJITIISHA kwa Mungu na mwishowe Mungu alimfurahia na ndipo aliamuru vitu vimjilie na akawa TAJIRI zaidi ya alivyokuwa mwanzo. KUJITIISHA ni jambo la msingi sana kwako kama unataka KUSTAWI.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – EFATHA MINISTRY.

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA (SIKU YA 2)

Kufunga na kuomba haimaanishi kuwa sasa umekubaliwa na Mungu na unastahili kupokea yale unayotaka, bali unafunga na kuomba ili kujiweka katika nafasi ya kumsikia Mungu.

• Unapofunga na kuomba unajiweka katika nafasi ya kuweza kuyafanya mapenzi ya Mungu.
• Kufunga na kuomba kunakusaidia wewe uweze kutembea katika njia ya Mungu.
• Unapofunga na kuomba, maana yake unamwambia Mungu, dunia na kila kitu kuwa “ninafunga shughuli za kidunia ndani yangu au katika maisha yangu, kwasababu nataka kufungulia mambo ya kiroho kwangu.”
• Kufunga sio kukoma kula bali ni kitendo cha kitu na ni mtembeo wa jambo.
• Haufungi ili kusababisha uzito wako upungue!!!
Hana mama yake Samweli alipofunga tuliona matokeo, Yabesi alipofunga tuliona matokeo.

KUFUNGA MAANA YAKE UNAFUNGA ULE UPUMBAVU WAKO NA KUFUNGULIA UFAHAMU WAKO.
• Unafunga ili kuzuilia ulimbukeni wako na ujinga wako ili uweze kufungulia tabia na sifa njema.

KUFUNGA NI UFUNGUO
• Kufunga maana yake unazuia kitu, na unapofungulia ili uruhusu kitu kitokee.

Mfano: Unapofunga kuanzia asubuhi mpaka jioni maana yake unataka yale mambo yanayokuzunguka yakome.
Usifunge kwasababu mtu amekudhihaki, au kwasbabu unahitaji chakula au unahitaji hela; bali funga kwasababu unataka kuuzuia ulimwengu usikushugulikie lakini unataka Mungu akushughulikie.

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA KWANZA:

Bwana Yesu ndiye anaye tutunza na Yeye amelipa deni zetu, usiruhusu adui akuonee kwa maana deni zako zimelipwa pale msalabani tayari.

Ukielewa haya ninayo kufundisha utakuwa huru kweli kweli kwa maana mema yatakujilia, kwani imeandikwa “mjue sana Bwana ndipo mema yatakujilia” hii inamaana kuwa usipo Mjua Mungu kamwe hautayaona mema kutoka kwake.

Siku nilipo mjua Bwana ndipo tabu yangu iliisha, uchovu ulikoma na sasa natembea katika Utukufu wa Bwana, Mungu anayo MEMA kwa ajili yako lakini kwa nini hauyapati? Ni kwa sababu bado una utoto ndani yako. Katika uhalisia wa kawaida mtu anapokuwa mtoto mdogo mali zake zinalindwa na kuhifadhiwa lakini atakapofika mahali pa kujitambua mahali pa UWANA humilikishwa mali zake mwenyewe, ukimjua Mungu unafikia kiwango cha kuwa MWANA na ndipo Mungu anaachilia aliyo kukusudia uwe nayo.

Ukifikia kiwango cha kuwa MWANA shetani hawezi kukuzuia wala wanadamu pia.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – EFATHA MINISTRY.

Huduma ya Efatha Kahama Chini ya mtumishi wa Mungu Emmanuel Urassa tunayofurahaa kubwa kukualika kwenye mwezi wa kufunga na kuomba mwezi wa tano kuanzia tarehe 1 hadi 31, muda ni kuanzia saa kumi jion hadi saa kumi na mbili.

Ushuhuda,
Napenda kumshukuru Mungu maana Ameniponya katika nguvu ya mauti, tambua ya kwamba Shetani ananguvu lakini hana nguvu ya ZIADA sisi tunanguvu ya ZIADA na hii ndiyo iliyo nisaidia hadi nikatoka katika mauti nimemwona Mungu. Pale unapopita katika majaribu Mkumbushe Mungu naye atarejea katika neno lake na kukutoa katika Maumivu unayoyapitia.

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA EFATHA – MINISTRY.

UJUE UZAO WA KIUNGWANA.

Uzao wa kiungwana wanapokuwa mahali huchukua majukumu. Akifika mgeni ni lazima wamtafutie mahali pa kukaa kwa kuwa wanajua majukumu yao. Wanawaza kufanya mambo au vitu kwa ubora, kujenga heshima na hawafanyi vitu vya aibu. Uzao wa kiungwana na wa kifalme unaheshimika. Haijalishi umezaliwa katika hali gani kwa sababu mtu hawezi kuchagua mahali pa kuzaliwa laki bado mtu anaweza kuwafanya watoto wake waishi kifalme na kiungwana kwa kupanga utaratibu wa kuishi ili wawe watu bora katika jamii yao.

Kama unataka kwenda mbinguni ni lazima uwe na Nguvu ya Mungu ndani yako itakayokupa mahusiano mazuri na kukuwezesha kufanya mapenzi yake kwa ukamilifu. Wana Mungu wanao kwenda Mbinguni hawawezi kustawi kwa kutumia nguvu za giza, lakini wana uovu wanastawi kutumia nguvu za giza kwa sababu ndiyo fungu lao.

Hivyo ukiona jambo lolote linakusumbua jua kwamba ndani yako Nguvu ya uwezesho imekosekana, kwahiyo itafute Nguvu ya Damu ya Yesu inayozidi nguvu zote ili iweze kukuvusha katika jambo au tatizo linalokusumbua.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA –
EFATHA MINISTRY.

Katika ibada ya jumapili ya tar 10.03.2019
SOMO : MAISHA YA IMANI.
MCH EMMANUEL URASSA

Bidii yako katika IMANI ndiyo inayokupa maisha toka Mungu yanayoleta maana halisi ya wokovu wake kwako.
Bidii ya mtu katika imani,husababisha neno la kitume limjilie hayo mtu,kisha kubadilisha hali na mazingira yake.
* Kila mtu ana Mungu lakini kumwona Mungu katika maisha yako inategemea sana bidii yako katika imani uliyonayo.
* Kusema mimi sio mdhambi haitoshi bali kinacho kutoa katika dhambi ni yale maamuzi yako ya kimani, kumbuka Imani ni Mungu mwenyewe.
* Wakati wote mtu wa Imani anaushinda ulimwengu [ 1Yoh5:4 ] mtu wa Imani hakataliwi.
• Je watu wanapokutaja,wanakutaja katika nini wewe?
- Ni katika mema au mabaya
- Ni katika Matakatifu au dhambi na uovu.
CHAKUFANYA
* 1pet 2:1 usipoyaweka mbali haya; uovu wote, hila zote, unafiki wote, husuda zote, na masingizio yote.( Chukia dhambi yote na ukajitenge na uovu wote ), ndipo Imani yako italeta maana.
NAMNA YA MTU WA IMANI Ni BIDII KATIKA
• Kusikia yaliyo ya imani yake.
• Kusema alichosikia na kuamini.
• Kutenda alichosikia katika Imani yake.
Mambo hayo matatu ndio chakula cha imani,huifanya imani kua hai ( inamatendo ) na yenye nguvu ndani ya mtu.

* Bidii ya mtu katika Imani yake husababisha watu wengine waitii ile Imani,ndiposa ajabu nyingi na ishara zinafanyika kwa mikono ya wazee wa Imani na makuhani au viongozi wa kiroho.
* Umezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyo haribika,mbegu ya neno Neno la Mungu umezaliwa na Mungu.
* Siku ukijitambua kilamtu ataiona Imani yako na kuitii,ndipo utaona Imani yako ikikutengenezea nafasi katika mazingira yako na katika jamii yako pia.
* Haya ni maisha ya ushindi hivyo kila kitu utakifanya kwa ushindi wa asilimia miamoja.
* Dhambi, ni kitu kilicho kufa hakuna uhai ndani yake,hivyo basi, ikiwa wewe ni hai basi hautakiwi kutajwa wala kukuta katika dhambi.........

Efatha Ministry Kahama

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
IBADA YA MKESHA WA MWAKA 2019.

2019 NI MWAKA WA USHINDI, wewe uliyekuwa unashindwa darasani hautashindwa tena, uliyekuwa unashindwa kwenye ndoa hautashindwa tena, uliyekuwa unashindwa na magonjwa hauta shindwa tena, maana Bwana ameruhusu afya tele.

MWAKA HUU kutakuwa na mambo saba yatakayo tokea, kuna wengine yatawatokea yote kulingana na walivyo elewa.
- Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa marejesho makuu katika maisha yako, Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.”

• Mwaka jana mwaka wa nguvu kulikuwa na mambo ambayo yalikuwa ni magumu sana lakini Mungu aliruhusu Nguvu yake itujilie ili tushinde. Kilichokuvusha mwaka 2018 ni Nguvu ya Mungu pekee.

• Kwa sababu huu ni mwaka wa UREJESHO kutakuwa na UTELE katika maisha yako, katika nyumba yako hautahangaika kuhusu chakula.

• Na kwa vile ni mwaka wa urejesho kutakuwa na mashangilio makuu maana Mungu atasababisha urejeshewe vile ulivyo poteza.

• Mwaka huu ni mwaka wa pekee ni mwaka wa marejesho, kila iitwapo leo utaona marejesho katika maisha yako, hata wale watu ambao walikuwa wanakung’ong’a watarejeshwa, kila biashara uliyokuwa unaifanya ikawa inakwama kwama inakwenda kurejeshwa na Bwana.

- Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa ukombozi wa milki, nyumba za kupanga hazitakuwa juu yako tena utakuwa na zakwako na wewe utapangishia wengine maana Bwana atakurejeshea. Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.”
• Mwaka huu ni kipindi chako cha kumiliki maana Bwana ameridhia ukombolewe, usiogope kuanza kujenga kwa sababu hauna fedha anza na tofali moja Bwana atamaliza.

• Mwaka huu Bwana ataleta moto ili kulamba adui zako nao watateketea, Mungu atasababisha moto ndani yako ili kulamba wale wanao inuka kinyume chako nao watateketea.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Kahama?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


Mbulu
Kahama
KAHAMA
Other Religious Organizations in Kahama (show all)
Family Vision Foundation Family Vision Foundation
P.O BOX 629
Kahama, P.O BOX 629 KAHAMA

MTOTO NA Kijana Kwanza MTOTO NA Kijana Kwanza
P.O BOX 237 KAHAMA
Kahama

releasing children from poverty in Jesus name

Mwenyehaki KIDS Prayer Mwenyehaki KIDS Prayer
S. L. P 856 KAHAMA
Kahama, +255

International Evengelism Church

FPCT Shalom Temple FPCT Shalom Temple
Nyihogo
Kahama, BOX 350

Official Page FPCT Shalom Temple Church Kahama Town,Box 350 Kahama Town.