Ndugu Wafransisko Wakapuchini Tanzania

Ndugu Wafransisko Wakapuchini Tanzania

Comments

Aman na salama
HAPPY ST FRANCIS DAY
TOENI MAJIBU MNAYOULIZWA
Nawatakia heri ya mwaka mpya 2018, ndugu zangu wote Wafransisko wakapuchini, God Bless you.

Shirika la Ndugu Wadogo Wafransisko Wakapuchini lilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1528. Hili ni tawi mojawapo la familia tatu za Shirika la kwanza.

Shirika la Wafransisko lilianzishwa na Mtakatifu Fransisko wa Assizi aliyeishi huko Italia. Alizaliwa kati ya 1181 na 1182 mjini Assizi katika familia tajiri. Baba yake alikuwa Petro Bernadone ambaye alikuwa mfanya biashara na mama Yohana Pika. Fransisko alipokuwa kijana alimsaidia baba yake shughuli za biashara. Kama vijana wengine alipenda maisha ya starehe na umaarufu. Mwaka 1202 mapigano yalitokea kati ya Assizi na Perugia. Kwa vile Fransisko alipenda kupata umaarufu hivyo basi alijiunga katika vita hiyo. Kwa bahati mbaya baadhi yao na yeye akiwemo walitekwa na kuwekwa gerezani huko perugia. Alipoachiwa huru na kurudi Assizi hamu yake ya kutaka umaarufu ilikuwa bado inamsukuma. Vita ilitokea tena Apulia kati ya majeshi ya mfalme na ya Papa. Fransisko alijiandaa kwa ajili ya kujiunga na vita hiyo na kuanza safari mara moja kwenda Apulia ili atimize shauku yake ya kuwa sharifu. Akiwa njiani kuelekea vitani siku ya kwanza ya safari alipofika Spoleto usiku, alisikia sauti katika maono ikimwambia "Fransisko unakwenda wapi namna hii?...unamtegemea nani--Bwana au mtumishi?...kwa nini unamfuata mtumishi badala ya Bwana?" Fransisko akajibu: "Nifanye nini Bwana?" "Rudi katika mji wako Assizi na huko itabainishwa kwako jambo la kufanya na utaelewa maana halisi ya njozi yako. Tungeweza kusema jibu hili la Fransisko ni kama sala yake ya kwanza akiomba Mungu amjulishe jambo la kufanya. Sala hii "Nifanye nini Bwana?" inafaa pia kwa wote wanaojikuta njia panda katika mchakato mzima wa kuutambua wito wao. Ndoto ya Fransisko ya kujipatia utukufu, umaarufu na usharifu wa kidunia ilibadilika hadi kujitenga na malimwengu na kutaka kuwa sharifu wa Kristo kama alivyosema mwenyewe katika wosia wake; "Nilipokuwa dhambini nilichafuka roho, nilipowaona wakoma halafu Mungu mwenyewe akaniongoza nijiunge nao, hapo niliwaonea huruma. .... Kilichonichafua zamani sasa kikawa kwangu kitulizo cha roho na mwili. Baada ya hayo sikukawia kujitenga na malimwengu." (Wosia 2-3) Wengi walivutwa na mtindo wa maisha yake wakajiunga naye. Idadi ilipoongezeka Fransisko aliandika kanuni ya kuwaongoza katika maisha yao ya pamoja. Kanuni hiyo ambayo msingi wake ni Injili ya Yesu Kristo ilikamilika mwaka 1223. Safari ya maisha yake ilipokaribia mwishoni mwaka 1224 akiwa anasali juu ya mlima La Verna, Kristo Msulubikwa alimshirikisha Fransisko mateso yake kwa kumzawadia madonda yake Matakatifu. Zawadi hiyo alikaa nayo kwa miaka miwili hadi dada Mauti alipomtembelea mwaka 1226 alipoaga dunia. Fransisko alitangazwa Mtakatifu mwaka 1228, miaka miwili tu baada ya kifo chake. Shirika la Ndugu Wadogo Wafransisko Wakapuchini lilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1528. Hili ni tawi mojawapo la familia tatu za Shirika la kwanza la Mt. Fransisko wa Assizi. (Wafransisko Wakapuchini, OFM Cap, Wafransisko Wakonventuali OFM Cov. na Wafransisko, OFM

Form Four 2018 : MAUA Seminary Kilimanjaro

Hii ni Form Four ya Kwanza tangu shule ianzishwe. Kwa kweli wamefanya vizuri sana. Hongereni sana uongozi wa shule walimu wote pamoja na uongizi wa shirika.

Hongereni sana uongozi wa Maua Seminari, walimu wote pamoja na uongozi wa Shirika. Kwa kweli shule zote mbili zimefanya vizuri sana.

Padre Corado Pre and Primary English Medium School Kongwa Dodoma

Photos from Ndugu Wafransisko Wakapuchini Tanzania's post

Capuchin Boys Secondary School-Mivumoni, Pangani

Mahafali ya Kwanza ya Kidato cha Nne- Capuchin Boys Secondary School - Mivumoni, Pangani

Photos from Ndugu Wafransisko Wakapuchini Tanzania's post

Capuchin Boys' Secondary School
Mivumoni-Pangani.

[07/03/17]   BABA YETU MT. FRANSISKO WA ASIZI
Muungama na Mwanzilishi wa Mashirika Matatu
-----------------------------------------------------------
Fransisko alikuwa mtoto wa Petro Bernadone, mfanya biashara tajiri wa Asizi. Petro alidhamiria kuwa mwanae wa kwanza angerithi kazi yake. Lakini Fransisko kwa namna yo yote hakuwa na uroho kama baba yake. Bali, alikuwa mkarimu sana na katika hali ya uchangamfu na ucheshi alitoa chochote kilichokuwa chini ya mamlaka yake.
-------------------------------------------------------------------------------------------
Bwana wetu, ambaye furaha yake ni kuonesha huruma kwa wenye huruma, alidhamiria kumuepusha Fransisko kutoka kwenye hatari ya starehe za kidunia na kumvuta kwake. Aliruhusu Fransisko augue sana. Akiwa amelala katika upweke wa chumba cha wagonjwa, akidhoofika kimwili, roho yake ilikuwa inaandaliwa na Mungu kwa mambo ya juu zaidi. Alijisikia hamu kubwa ya ukamilifu, na kujishinda kishujaa kulihitajika kama msingi wa ndoto hiyo.
---------------------------------------------------------------------------------------------
Siku moja baada ya kupona akiwa amepanda farasi akikatiza uwanda wa Asizi, alikutana na mkoma. Hali hiyo isiyotegemewa, ilimwogopesha, na alitaka kurudi nyuma. Lakini alikumbuka azimio lake, akateremka na haraka akabusu mkono wa yule mkoma na kuweka sadaka kwenye mkono wake. Alipopanda punda tena na kugeuka ili amuage mkoma yule, hapakuwepo na mtu ye- yote kwenye uwanda ule. Inaonekana Kristo alijionesha kwake katika umbo la mkoma.
-------------------------------------------------------------------------------------------
Fransisko aliwapenda mafukara kiasi kwamba mara nyingi alishirikiana nao. Pia akitimiza amri ya Mungu, aliomba mawe ya kukarabati makanisa matatu yaliyokuwa yameharibika. Baba yake alikasirishwa sana na mwenendo huo wa ajabu na kumpeleka mwanae mbele ya Askofu wa Asizi. Hapo Fransisko hakumrudishia tu baba yake pesa alizokua nazo, bali hata nguo alizokuwa amevaa akisema: "Sasa hakika naweza kusema, Baba yetu uliye mbinguni".
-----------------------------------------------------------------------------------------
Askofu alimpa joho kuukuu la mtunza bustani, ambalo kwa nyuma Fransisko alichora msalaba kwa kipande cheupe cha chaki. Kuanzia wakati huo alimwomba Bwana Yesu amfunulie mapenzi yake kuhusu mambo yajayo.
--------------------------------------------------------------------------------------------
Muda si mrefu, Fransisko akiwa kwenye misa takatifu Portiuncula, alisikia injili ambapo Bwana wetu anawatuma mitume wake na kuwaambia wasichukue wala dhahabu, wala fedha, wala makoti mawili, wala viatu. Moyo wa Fransisko ulijazwa furaha, kwani aling'amua mapenzi ya Mungu kuhusu maisha yake. Akiwa amevaa vazi la toba, lililofungwa kwa mshipi, na bila viatu, alianza maisha ya ufukara halisi na kuanza kuhubiri toba. Hii ilitokea mwaka 1208, akiwa na umri wa miaka ishirini na sita hivi.
--------------------------------------------------------------------------------------------
Mara wenzi kadhaa wakajiunga naye. Walipofikia kumi na moja, aliongozana nao kwenda Roma, ambapo Papa Innocent wa III alitoa idhini yake kwa Shirika jipya. Waliishi katika ufukara halisi na katika uelewano wa kidugu, wakihubiri toba kwa watu kwa matendo na maneno yao. Mwanzilishi mtakatifu aliwaita Ndugu Wadogo, ili daima wathamini karama ya unyenyekevu kama msingi wa ukamilifu. Yeye mwenyewe alikuwa mnyenyekevu kiasi kwamba watu walipomwita mtakatifu, alijiita mdhambi mkubwa, "kwani," alisema, "kama Mungu angempa mhalifu mkubwa zaidi neema alizonijalia mimi, angeweza kuzitumia kwa faida kubwa zaidi kuliko mimi nilivyofanya".
---------------------------------------------------------------------------------------------
Shirika lilikua kwa haraka. Mwaka 1219 ndugu zaidi ya elfu tano walikusanyika kwenye mkutano mashuhuri wa mikeka. Kama Kristo alivyowatuma mitume kuhubiri injili kwa mataifa yote ndivyo Fransisko alivyowatuma ndugu zake. Yeye mwenyewe kwa ujasiri alimkabili Sultani wa Misri na kumtangazia kwamba ukombozi unaweza kupatikana kwa Kristo tu.
----------------------------------------------------------------------------------------------
Ili kufungua njia ya ukamilifu kwa wale wote wanaopenda kufuata maisha yake, Fransisko alianzisha Shirika la Pili liliongozwa na Mtakatifu Klara, na Shirika la Tatu kwa watu wote, wake kwa waume. Upendo wake kwa roho za watu ulimsukuma kufanya kazi kwa ajili ya watu wote.
----------------------------------------------------------------------------------------------
Hata hivyo hamu yake ya kuunganika zaidi na Mungu ilimsukuma tena na tena ajitenge na kukaa upwekeni kwa ajili ya kufunga na kusali. Aliwaka moto wa upendo kwa Mungu Mkuu na aliye juu. "Katika uzuri wa vitu," anasema mtakatifu Bonaventura, "aliona Muumbaji wa uzuri wote, na alifuata nyayo za mpendwa wake aliyetia chapa ya taswira yake katika viumbe vyote". Akiwa amejaa upendo aliweza kualika viumbe vyote vimsifu Muumba pamoja naye, na ndege waliungana naye kuimba nyimbo za kumsifu Mungu.
---------------------------------------------------------------------------------------------
Zaidi ya yote ilikuwa ni mateso na kifo cha Kristo msalabani ambavyo viliujaza moyo wake upendo wa Mkombozi wake, na alijatahidi kadiri alivyoweza kufanana na Kristo msulubiwa. Miaka miwili kabla ya kifo chake, katika mlima La Verna, Mwokozi msulubiwa alimtokea Fransisko katika umbo la kiserafi na kumpiga chapa ya madonda matano matakatifu kwenye mwili wake.
---------------------------------------------------------------------------------------------
Fransisko alijua mapema siku ya kifo chake. Ingawaje kilitanguliwa na maumivu makali, alimshukuru Mungu kwa ajili hiyo na kusema wazi wazi kuwa yupo tayari kuteseka hata mara mia zaidi kama ni mapenzi ya Mungu
Akiwa amefarijiwa kwa sakramenti zote za Kanisa Takatifu, na akiwa amelala juu ya ardhi kwa mfano wa kifo cha Mkombozi msalabani, Fransisko alikwenda makao yake ya mbinguni tarehe 3, Oktoba 1226.
-------------------------------------------------------------------

Nd. E.F.N OFM Cap.

[07/02/17]   Mkurugenzi wa Miito,
Ndugu Wafransisko Wakapuchini,
S. L. P. 1522
Dodoma,
Tanzania.
-------------
Simu #
0784 697 045
0759 759 484

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Dodoma
1522
Other Religious Organizations in Dodoma (show all)
Kanisa La Kristo Kanisa La Kristo
Dodoma

CHURCH OF CHRIST (NON DENOMINATIONAL)

Makedonia Gospel Centre-Kisasa,dodoma Makedonia Gospel Centre-Kisasa,dodoma
Kisasa
Dodoma, 542

Kanisa letu zuri linapatikana eneo la Kisasa C centre mkabala na shule ya sekondari ya Kisasa:

Dodoma Christian Fellowship Church Dodoma Christian Fellowship Church
Dodoma
Dodoma

Dodoma Christian Fellowship Church is a Pentecost Church lead by Rev. Past INNOCENT MBYALLU based at Dodoma /Tanzania

The Carpenter's Kids Program The Carpenter's Kids Program
Dodoma

The Carpenter's Kids Program was founded in 2005 to support vulnerable children gaining access to education in Central Tanzania.

TUCASA-IRDP Dodoma. TUCASA-IRDP Dodoma.
138
Dodoma, 41113

special for TUCASA Members at Mipango Institute,sharing ideas on spiritual perspective as well as memory events' photos,also getting informations and chat.

ICC Dodoma ICC Dodoma
Dodoma

We preach the Gospel of Jesus Christ by fulfilling the purpose of Church which is evangelism, fellowship, worship, spiritual maturity and ministry.

Upendo Revival Christian Centre-URCC Upendo Revival Christian Centre-URCC
TAG Upendo Revival Christian Centre
Dodoma, P. O. BOX 1098

Upendo Revival Christian Centre is a Christian Pentecostal Church of the Assemblies of God origin with one purpose: defining Christian Love to all people, Christians and non-Christians, the churched and the un-churched, in towns and in villages.

Mennonite Church Tanzania Dodoma  Iringa Road Mennonite Church Tanzania Dodoma Iringa Road
Box 3230
Dodoma, 255

Kila mwenye pumnzi na amsifu Bwawa

Jireh Ministry International Jireh Ministry International
[email protected]
Dodoma

Welcome to the Official page for the potter's House and YEHOVA-YIRE INTERNATIONAL Ministries "On the mount of the LORD it shall be provided.

MoreGrace International Ministry - MGIM MoreGrace International Ministry - MGIM
[email protected]
Dodoma, +255

Building people spiritually, knowledgeable, intellectually.

TAFES UDOM TAFES UDOM
UDOM
Dodoma, 0105

TAFES NI FELLOWSHIP YA KIKRISTO ISIYOFUNGAMANA NA DHEHEBU LOLOTE, TUNAPATIKANA COLLEGE ZOTE HAPA UDOM, KARIBU UABUDU NASI