Jireh Ministry International

Jireh Ministry International

Welcome to the Official page for the potter's House and YEHOVA-YIRE INTERNATIONAL Ministries "On the mount of the LORD it shall be provided.

#SABABU_YA_WOKOVU
Walioingia kwenye mokovu
Ili wapate magari au nyumba au mchumba au mke au mume hao ndiyo wanaoangaika.
Luka 9:23
Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, #na_ajikane_mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.

Kuokoka ni kujikana, kujikana ni kufanya maamuzi magumu na kuamua kuishi na Mungu maisha yoyote.

Walioingia kwenye mokovu
Kwa sababu ya kumpenda Mungu hao ndiyo wanao kula mema ya wokovu na kutawala.

Leo hii unaambiwa okoka Yesu atakununulia vitumbua. Na asipo kununulia?

#THAMANI_YA_MAONYO
Maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima, Maana yake anayekataa Maonyo nakataa uzima.
Mtu mwenye Roho wa Mungu hawezi kukataa maonyo kwa sababu unyenyekevu ni tunda la Roho, mtu mwenye Roho Mtakatifu hawezi kuishi nje na maonyo.
Pepo akishaingia ndani ya mtu anafunga mlango wa maonyo.
#neema_ya_Yesu_Kristo_iwaokoayo_wanadamu_ikuokoe_nawewe_mwisho_mwakahu. Amina

Dhiki unayopitia iimarishe imani yako na usiue imani yako. Paulo na Sila walikuwa waaminifu kwa Mungu hata walipokuwa dhiki ndipo neema ya Mungu ikashuka pale gerezani.
Usiipe nafasi dhiki yako ikakutenga na watumishi wa Mungu na kukuondoa uweponi mwa Mungu, kama utaona ni dhiki ya kifo basi ni heli ukafia mikononi mwa Mungu.
#Uwe_na_mwisho_wa_mwaka_mwema

#MJUE_ADUI_YAKO
Ufalme wa rohoni hufanya makao ndani ya moyo wa mtu au roho ya mtu na kumwambukiza mtu huyo tabia za kiroho za ufalme huo.
Ufalme wa Shetani unapopata nafasi ya kufanya makao ndani ya mtu, ndipo Shetani huanza kupigana na watu kupitia mtu huyo.
Remember your enemy is inside somebody.

#DUNIA_YA_LEO
inahitaji watu wenye imani yenye misuli 💪🔥kwa sababu ufalme wa kuzimu unapambana nasi kupita kawaida. Endelea kuimarisha imani yako kila iitwapo leo. Amina?

#ILI_MEMA_YAWEZE_KUKUJILIA

Kanuni moja wapo ya kupenda mema ni kutenda mema. Biblia inamtaka mtu anayependa kutendewa mema yeye kwanza awe mtende mema.

Luka 11:4
Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila aliyetukosea. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
Mungu anatutaka sisi tuwe watenda mema ili mema ambayo tunayahitaji katika maisha yetu yapate kutujili.

Neema ya Yesu na iwe juu yako Amina.
Maliza mwaka uweponi mwa Mungu.

#CHANDA_CHA_MUNGU_JUU_YA_FARAO
kati ya mapigo kumi ambayo mkono wa Mungu ulimpiga farao kupitia Musa, lakini ni pigo moja tu ndilo lililomtoa machozi Farao na kuamua kuwaacha Waisrael waondoke.

adui yako anaweza kupigwa mapigo mengi yakamuumiza na kumjeruhi lakini yasimtoe machozi.
Pigo linalomfanya mtu aliye ndilo pigo linalouma , kwa sababu ni pigo lililoenda moja kwa moja penye maumivu makali yenye kusababisha machozi.
#FAHAMU_KWAMBA
maumivu yoyote yanayosababisha machozi ndiyo maumivu makali kuliko yote.
Farao asingelia Esrael wasingetoka katika utumwa ule.
Usiku ule wa machozi ya farao ndio ulikuwa usiku wa uhuru wa Waisrael.

#NAMI_NAKUOMBEA_KWA_JINA_LA_YESU
Mkono wa Mungu uliompiga farao pigo lililompelekea maumivu yaliyomtoa machozi, umtandike adui yako anayepambana usifanikiwe kupitia uchawi wake na ushirikina wake pigo lenye maumivu makali litakalomfanya audharau uchawi wake na aganga wake na ushirikina wake milele.
#Ameeeeeeen?

UNATAKA KUTAWALA?
JIFUNZE KUPAMBANA.
Kutoka 15:3 BWANA ni mtu wa vita,
BWANA ndilo jina lake.
#Wenye_nguvu_ndio_hutawala_watu.

NAFASI INAYOKUSUBIRI NDIYO INAKUPITISHA KWENYE MOTO MKALI KIASI HICHO
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Danieli 3:20
Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.

Kisha mfalme akawakuza Shadraka, na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli.
#Usimwache_Mungu
#Ameeeeeeen?

#KUDHARAULIWA_SIYO_KIFUNGO_CHAKUJIDHARAU
1Samweli 16:3
Daudi alidharauliwa na baba yake na ndugu zake ndiyo maana hata kwenye ibada iliyofanyika nyumbani kwao hawakuona sababu ya yeye kutaarifiwa wakaona acha Daudi achunge kondoo lakini wao wakae ibadani.
Maana yake, hawakuona hata thamani ya Daudi kuwepo ibadani.

Daudi alijiheshimu na kujiamini mpaka kuthubutu kupambana na simba na dubu.

Daudi alijiheshimu na kujiamini mpaka kwenda kwa mfalme na kumuhakikishia kwamba anaweza kupambana na Goliati na kumwangamiza.

Daudi alijiheshimu na kujiamini hata kwenda vitani na mawe badala ya siraha za vita.

Daudi alijiheshimu na kujiamini katika jina la Mungu aliye hai hata kulipelekea taifa la Israel heshima kubwa duniani.

#HELOOOOOOO
kudharauliwa kwako na ndugu zako hakumaanishi na wewe si chochote si lolote
#HELOOOOOOO
shetani hapiganagi na watu dhaifu, Shetani hupigana na watu waliobeba heshima ya ukoo wao, familia zao, na taifa leo.
#HELOOOOOOO
Shetani hupambana na watu wenye hatima kubwaaaaaaaa.
#HELOOOOOOO
vita yako inakutambulisha ulichobeba ndani yako

#POKEA_NEEMA_YA_KUSHINDA_NA_ZAIDI_YA_KUSHINDA_KWA_JINA_YA_YESU.
Sema ameeeeeeeen

#MIMBA_YA_MADHARA
Ayubu 15:35
Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu,

Naamuru kila mimba ya madhara iliyotungwa kwenye tumbo la kiroho la kishetani ili ikuzalie madhara, mikosi, balaa, umaskini, fedheha nk.

Kwa jina la Yesu Kristo ninaiharibu mimba hiyo kabla haijafikia wakati wa Kuzaa, naikata milija yake kwa jina la Yesu #Sema_Ameeeeeeen

#NJIA_YA_UZIMA

Yeremia 21:8
Nawe waambie watu hawa, BWANA asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.

Na kuombea kwa jina kuu la Yesu Kristo, kuanzia mwezi huu wa 7 mpaka wa 12 miguu yako ipitishwe katika njia ya uzima. Mauti isionekane kwako, unaye mwamini Mungu kuwa atakuvusha salama Type #Ameeeeeen

#AKILI_ZA_MOYONI
kuna mambo mengine huwa yanapatikana kwa neema ya Mungu tu, Tunasoma ili kuongeza au kupata ujuzi ufahamu na maarifa.

Hapa Mungu anawajaza watu akili za moyoni Ili watumike katika kila aina ya kazi.(genius)
👇👇👇👇👇👇
Kutoka 35:35
Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.

#Pokea_akili_ya_ziada_isiyo_kawaida. Pasiwepo na jambo lakushindikana mbele yako katika jina la Yesu.
#Type_Ameeeen

Watu waoga huwa hawana maono watu wenye maono ni watu majasiri. Maono hutengeneza ujasiri ndani ya mtu

#Bwana_Yesu_Asifiwe_milele!!
Namtukuza Mungu kwa kukuamsha salama mtu wa Mungu.
Leo tumeanza kongamano la siku 3 la maombi ya kustawisha uchumi.

Mzigo wa ujumbe huu, Mungu ameuweka ndani yangu kwa sababu Wakristo wengi ni watu wanaoishi maisha yale yale miaka yote, na hata sasa ni mwezi wa sifa lakini ukitafakari maisha utaona hakuna maongezeko yoyote zaidi ya mapito mapito tu na changamoto mbali mbali. Ukweli ni kwamba adui amefanya vita vikali sana na uchumi wa Wakristo ndio maana kustawi kwao ni changamoto sana na ndiyo maana wanajikuta wanaishi maisha yale yale miaka yote.

Katika hili napambana sana kuvusha watu eneo hilo kupitia uwezo wa damu ya Yesu. Amen

Ungana pamoja nasi katika siku hizi 3 za Maombi kwa ajili ya kuchipuza uchumi

Ayubu 14:7
Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,
Wala machipukizi yake hayatakoma.

Nitasema na uchumi wa kila mtu uliokwatwa,na uliokatika, kwamba yako matumaini katika Bwana, utachipuka tena kwa jina la Yesu.
Nasema na uchumi wa mtu akue tena kwa jina la Yesu, uchipue tena kwa jina la Yesu, usitawi tena kwa jina la Yesu.

Neema hii na iwe kwako katika majira haya mbingu zifungue malango yako tena kwa jina la Yesu.

#MAJIRA_YA_ADUI_KUJA_KUPANDA_MAGUGU
👇👇👇👇👇
Mathayo 13:24
Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda #mbegu njema katika konde lake;
lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda #magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

Adui yako ni mtu mwenye akili na ufahamu na maono ya kiroho, ni mtu ambaye anayajua majira yako ya kujiliwa na mema kuliko unavyodhani. Ndio maana huyu mpanzi alipomaliza kupanda mbegu zake njema katika shamba lake, alipoondoka, adui yake akaenda majira ya usiku kwenye shamba lile, akapanda magugu.

#Kwanini_adui_alipanda_magugu?
Alipanda magugu ili kuharibu mazao yale katika majira ya kumea na majira ya kuvuna, ili aliyepanda avune asichotarajia. ili kudhohofisha mmea katika hatua zake za ukuwaji, ili mkulima asipate anachostahili.

Kama adui alienda usiku kupanga magugu, jiulize, ile mtu anayekutokea mara kwa mara kwenye ndoto usiku, huwa anakuja kupandanini kwako? Na kusudi lake ni nini juu ya hayo anayofanya usiku wakati umelala?
Alipoona nyakati zako za kufanikiwa zimekaribia, akaja usiku akapanda magonjwa kwenye mwili wako au watoto wako ili kukurudisha nyuma. Unashangaa ghafla mtoto anaumwa serious, ghafla unaanza kuzunguka mahospitarini nk.

#FAHAMU_HILI
adui anaweza kupanda magugu ndani ya tumbo la mama mjamzito, ili katika majira ya mtoto kuzaliwa, mimba iharibike, alienda kupanda saa ngapi, Mimi mwenyewe sijui, isipokuwa nataka ujue kwamba katika majira yako mema, adui anauwezo wa kuja na kupanda magugu.
Neema ya Yesu na iwe kwako katika kuyafahamu haya. Amina na Amina.
#By_Mwl_Boniface_Mwamafupa
0769220278

AIC BUJORA MWANZA

#IBILISI_HUONEA_WATU
Mwl Boniface Mwamafupa
Matendo10:38
Na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

kuonea watu ni kazi ambayo Ibilisi aliianza tangu Karen na karne.
Wengine amewaonea kwa kuwafunga wasizae, wengine kwa kuwafunga wasione, wengine wasiolewe, wengine kuharibu mimba, wengine kwa umaskini, wengine kwenye madawa ya kulevya, wengine kwenye magonjwa, wengine kwenye ajari, wengine kwenye majanga mbali mbali, wengine kwenye mikosi nk.

Kuwaponya watu walioonewa na Ibilisi ni shuguli moja wapo ambayo Yesu aliifanya kwa sehemu kubwa alipokuwa duniani na kuwaagiza Watumishi wake wote kufanya shuguli hiyo kila waendako.

#NASEMA
natuma neema ya Mungu na nguvu zake ndani yako, na usionewe na Ibilisi siku zote za maisha yake.
Kwa jina la Yesu Pokea
#Type_Amen_Kubwaaaaa

Bwana Yesu Asifiwe, heri ya kuamka salama.
Nakuombea neema kuu kutoka kwa Mungu ikuongoze katika njia ya mema na haki katika kazi za mikono yako,
#Mungu_anapoinua_wengine_akukumbuke_na_wewe_na_familia_yako_Amen
Isaya 49:15
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
#Amen_Mungu_anakupenda_sana
YouTube channel yetu
https://youtu.be/XIdSMweCAF0

#UJUMBE_WA_SIKU
Hatuwezi kumshinda Shetani ikiwa hatujaamua kujiweke chini ya Mungu.

Yakobo 4:7
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Hatuwezi kumpinga Shetani ikiwa hatujaamua kujiweke chini ya Mungu.
Ili tuwe na mamlaka juu ya Shetani, lazima tuwe chini ya Mungu.
Tusipokuwa chini ya Mungu Hatuwezi kuwa na mamlaka mbele ya Shetani.

Je, katika hili umejifunza nini?
Naomba comment yako juu ya ulichojifunza katika jumbe huu. Amen
Neema na iwe kwenu ninyi nyote.

[02/26/19]   #MLANGO_WA_DHAMBI.
Mwl Boniface Mwamafupa

Ufunuo wa Yohana 18:2
Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

Inawezekana mtu akawa makao ya mashetani na ngome ya kila roho za kuzimu nk.

Nini kinamfanya mtu awe makao ya mashetani?

Ni uovu. Mtu mwovu hukaribisha roho zinazitawala mambo maovu ziishi ndani yake na zimtumie vile ziwezavyo.
Dhambi ndiyo hufungua mlango wa roho chafu kuingia ndani ya mtu.

Utakatifu, kuchukia dhambi ndiko kinamfanya roho wa Mungu kuishi ndani ya mtu.

Ukiona mtu anamashetani fahamu kuwa yalipata mlango wa kumwingia kupitia dhambi iliyotendwa.

WENGINE HUNIULIZA.
Mbona mimi naombewa lakini sifunguliwi?

#Nawajibu.
Lango la dhambi bado liko wasi, yale maroho yakikutazama bado yanaona kuna fursa bado ya kuendelea kukaa ndani yako, ndiyo maana yanarudi.

Siunataka ufunguliwe ukaendelee na mambo yako. Kwani unataka ufunguliwe ili uishi na Kristo?

Tatizo nambali wani ndio hilo kwa watu ambazo wanaombewa kila siku na mashetani yanawarudia.

Neema na iwe kwenu na imani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Kristo Bwana wetu. Amina.

#MAISHA_YALEYALE_UCHUMI_ULEULE.
By.
Mwl Boniface Mwamafupa

Kuna watu huwa wanaishi maisha yaleyale yaani hayabadiriki miaka nenda miaka rudi.
Kuna wapo huwa wanauchumi uleule miaka nenda miaka rudi.
BAADHI YA WATU HUWA WANAJUA KUWA HII NI HALI YA KAWAIDA TU.

#HAPANA.
Hii siyo hali ya kawada katika maisha ya mwanadamu. Maisha ya mwanadamu ni maisha ya makuzi, nikisema makuzi nazungumzia kukua au kuongezea. Maisha ya mwanadamu hayakufanywa yawe yaleyale bali yalifanywa yawe ya mabadiriko.

Ndio maana hakuna mwanadamu anabaki kuwa na mwaka mmoja mtu baada ya kuzaliwa, ndio maana hakuna mwanadamu asiyeuongezeka umari na umbo lake baada ya kuzaliwa.

Ukizaa mtoto, alafu imefikia miaka wili akawa na umbo lilelile la kitoto kichanga unaweza kumtupa huyo mtoto ukifikiri yamkini siyo mwanadamu, au unaweza kuona siyo jambo la kawaida na kutambua kuwa lazima kunatatizo juu ya mtoto huyo.
Kwanini hayo yote? Kwa sababu mwanadamu lazima awe na makuzi kila baada ya muda husika kimaumbile.

Ikiwa kimaumbile unaweza kuona ni tatizo kwa kuto kuona makuzi kwa mwanadamu, kwa nini katika hali ya uchumi na maendelea uone ni kawaida tu mtu kuto kuwa na makuzi?

Yaani unaweza kuachana na mtu miaka mitano au sita au kumi, ukija kukutana naye unamkuta ana hali ile ile kimawazo kifikira na hana maendeleo yoyote.
Kama ulimwacha na baiskeli unamkuta na baiskeli ile ile, kama ulimwacha anatembea kwa miguu unamkuta na hali ile ile hakuna mataendeleo yoyote
Kama ulimwacha anabangiza bangaiza tu unamkuta anabangaiza vile vile.

#WATU_WA_MUNGU_HILI_NI_TATIZO
Mwanadamu aliumbwa aendelee, na kama haendelei lazima kuna kifungo flani kafungwa huyu.
Either fikira zake zimezuiliwa kabida na nguvu flani ili asisonge mbele.
Na kama kuna mtu amemfunga, maana take mtu huyo kuna namna ana masrahi yake kupitia kifungo hicho.

Unaweza kukuta mtu una muwazisha jambo la maendeleo yake mwenyewe lakini unaona ni mzito sana kulipokea, na hata kama akilipokea halifanyii kazi.

#FIKRA_HUTIWA_UZITO
2 Wakorintho 3:14
ila fikira zao zilitiwa uzito.

Fikira za mtu zikitiwa uzito mtu huyo hawezi kufikiri maendeleo, hawezi kufikiri kustawisha uchumi wake, hawezi kufikiri kusonga mbele kimaisha. Kwa sababu mambo haya lazima yafanyiwe Nazi ndani ya mawazo na fikira kwanza ndipo yaje nje.

#FIKRA_HUPOFUSHWA
2 Wakorintho 4:4
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru.

Fikira hupofushwa, ikipofushwa fikira za mtu, mtu huyo anakuwa gizani, ndio maana Biblia inasema, amewapofusha fikira isiwazukie nuru. Maana yake ndani yao hawako nuruni wako gizani.
Sasa fikira za mtu kama ziko gizani, kama zimepofushwa, maendeleo anayapata wapi mtu huyu?

#KIFIRA_HUTEKWA
2 Wakorintho 10:5
Tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

Fikira inaweza ikatekwa nyara kusudi zitii mtu flani ndio maana hapa unaoba biblia inasema tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo. Kwa sababu fikira za watu zimetekwa nyara ili watu wamtii Ibilisi, sasa ili zipate kumtii Kristo lazima zitekwe nyara pia na kuzirudisha katika hali ya kumwofu Mungu.

Kwa hiyo ukiona mtu miaka yote inakuwa ya mateso kwake, fahamu kuwa lazima anakifungo.
Na inawezekana ni mtumishi wa mtu rohoni. Ndiyo maana hasongi mbele kabisa.
Siku zote mtumwa kazi yake ni kutumukia tu. Mtu hawi huru kufanya mambo yake. Ndio maana hana maendeleo.

#WATU_WA_MUNGU.
Kufanya huduma za kufungua watu ni muhimu sana katika ibada zetu. Maisha ya watu hayasogei kwa sababu ya vifungo mbali mbali wanavyokutana navyo kwenye jamii za watu wanaoishi nao.
AAdilimia kubwa dunia inaongozwa na roho za kishirikiana katika bihashara za watu na ofisi zao.

Mshirikina hutumia watu ili afanikiwe yeye, ustawi wa maisha ya mshirikina unategemea roho za watu, viungo vya watu nk.

Ingawa siyo kila mtu ambaye hana maendeleo amelogwa. Achache sana ni mzembe wao na kujidharau.
Lakini wengi wao ni vifungo vya na mazuio ya kiroho.
Funguo, mawazo yako, fungua fikira zako, fungua mikono yako, fungua karama yako iliyofungqa na maneno ya watu na hila zao. Fungua milango yako ya neema na kibali, fungua bihashara yako, fungua ofisi yako, fungua imani yako, fungua jina lako kwa damu ya Yesu.

Neema na iwe kwenu kwa damu ya Mwokozi. Amina na amina.

#INJILI_ZINGINE_JAMANI!

Eti wanaoabudu jumapili wanamwabudu mungu jua, eti kwa sababu jumapili ilikuwa siku ya kuabudu jua kwa hiyo ikaitwa sun day.
Wakaendelea mbele tena jumatatu pia kuna mungu aliabudiwa, jumanne pia kuna mungu aliabudiwa, jumatano, alhamisi na ijumaa.
Haya ni mafundisho na mafunuo ya mpinga Kristo 100%.

Hakuna siku iliyoumbwa na shetani wala mungu mwingine isipokuwa Mungu wa mbingu na nchi.
Siku zote niza Mungu hakuna siku ya shetani.
Hata kama kuna watu waliabudu jua siku ya jumapili, haimaanishi kila anayeabudu jumapili anaabudu huyo mungu jua.
Ina maana Wakristo kwenye ibada ijumaa ni waislamu, kisa tu wanaibada siku ya ijumaa?

#SIKILIZA_NDUGU
Mashetani yanaweza kuabudiwa siku yoyote ile hata jumamosi kama anayeyaabudu atapenda kuyaabudu siku hiyo.
Hakuna siku ya Shetani wala shetani hakuumba siku.
Siku zote ni za Mungu alizifanya kwa kusudi lake.
Mungu anaweza kuabudiwa siku yoyote ile.
Biblia inatupa Uhuru wa kuabudu.
#SOMA_HAPA ujue Mungu anaabudiwa wapi.
Yohana 4:23-26
[23]Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
[24]Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
[25]Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
[26]Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.

Alikua akisubiriwa Masihi ambaye ni Kristo ili aje kuweka sawa mambo ya ibada ndio maana huyu mwanamke alimuuliza Yesu kwa sababu nyakati hizo pia kulikuwa na ubishani mkubwa wa ibada na ndiyo maana Yesu akajibu kwamba waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli.

#JE_UNAIJUA_HII?
Wagalatia 5:18
Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

Wagalatia 3:23-27
[23]Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.
[24]Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.
[25]Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.
[26]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
[27]Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

#NDUGU_ZANGU.
Agano jipya ni agano lenye tamani kubwa sana Nyakati hizi. Ndiko tunapata neema ya ajabu sana kwa Mungu. Ndilo linaotufanya tuitwe wana wa Mungu.
Ukitaka kuwa wa thamani mbele za Mungu lazima utoke kwenye agano LA sheria, na kuingia kwenye agano la neema.

Neema na iwe kwenu na imani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Kristo Bwana wetu. Amina na amina

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address

Other Religious Organizations in Dodoma (show all)
Saint Gemma Sisters of Dodoma. Saint Gemma Sisters of Dodoma.
Dodoma Cathedral Church(Catholic)
Dodoma, DODOMA

St.Gemma Sisters Congregation is a Diocesan Institution that was founded in Kondoa Irangi, Dodoma Region on the 14th September 1947 by the late Monsigno

Kizota Gospel Church Kizota Gospel Church
Dodoma
Dodoma

Ni kanisa la kipentekoste lililopo manispaa ya Dodoma mjini! Ili kufika panda gari zinazoelekea nkuhungu kisha shuka kituo cha daraja la kwanza utaona kiba

ICC Dodoma ICC Dodoma
Dodoma

We preach the Gospel of Jesus Christ by fulfilling the purpose of Church which is evangelism, fellowship, worship, spiritual maturity and ministry.

JCC Nkuhungu Dodoma JCC Nkuhungu Dodoma
Nkuhungu
Dodoma, +225

Ni kanisa la kiroho lililopo DODOMA maeneo ya nkuhungu stand karibuni nyote

TAFES UDOM_University Of Dodoma TAFES UDOM_University Of Dodoma
UDOM
Dodoma, 0105

TAFES NI FELLOWSHIP YA KIKRISTO ISIYOFUNGAMANA NA DHEHEBU LOLOTE, TUNAPATIKANA COLLEGE ZOTE HAPA UDOM, KARIBU UABUDU NASI +255755566334 Call/Sms/whatsapp

Prophet Linus Ministries Prophet Linus Ministries
Dodoma

Prophet Linus Tesha Is The founder of MRD Prophetic Church Worldwide. Find the Prophet Through wasp+255713344025

Makedonia Gospel Centre-Kisasa,dodoma Makedonia Gospel Centre-Kisasa,dodoma
Kisasa
Dodoma, 542

Kanisa letu zuri linapatikana eneo la Kisasa C centre mkabala na shule ya sekondari ya Kisasa:

TAFES CBE Dodoma TAFES CBE Dodoma
[email protected]
Dodoma, 2077 DODOMA

TAFES-CBE DODOMA Is an interdenominational movement reaching every student in the campus with the gospel of Jesus Christ.

Safina Anglican Choir - SAC Safina Anglican Choir - SAC
Dodoma, +255

A religious and community-based group called SAFINA GROUP (SAG), was established in the Anglican Cathedral of the Holy Spirit in 11th February, 1996.

Dodoma Christian Fellowship Church Dodoma Christian Fellowship Church
Dodoma
Dodoma

Dodoma Christian Fellowship Church is a Pentecost Church lead by Rev. Past INNOCENT MBYALLU based at Dodoma /Tanzania

TUCASA-IRDP Dodoma. TUCASA-IRDP Dodoma.
138
Dodoma, 41113

special for TUCASA Members at Mipango Institute,sharing ideas on spiritual perspective as well as memory events' photos,also getting informations and chat.

Christian Council of Tanzania (CCT) Christian Council of Tanzania (CCT)
P.O.Box 1454,
Dodoma

The Christian Council of Tanzania (CCT) was established in January 1934 as a fellowship of Churches and Christians. It was then named the Tanganyika Missionary Council until 1964 when it adopted its current name. The CCT has 12 National Churches