AICT Kizota Local Church Dodoma

AICT Kizota Local Church Dodoma

Comments

Samahani nauliza huku Ihumwa kuna kanisa la Aic
Ni jumapili ya kupendeza mbele za Mungu, hakika uwepo wake ulionekana katika ibada ya tarehe 25/11/2018
JUMAPILI YA TAR 25.11.2018
JIANDAE KUKUTANA NA MUNGU WAKO! Alichoonyeshwa Angelica kuhusu Mbinguni, Kuzimu na Kurudi kwa KRISTO Jina langu ni Maxima Zambrano Mora, tunasali kanisa la "Casa de Oracion" huku El Empalme. Tulikuwa katika kufunga kwa siku 15, na kulia kwa Mungu. Binti yangu Angelica aliungana nasi pia. Katika kipindi hicho cha siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya asili, ambayo sijawahi kuona kabla. Tulikuwa tunaomba na kufunga katika kipindi maalumu cha kumtafuta Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri Mungu aseme nasi. Bwana alitutia matumaini makubwa sana. Kwaajili ya majaribu yetu tulikaribia kukata tamaa, lakini Bwana alikuwa pamoja nasi kutusaidia. Alitupa neno la YEREMIA 33:3 "NIITE, NAMI NITAKUITIKIA, AME NITAKUONYESHA MAMBO MAKUBWA, MAGUMU USIYOYAJUA.” Binti yangu alitia msisitizo sana katika neno hili kwa Bwana, japokuwa sikujua kwa wakati huo. ANGELICA (BINTI MWENYEWE): Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina umri wa miaka 18, na ninasoma katika Chuo cha José María Velazco Ibarra, hapa El Cantón, El Empalme, katika nchi ya Ikwado. Nilimpokea Yesu kama Mokozi wangu kwa mara ya kwanza nilipokuwa na umri wa miaka 12, lakini nilijisemea, “Hakuna rafiki yangu hata mmoja aliye mlokole,” kwa hiyo nikawa najisikia aibu katikati yao. Kwa hiyo, niliachana na Mungu na nikaanza kuishi maisha mabaya. Lakini Mungu Katika sherehe ya kutimiza miaka 15 ya kuzaliwa kwangu, nilipatanishwa na Bwana, lakini bado nilikuwa na roho ya kusitasita ndani yangu. Biblia inasema, “MTU WA NIA MBILI HUSITA-SITA KATIKA NJIA ZAKE ZOTE” (YAKOBO 1:8). Nilikuwa mmoja wa watu wa aina hiyo. Baba yangu alikuwaakisema, “Huna haja ya kuwa hivyo; inatisha; ni makosa.” Nami ningemjibu, “Hivi ndivyo nilivyo, na ndivyo ninavyotaka kuwa! Hakuna mtu wa kuniambia ninatakiwa niweje, au nifanye nini, au nivaeje, au niwe na tabia gani!” Naye alijibu, “Mungu atakushughulikia. Atakubadilisha.” Nilipofikisha miaka 17, nilifika karibu na Bwana. Tarehe 18 Aprili nilimjia na kumwambia, “Bwana, nasikia vibaya sana. Najua kuwa mimi ni mwenye dhambi. Bwana, nisamehe. Naomba uandike jina langu kwenye kitabu cha uzima na unikubali kama mwana wako.” Nikasema, “Bwana, nataka unibadilishe; unifanye kuwa mtu wa tofauti.” Lakini kadiri muda ulivyoendelea, sikuona badiliko lolote. Labda tofauti tu ni kuwa nilianza kwenda kanisani, kusoma Biblia na kuomba. Hayo tu ndiyo yalikuwa mabadiliko maishani mwangu. Ndipo, mwezi Agosti, nilialikwa kwenye mfungo wa siku 15. Niliamua kujiunga, lakini kabla ya kuanza nilimwambia Bwana, “Bwana, nataka ushughulike name hapa.” Wakati wa mfungo, Bwana alikuwa kizungumza karibia na kila mtu, isipokuwa mimi! Ilikuwa kana kwamba Bwana hajaniona. Nilikuwa naumia sana. Niliomba, “Bwana, hautashughulika na mimi?” Nililia peke yangu na kuendelea kusema, “Bwana, hivi unanipenda kweli? Kwa nini husemi na mimi kama unavyosema na wengine? Unaongea mambo mengi kwa watu wengine, hata mambo ya unabii, lakini si kwangu.” Nikamwomba anipe ishara ili kuionyesha kwamba alikuwa pamoja name, na Bwana akanipa YEREMIA 33:3, “NIITE NAME NITAKUITIKIA,, NAMI NITAKUONYESHA MAMBO MAKUBWA, MAGUMU USIYOYAJUA.” Nilisema, “Bwana, hivi umesema nami?” - maana nilisikia sauti yake wazi kabisa na nikaona maono ya maneno yaliyoandikwa YEREMIA 33:3. Nikasema, “Bwana, hayo ni kwa jili yangu?”. Niliyaweka mambo hayo moyoni mwangu kimya wakati kila mtu alikuwa akishuhudia kile ambacho Bwana amempatia na kile alichoona. Niliendelea kutafakari maneno: “Niite” kwamba yanamaanisha kumwomba Bwana; lakini nikajiuliza, “Mambo makubwa magumu” maana yake nini? Niliwaza, “Hii inawewza tu kumaanisha mbinguni na kuzimu.” Kwa hiyo nikasema, “Bwana, ninataka tu unionyeshe mbingu, lakini si kuzimu, maana nimeshasikia kuwa kuzimu ni kubaya sana.” Lakini niliomba kwa moyo wangu wote, “Bwana, kama ni mapenzi yako kunionyesha kile utakacho, basi fanya hivyo, lakini kwanza unibadilishe. Nakata kuwa mtu wa tofauti.” Nilipomaliza mfungo, kulitokea majaribu na magumu na wakati mwingine nilijisikia mdhaifu sana, nikishindwa kuendelea na Bwana. Lakini alinitia nguvu. Bwana ni rafiki yetu mkubwa, Roho Mtakatifu. Nilimwambia “Bwana, wewe ni rafiki yangu mkubwa. Nataka kukufahamu zaidi.” Nilimweleza kila kilichokuwa moyoni mwangu. Niliomba mwezi wote wa Agosti na pia Novemba. Mtumishi mmoja wa Bwana alifika nyumbani kwetu na kusema, “Bwana na akubariki.” Nilijibu, “Amina.” Kisha akasema, “Nimekuja hapa kukuletea ujumbe wa Mungu ... ni lazima ujiandae kwa maana Bwana ataenda kukuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua. Anaenda kukuonyesha mbingu na kuzimu kwa maana umekuwa ukiomba kutoka YEREMIA 33:3.” Nikasema, “Ni kweli, lakini umejuaje? Sijamwambia mtu yeyote kuhusu jambo hilo!” akasema, “Mungu huyo huyo unayemtumikia na kumsifu, ndiye huyo huyo aliyeniambia kila kitu.” Mara tulianza kulia. Baadhi ya akina dada kutoka kanisani kwetu, na wengine kutoka kwenye familia yangu walikuwapo pale pamoja nasi tukiomba. Lakini mara tulipoanza kuomba, nilianza kuona mbingu zimefunuka. Kwa hiyo nikasema, “Naona mbingu zinafunguka na malaika wawili wanashuka kuja!” Huyo mtumishi akaniambia, “Waulize wamefuata nini hapa?” Walikuwa warefu na wenye kuvutia; wakiwa na mbawa za kuvutia. Walikuwa wakubwa na wanang’aa, na walionekana kama waangavu kama kioo, na wenye kumetameta kama dhahabu. Walivaa viatu vya madini kama kioo na mavazi matakatifu. “Mmefuata nini hapa?” Wakatabasamu na kusema, "Tupo hapa kwa sababu tuna kazi ya kufanya….. Tupo hapa kwa sababu wewe unatakiwa ukatembelee Mbinguni na Kuzimu nasi hatutaondoka mpaka yote hayo yatakapotimia." Nikawajibu, “Sawa, lakini mimi natamani kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu” Wakatabasamu na kuendelea kuwapo pale lakini hawakusema lolote zaidi. Tulipomaliza maombi, bado niliendelea kuwaona wakiwa wapo pale. Pia nilianza kumwona ROHO MTAKATIFU. Yeye ni rafiki yangu bora kabisa. Yeye ni MTAKATIFU. Yuko kila mahali! Niliweza kumwona. Alikuwa angavu kama kioo na mwenye mng’ao wa kuvutia sana. Akiwa na uso unaong’aa kwa uzuri, niliweza kuona tabasamu lake na jinsi alivyonitazama kwa upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni mzuri sana kuliko malaika. Malaika wana uzuri wao lakini ROHO MTAKATIFU ni mzuri zaidi kupita wao. Niliweza kuisikia sauti yake waziwazi; sauti iliyojaa upendo mkubwa. Kwa hakika siwezi kuelezea kabisa sauti yake; ni kama radi, lakini wakati huo huo anasema “NIKO PAMOJA NAWE.” Kwa hiyo, nilipambana kwa bidii kuendelea kutembea na Mungu, japo majaribu yalituzunguka kila upande. Tulikuwa tunapita katika kipindi kigumu sana, lakini wakati huo huo tukipata ushindi. Nikasema, “Bwana, mapenzi yako yatimizwe.” Niliendelea kuwaona malaika wale hata nikiwa shuleni, na pia darasani. Nilikuwa mwenye furaha ya ajabu kwa sababu niliweza kuwaona! Mtumishi wa Bwana aliyetutembelea aliniambia nijiandae kwa sababu nilikuwa nakwenda kuona Mbingu na Kuzimu. Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema, “Utakufa.” Haikuwa jambo rahisi niliposikia neno hili. "Nitakufa namna gani? Mbona mimmi bado mdogo sana?" nilimuuliza. Akanijibu, “Usihofu juu ya lolote. Kila kitu ambacho Mungu hufanya huwa hakina makosa kabisa. Atakurejesha duniani ili uweze kuwashuhudia watu kuhusu Mbinguni na Kuzimu, kwa kuwa hilo ndilo Bwana anataka sote tujue.” Nikasema “Amina. Lakini nitakufa kwa kugongwa na gari au nitakufaje?” Mawazo mengi yalinijia akilini mwangu, lakini Bwana akaniambia nisihofu, kila kitu kilikuwa kiko katika udhibiti wake. Nikasema, “Ahsante, Bwana!” Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani toka shuleni, malaika wale bado walikuwa nami, hata nilipokuwa namsifu Bwana. Wao walikuwa hawaongei nami; bali wakati wote walikuwa wakisema tu, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah." Walikuwa wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba yetu wa Mbinguni. Roho Mtakatifu naye alikuwa pale pamoja, jambo ambalo lilinifanya nifurahi. Watu wengi husema kuwa injili inachosha na haina mvuto, lakini huo ni uongo mkubwa kutoka kwa ibilisi wenye lengo la kuwafanya watu wasitafute uwepo wa Mungu. Nami pia nilikuwa nikiamini hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na Bwana na Roho Mtakatifu, najua fika kuwa injili haikeri wala kuchosha. Ni jambo zuri sana kuliko yote hapa duniani! Niliweza kumwona Roho Mtakatifu; kucheza naye na hata kuongea naye. Lakini malaika walikuwa hawaongei nami, bali walikuwa wakimsifu tu Bwana. Ningeweza kusema, “Roho Mtakatifu, twende nami tukafamye jambo hili na lile,” naye angekuwa nami. Niliweza kumhisi na kumwona vema. Niliweza kumwona aliposimama; na niliweza hata kumwandalia kiti cha kukaa. Japokuwa watu wengi hawamwoni, Yeye yupo! Uhusiano huo umeendelea. Hakuna sababu ya kuusimamisha, hasa baada ya mtu kuwa umekutana nao ... hakuna namna ambavyo naweza kuufuta Ninapokumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa hapo kabla, ninamshukuru sana kwa rehema zake na upendo wake kwa wanadamu na kwangu mimi! Tarehe 7 Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani, nilisikia sauti ikisema, “Jiandae, kwa kuwa leo utakufa.” Nilijua kuwa ni Roho Mtakatifu kwa vile nilikuwa namwona. Niliipuuza sauti yake na kusema, “Bwana, sitaki kufa leo!” Lakini alirudia, “Jiandae, kwa kuwa leo utakufa!” Safari hii alisema kwa sauti ya juu zaidi na kwa mkazo mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe unayesema nami; ninaomba tu kupata uthibitisho na baada ya hapo, nitendee kama upendavyo. Nitafanya kila utakaloniambia; najiachia kwako Bwana, japo naogopa, maana najua upo nami, na wewe ni halisi.” Niliomba, “Bwana, yule mtumishi wako uliyemtumia kunipa ujumbe mara ya kwanza, naomba basi mpeleke nyumbani muda huu, nimkute pale, na umpe tena neno hili aseme nami kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.” Sasa, mara zote Bwana maisha yetu ya nyuma, yaliyopo na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo, nilipofika nyumbani nikamkuta mtumishi wa Bwana yukop pale!. Maxima: Binti yangu alipofika nyumbani, tulikuwa jikoni. Angelica alipomwona mtumishi wa Bwana, akasema, “Bwana na akubariki.” Mtumishi wa Mungu akajibu, “Bwana akubariki nawe. Je, uko tayari? Kwa kuwa leo ndiyo siku ambayo Bwana atakuchukua, saa 10 jioni.” Angelica alisimama tu pale kwa mshangao kwamba Bwana amejibu ombi lake na kufanya vilevile alivyomwomba njiani. Angelica: Niliposikia maneno hayo ya mtumishi, nikasema, “Amina ... Lakini sitaki kufa; sitakufa! Hapana, Bwana, naogopa, naogopa sana, ninahofu kubwa!” Mtumishi wa Bwana akasema, “Tuombe ili hofu hiyo ikutoke sasa hivi kwa jina la Bwana.” Nikasema, "Amina" na tukaomba. Ghafla nikajisikia hofu yote imenitoka na furaha isiyoelezeka ikajaa ndani mwangu; nikaanza kuona kuwa kifo ni kitu kizuri kuliko vyote na nikatamani kije! Nikaanza kutabasamu na kucheka wakati kila mmoja aliyekuwapo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika kutoka kwenye unyonge na kuwa mwenye furaha. Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba. Maxima: Binti yangu alijawa na furaha ghafla ndani ya moyo na akaanza kula. Alionja karibia kila kitu kilichokuwapo, huku akisema, “Kama sitarudi, sawa tu; nimeshakula na kushiba.” Angelica: Kila mmoja alianza kucheka na kuuliza, “Kwa nini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni? Una furaha na mwenye raha.” Nikawajibu, “Ndiyo, nina furaha. Ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye. Lakini sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote walinikodolea macho na kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” Macho ya mama yangu yalinitazama kwa mshangao zaidi! Maxima: Binti yangu alianza kugawa vitu vyake. Aligawa vitu vyote; kila kitu! Masista wa kanisani kwetu walikuwa pamoja nasi pale kama kawaida; nao pia kila mmoja alipata kitu kutoka kwake. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi, watanirudishia kila kitu, lakini nisiporudi, watabaki navyo.” Angelica: Naweza kupata picha ya jinsi mama yangu alivyojisikia niliposema maneno hayo. Lakini mimi nilikuwa najisikia furaha tupu, ndiyo maana nikaanza kugawa kila kitu: nguo zangu, kitanda, simu ya mkononi, kila kitu, lakini kwa sharti moja: kama nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka. Maxima: Binti yangu alikuwa na msimamo na nia ya dhati, lakini mimi kama mama, nilishikwa na huzuni sana. Halikuwa jambo rahisi. Niliwaza, “Bwana, muda huo utakapowadia, itakuwajekuwaje?” Sikuweza kuelewa. Na walipoanza kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema, “Dada, njoo tuombe.” Lakini niliwajibu, “Nyie endeleeni tu, nitajiunga nanyi muda si mrefu. Ngoja nimalizie kazi hii.” Angelica: Wote walikuwa wananichunguza mimi tulipokuwa tunaomba. Niliomba, “Bwana, nataka kufanya mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata useme uwongo au ujute. Najua wewe ni halisi. Kama nitakuaibisha baadaye, basi ni bora unichukue moja kwa moja. Lakini, kama nitayafanya mapenzi yako, basi unirejeshe tena; lakini nisaidie kusema ukweli, niandae, nisaidie kuhubiri na kuwaambia watu kutubu.” Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana. Nilimwambia mtumishi wa Bwana, “Usimwambie mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye akajibu, “Sitamwambia sasa, lakini mara Bwana atakapokutwaa, nitamwambia.” Tuliendelea kuomba na kuungana katika duara. Maxima: Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana akamwambia mtumishi wake ampake mafuta binti yangu. Kwa hiyo, baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake mafuta mwili mzima, toka kichwani hadi chini, kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote amepakwa mafuta. KIFO CHA ANGELICA Angelica: Mama yangu na dada mmoja wa kanisani, Fátima Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri walivyokuwa wananipaka mafuta, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika; ni kama kioo kilinizunguka mimi. Ni vigumu kuelezea. Nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea nilivyokuwa nimefunikwa. Baada ya hapo, kila walipojaribu kunigusa walishindwa! Maxima: Tulipokuwa tukimwombea Angelica, nilijaribu kuweka mkono juu yake, lakini nilishindwa! Alikuwa amezingirwa na kitu fulani. Lilikuwa ni jambo la ajabu kweli! Hakuna aliyeweza kumgusa tena! Kifuniko hiki kilianzia kichwani hadi miguuni, karibia sentimeta 30 (inchi 12). Hilo lilikuwa ndilo jambo lililonitisha zaidi mimi. Nimewawekea mikono watu wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili lilikuwa halijawahi kunitokea! Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza kuomba na kumshukuru Bwana. Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni iliyokuwa moyoni ikatoweka, maumivu yakakoma na sasa nikajisikia mwenye raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na ilipofika saa 10.00 jioni, binti yangu akaanguka sakafuni. Angelica: Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa kupumua. Nilisikia maumivu tumboni na kwenye moyo. Nilihisi damu yangu ikisimama, na ghafla nilipata maumivu makali mwili mzima. Nilichoweza tu kusema ni, “Bwana, nipe nguvu; nipe nguvu!” maana niliona sitaweza kustahimili zaidi. Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilikuwa zinanitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika ulimwengu wa roho, si kwa macho ya mwilini, niliona mbingu zimefunguka. Niliwaona malaika, siyo wawili au kumi, bali kwa mamilioni wakiwa wamekusanyika pamoja. Katikati ya hayo mamilioni ya malakika, niliona mwanga ambao mng’ao wake ni mara 10,000 zaidi ya ule wa jua. Na nikasema, “Bwana, huyo ni wewe unayekuja!” Maxima: Alipoanguka chini, tulijaribu kumsimamisha, lakini hakuweza kusimama mwenyewe. Muda huu tuliweza sasa kumgusa. Alikuwa akisema, “Omba. Sina nguvu. Mama, sina nguvu na ninasikia maumivu.” Mwanzo alisikia maumivu kwenye moyo, kisha baadaye yalishuka hadi karibu na tumbo. Tuliendelea kuomba na kumsihi Bwana. Bwana alimwondolea uhai! Sijawahi katika maisha yangu kumwona mtu yeyote akifa. Nilimshuhudia binti yangu, akigugumia kwa maumivu! Halikuwa jambo rahisi hata kidogo! Sikuweza kuelewa maneno yake machache ya mwisho, lakini mwishowe alitulia. Niliweka mikono yangu usoni pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua. Hakuwa na pumzi tena, alitulia kimya kabisa. Nilimshika, alikuwa angali na joto kama kawaida. Nilichukua shuka na kumfunika, na baada ya muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa baridi sana. Nywele zake zikalala kama za maiti; na akabadilika na kuwa baridi kabisa kama barafu. Angelica: Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili wangu unakufa. Kadri Yesu na malaika walivyozidi kukaribia, nikajisikia kuwa ninaondoka, na kwamba sikuwa ni mimi tena. Sikuwa hai tena, nilikuwa nakufa na kulikuwa na maumivu makali! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini, walikuwa tayari wako pale. Nyumba yetu ilijaa malaika, na katikati yao niliona Nuru kali kuliko ya jua! Ilikuwa ni hali ngumu sana; nilisikia maumivu makali wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili. Nilikuwa nalia na kupiga kelele, kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni. Niliuliza, “Bwana, nini kinachotokea? Nini kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa mwili wangu na kurudi ndani yake tena, lakini nilipojaribu, ilikuwa kama kushika hewa tu! Sikuweza kuugusa. Mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya wale waliokuwa wananiombea aliyenisikia! Na nikapiga kelele, “Bwana, nisaidie mimi!” Maxima: Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale. Bwana alinipa nguvu wakati huo kwa kuwa sikujua la kufanya. Alikuwa kama mtu ambaye ni mahututi, aliyepoteza fahamu. Lakini nilijua kuwa yuko salama, maana ile ilikuwa ni kazi ya Bwana. Kwa hiyo nikasema, “Bwana, mapenzi yako yafanyike.” BWANA YESU KRISTO Angelica: Wakati huo nilisikia sauti ya Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya upendo, “Usiogope, Binti, kwa kuwa mimi ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa kukuonyesha kile nilichokuahidi wewe. Inuka, kwa kuwa mimi ni Yehova, ninayekushika mkono wako wa kuume na kukuambia, Usiogope, nitakusaidia." Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti, nikiuangalia mwili wangu, nikitaka kurejea ndani yake lakini bila mafanikio. Niliposikia sauti yake, woga ukanitoka, na sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika wakaanza kufungua njia. Kulikuwa na mwanga mkali ung’aao, na nilipouangalia nilisikia amani ya ajabu. Kadri nilivyoangalia, nilimwona mwanaume mzuri, mrefu, aliyevaa vizuri, alivutia sana kumwangalia, na ambaye mwili wake ulijaa misuli. Ule mwanga ulikuwa unatokea kwake. Kulikuwa na mwanga mkali sana kiasi kwamba sikuweza kuona uso wake! Lakini niliweza kuona nywele zake nzuri za dhahabu ing’aayo na vazi jeupe na mshipi mpana wa dhahabu kifuani pake. Mshipi huo uliandikwa, “MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.” Nilimwangalia miguuni pake. Alikuwa amevaa viatu vya dhahabu vinavyong’aa. Alikuwa ni mzuri sana! Akanyoosha mkono wake kwangu. Nilipomshika mkono wake, haikuwa kama ilivyo ninapogusa mwili wangu. Mkono haukupitiliza. Nikauliza, “Kitu gani kinachotokea?” Naye akasema, “Nitakuonyesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi; kwamba ni kweli kuzimu kupo. Na pia, utukufu wangu nitakuonyesha wewe, ili uwaambie watu wangu wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia ni halisi.” Akasema, "Binti, usiogope.” Alirudia tena kusema hivyo nami nikasema, "Bwana, nataka tu kwenda Mbinguni, lakini siyo kuzimu, kwa sababu nimesikia kunatisha!” Akasema, “Binti yangu, nitakuwa nawe. Sitakuacha huko ila nitakuonyesha mahali hapo kwa sababu watu wengi wanajua kuzimu ipo lakini hawaiogopi. Wanaamini kuwa ni mchezo tu, kwamba na kuzimu ni jambo tu la mzaha, na wengi hawajui lolote kuhusiana nayo. Ndiyo maana nitakuonyesha wewe sehemu hiyo kwa sababu wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika utukufu wangu. Aliposema hayo, niliona machozi yakimtiririka hadi kwenye mavazi yake. Nikamwuuliza, “Bwana, kwa nini unalia?” Akanijibu, “Binti yangu, ni kwa sababu watu wanaoangamia ni wengi zaidi, na nitakuonyesha jambo hili, ili kwamba uende na uwaambie ukweli na pia ili na wewe usije kurudi mahali hapo.” Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. USIKOSE SEHEMU YA PILI YA USHUHUDA HUU UBARIKIWE SANA

Wakati wa kutoa shukrani kanisani

Photos from AICT Kizota Local Church Dodoma's post

Imani Choir

Mhubiri Mch. John Sweya
mwenyekiti Njingo Mrs

Shalom choir katika uimbaji

Ibada ya tarehe 5.1.2020

Mr. Samson Mahalu akitoa matangazo
5.1.2020

Waumini wakitoa shukrani 01.01.2020

Mr.Samson Mahalu katika ibada ya mkesha siku 1.1.2020

Photos from AICT Kizota Local Church Dodoma's post

Photos from AICT Kizota Local Church Dodoma's post

Shalom kwaya wakimwimbia mungu katika ibada ya 01.01.2020

Aictkizota idara ya tehama wakitoa shukrani....

Mr. William Magesse.. Mwenyekiti wa ibada 01.01.2020

Mch. John Sweya, Mr. Mshokela, Baraka, na Godwin wakikamata vyombo na kumsifu Mungu

Tunakutakia kheri ya meaka mpya 2020 Mungu awabariki

From AICT Kizota Local Church Dodoma

Kwaya ya mtakatifu Andrea katika ibaada 29.12.2019

Ibada ya sifa 29.12.2019

follow us on instagram:visit the page and follow us
https://www.instagram.com/aictkizota/?hl=en

Ubatizo 25.12.2019

Ebenezer Choir katika mkutano wa krismasi AICT NDachi
#christgmas2019

Emmaus band katika mkutano wa krismasi AICT NDachi
#christmas 25.12.2019

Unabii choir katika mkutano wa krismasi AICT Ndachi
#christmas2019

Waumini katika ibda ya tarehe 22.12.2019
#christmas friendship & fellowship sunday

Ibada ya tarehe 22.12.2019
#christmas friendship&fellowship sunday

Unabii choir katika huduma ibada ya tarehe 22.12.2019
#christmas friendship&fellowship sunday

waumini katika ibada ya 22.12.2019
#christmas Friendship&Fellowship Sunday

Vijana choir wakihudumu katika ibada ya tarehe 22.12.2019
#christmas friendship and fellowship sunday

Ibada ya tarehe 22.12.2019
#christmas friendship and fellowship sunday

Harusi ya Wiljones Nelson & Wande Dabuya
7.12.2019
Mungu abariki ndoa Yao!

Harusi kati ya Emmanuel Madata na Neema Isanzu
7.12.2019
Mungu Abariki Ndoa Yao!

Ibada ya tarehe 1.12.2019
Mhubiri: Mr. Lukiko

Ibada ya tarehe 1.12.2019
Mhubiri: Mr. Rukiko
Mwenyekiti: Mr. Zablon

Ibada ya tarehe 24.11.2019

Uzinduzi wacd za shalom

KAribu katika ibada y tarehe 24.12.2019
Mhubiri: Mch. Elikana Gonda
Mwenyekiti: Mrs. Tabitha Nkola

Tamasha La Uimbaji
#wikilavijana
7.7.2019

Ibada Hitimisho La wiki la vijana
Mhubiri: Burton Mballa
Mwenyekiti: Aaron Mashenene
#wikilavijana
7.72019

youtube.com

Gospel Concert AICT Kizota

Sasa unaweza kutupata
Kwenye Twitter: AICT Kizota Local Church Dodoma
Instagram: aictkizota
Youtube: AICT Kizota

Please dont forget to subscribe my Channel https://www.youtube.com/channel/UCsWz7YMepoRs0zCJD0T1wWA Welcome again and again,,I'm here to entertain you Today ...

youtube.com

Gospel Concert AICT Kizota

Please dont forget to subscribe my Channel https://www.youtube.com/channel/UCsWz7YMepoRs0zCJD0T1wWA Welcome again and again,,I'm here to entertain you Today ...

Ugawaji Wa Zawadi Kwa Washidi Wa Michezo
(Walawi,Waefeso,Waamuzi)
#wikilavijana
7.72019

Tamasha La Uimbaji
#wikilavijana
7.72019

Unabii Choir
Tamasha La Uimbaji
#wikilavijana
7.72019

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


Dodoma
839
Other Dodoma places of worship (show all)
Jireh Ministry International Jireh Ministry International
[email protected]
Dodoma

Welcome to the Official page for the potter's House and YEHOVA-YIRE INTERNATIONAL Ministries "On the mount of the LORD it shall be provided.

Efatha Ministry-Ihumwa Dodoma. Efatha Ministry-Ihumwa Dodoma.
Bwawani,Ihumwa.
Dodoma

Tunapatikana Mtaa wa Bwawani,Ihumwa.Panda daladala pale sabasaba Dodoma ushuke Flemingo Jeshini,utaona kibao cha huduma kinachokuelekeza ilipo huduma.

Upendo Revival Christian Centre-URCC Upendo Revival Christian Centre-URCC
TAG Upendo Revival Christian Centre
Dodoma, P. O. BOX 1098

Upendo Revival Christian Centre is a Christian Pentecostal Church of the Assemblies of God origin with one purpose: defining Christian Love to all people, Christians and non-Christians, the churched and the un-churched, in towns and in villages.

The capital tz The capital tz
Dodoma
Dodoma

www.capitaltz.com

The Bible Society of Tanzania The Bible Society of Tanzania
Makumbusho/ 9th Street
Dodoma, BOX 175

Box 175 Dodoma +255262324661 +255262324465

Ambassadors MegaFest Ambassadors MegaFest
Dodoma
Dodoma

Youths movement and explosion whose core vision is to see a generation of young people transform by the gospel and living for God's glory

TAFES CBE Dodoma TAFES CBE Dodoma
[email protected]
Dodoma, 2077 DODOMA

TAFES-CBE DODOMA Is an interdenominational movement reaching every student in the campus with the gospel of Jesus Christ.

TUCASA-IRDP Dodoma. TUCASA-IRDP Dodoma.
138
Dodoma, 41113

special for TUCASA Members at Mipango Institute,sharing ideas on spiritual perspective as well as memory events' photos,also getting informations and chat.

TAFES UDOM TAFES UDOM
UDOM
Dodoma, 0105

TAFES NI FELLOWSHIP YA KIKRISTO ISIYOFUNGAMANA NA DHEHEBU LOLOTE, TUNAPATIKANA COLLEGE ZOTE HAPA UDOM, KARIBU UABUDU NASI

Mennonite Church Tanzania Dodoma  Iringa Road Mennonite Church Tanzania Dodoma Iringa Road
Box 3230
Dodoma, 255

Kila mwenye pumnzi na amsifu Bwawa

New Jerusalem uscf-sjut New Jerusalem uscf-sjut
Dodoma
Dodoma, S.L.P 47

SAFU YA KWAYA YETU 1-JACOB YUSUPH-teacher 2-EZRA PAUL-Chair.p 3-SOLOMON GEOFREY-Secretary 4-MPINZILE HAPPINESS-VCP 5-MSAMBA MARIAM-Burser 6-ARON FATAEL-DSP

Christian Council of Tanzania (CCT) Christian Council of Tanzania (CCT)
P.O.Box 1454,
Dodoma

The Christian Council of Tanzania (CCT) was established in January 1934 as a fellowship of Churches and Christians. It was then named the Tanganyika Missionary Council until 1964 when it adopted its current name. The CCT has 12 National Churches