Doctrine of the Apostolic Faith - Arusha Tanzania

Doctrine of the Apostolic Faith - Arusha Tanzania

GOD IS ONE

[05/25/19]   Mungu awabariki wrote mchana wa leo ukawe wabaraka

Max Shimba Ministries

MKUTANO WA INJILI PAKISTAN

MAELFU KWA MAELFU WAINGIA UKRISTO NA KUBATIZWA

WAMEKIRI KUWA YESU NI MUNGU MKUU.

UISLAM BAI BAI NA UNAPUPUTIKA.

Doctrine of the Apostolic Faith - Arusha Tanzania's cover photo

Doctrine of the Apostolic Faith - Arusha Tanzania's cover photo

swahilitimes.com

Tamko la Marekani juu ya kushambuliwa kwa Tundu Lissu

swahilitimes.com Marekeani imeeleza kuwa imesikitishwa na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa anaelekea nyumbani kwake Dodoma eneo la Area D akitokea bungeni majira ya saa 7 mchana.

Max Shimba Ministries

JE UNAIJUA HOJA KUBWA NA PEKEE YA WASABATO “SDA” KUHUSU KUSHIKA SABATO?
SEHEMU YA KWANZA

Iko hoja kwamba Sabato ni amri ya muhimu sana kwa sababu ilitoka moja kwa moja kinywani mwa Mungu tofauti na amri zingine ambazo zililetwa kupitia manabii au mitume.

Katika Agano la Kale Mungu alisema, “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase…Kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.” (Kutoka 20:8,11)

Hoja hii haina uzito kwa sababu kuu mbili:
Biblia kwa ujumla wake ni Neno la Mungu ambalo limetoka kinywani mwake lote. Na maandiko yako wazi kwamba: Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa, apate kutenda kila tendo jema. (2 Tim. 3:16-17).

Na kimsingi maandiko haya, ukisoma kwenye Biblia ya Kiingereza, hayasemi “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu”. Badala yake yanasema: All Scripture is God-breathed (NIV); au All scripture is given by inspiration of God (KJV). Hii ina maana kwamba: Maandiko yote yametokana na pumzi ya Mungu.

Kwa hiyo, hakuna mantiki kusema kwamba andiko hili lina maana zaidi kuliko lile kwa kuwa hili alitamka Mungu mwenyewe. Yote yana nguvu ileile; yote yametoka kwa Mungu yuleyule.

HOJA ZINAZOTUMIWA NA WASABATO KUISHIKILIA SABATO YA MWILINI

1. WANASEMA MUNGU SI KIGEUGEU
Yaani Mungu hawezi kusema alafu akaghairi (Malaki3:6) (Zaburi89:34) (Yakobo1:17)

Ni muhimu kujua Biblia inaposema Mungu hana kigeugeu lazima tujue hana kigeugeu anamaanisha nini?

Mungu hana kigeugeu au habadiliki katika ahadi, yaani Mungu akikuhaidi atakubariki na ukakaa katika njia zake, kubarikiwa ni lazima na hata hivyo akikuhadi kukubariki halafu ukaenda kinyume na mapenzi yake hugeuka na kutokutimiza aliyoyaahidi kwako (1Samweli 2:30).

Tukiyachunguza maandiko yote yanayoelezea kuwa Mungu si kigeugeu utaona chanzo cha maandiko haya ni ahadi (Malaki 3:5-6) Mungu anasema “Nita” maana yake anaahidi mambo kadhaa katika mstari wa 5, na katika mstari wa 6 anaeleza kuwa yeye si kigeugeu katika yale aliyoyaahidi katika mstari wa 5.

USIKOSE SEHEMU YA PILI

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

Max Shimba Ministries

KWANINI ALLAH ANAOMBA MSAADA KWA MAKAFIRI?

Sura Al-Ankabut 29:6

Quran inasema:
Allah hahitaji kusaidiwa na viumbe wake. (bila shaka ni katika kutekeleza makusudi na mipango yake).

LAKINI QURAN HIYO HIYO INAWAAMBIA WAISLAMU:

Sura Muhammad 47:7
Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia na kuwafanya kuwa imara.

Maswali:

1. Umesema huhitaji msaada, kisha unasema tena unahitaji msaada! Je, Mungu anaweza kufanya jambo kama hilo?
2. Aya hizi zinafanana au zinapingana?
3. Je, hii si ishara kuwa aya hizi zilisemwa tu ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani, lakini msemaji alipoona anahitaji kuwafanya watu watende kinyume chake, akajikuta amesema tofauti na alivyosema siku za nyuma?

Na tena quran inasema katika sura Al-Baqara 2:244

Fanyeni vita kwa ajili ya Allah na mkumbuke kwamba anaona yote na anajua yote.

Maswali:

1. Kama kweli Allah hahitaji msaada wa viumbe wake; na kama kweli aliumba ulimwengu wote kwa NENO TU, iweje NENO hilo hilo lisiweze kuwabadilisha wanadamu hadi alazimike kuliingiza ndani yao kwa nguvu, kwa vitisho na kwa ukali namna hiyo?

(Ukristo unashinda na kufanikiwa kwa NENO tu. Maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wetu. Yeye aliumba kwa Neno; na sisi watoto wake, tunaumba kwa Neno hilo hilo. Tunahubiri tu na watu wanaokolewa, wanaponywa, wanalindwa na kusimama na Mungu wa kweli. Huoni kwamba hii hasa ndiyo maana ya nguvu ya Mungu? Hatuhitaji kuchinja au kupiga watu ili wampende Mungu!! Unawezaje, hata tu wewe mwenyewe, kumfanya mwanao au mkeo akupende kwa njia ya vipigo na kulazimisha? yaani, ukitaka mwanao au mkeo akupende utamshikia rungu au panga au bunduki? Je, hiyo si ishara kwamba wewe huna nguvu ndiyo maana unalazimisha? je, huko si kujikanganya maana umetuambia kuwa wewe ni Mungu unayeweza yote?)

2. Je, Allah anapotaka wanadamu wanaomwamini wafanye vita ili kuwalazimisha wasioamini wamwamini, huko si kutaka msaada kwa viumbe wake?

Ndio maana watu wenye kujitambua wanaukimbia Uislam.

Shalom

Max Shimba Ministries

Journalist Sylvester james

Bwana Yesu asifiwe
Unaendeleaje
KUOTA NDOTO YA NYOKA.

Nipe nafasi tena moyoni mwako nikufundishe juu ya “Mwongozo wa kibiblia wa namna ya kutafsiri na kuombea NDOTO zenye NYOKA ndani yake”

Je, unayaelewa maneno aliyoyasema Yusufu akizungumza na mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, juu ya kutafsiri ndoto?

Yusufu aliwaambia hivi: “Kutafsiri ndoto si kazi ya Mungu? Tafadhali mniambie” (Mwanzo 40:8). Yusufu alitaka wajue ya kuwa – ingawa atawatafsiria ndoto zao, lakini tafsiri hiyo itatoka kwa Mungu.

Kufuatana na kitabu cha Ayubu 33:14,15, ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu anaitumia kusema na watu. Na kwa msingi huu ina maana – lazima neno la Mungu (Biblia) lihusike (Warumi 10:17); katika kutafsiri ndoto, likishirikiana na Roho Mtakatifu (Yohana 16:13-15).

Hii ina maana ya kwamba Mungu anapokupa tafsiri ya ndoto, Roho Mtakatifu atakuelekeza kwenye mstari husika wa biblia, ili uweze kupata si tu tafsiri ya ndoto, bali pia upate na ujumbe uliomo ndani yake.

Ndoto ambazo mtu anaota zikiwa na “nyoka” ndani yake – zina maana gani, na zina ujumbe gani?
Mfano wa 1: Ukiota umeumwa na nyoka maana yake ni nini?

Biblia inasema: “…..na yeye abomoaye boma, nyoka atamuuma” (Mhubiri 10:8).

Kwa hiyo ukiota ndoto unaumwa na nyoka, ina maana kuna jambo ulilolifanya lililosababisha “boma” (au “ulinzi” wa Mungu kwako) libomoke, na kutoa nafasi kwa nyoka kukuuma.

Lakini katika Hesabu 21:6 tunasoma ya kuwa: “Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakauma, watu wengi wakafa”
Kwa hiyo – ikiwa umeumwa na nyoka kwenye ndoto, ujue pia ya kwamba kuna “sumu” iliyoingizwa ndani yako, kwa lengo la “kuua” kile kinachoendana na “eneo” alilokuuma!

Pamoja na kuingiziwa sumu ya nyoka unapoumwa na nyoka kwenye ndoto, lakini unaingiziwa pia “laana” kwenye “eneo” uliloumwa! Hii ni kwa sababu kufuatana na kitabu cha Mwanzo 3:14 – Nyoka “amelaaniwa” na kwa sababu hiyo amebeba laana ndani yake!

Tena, unapoumwa na nyoka kwenye ndoto, ujue unapandikiziwa roho ya “udanganyifu” kwenye “eneo” uliloumwa na huyo nyoka kwenye ndoto (Mwanzo 3:13). Na udanganyifu huo unalenga kwenye “fikra” zako, ili “ukosee” katika maamuzi yako (2 Wakorintho 11:3 na Timotheo 2:14).

Kwa hiyo ukiumwa na nyoka katika ndoto kwenye kisigino au kwenye eneo lolote la kiganja chako cha mguu wako; au nyoka akiingia mwilini mwako na kubaki ndani yako, kwa kupitia kwenye eneo la kiganja cha mguu wako, maana yake nini?

Ndoto kama hiyo ina maana ya kuwa “shetani” anatumia nafasi iliyowazi au mlango ulio wazi kwenye maisha yako, ili kwa kutumia hila na udanganyifu apoteze hatua zako zisifuate mapenzi ya Mungu aliyonayo kwa ajili yako (Zaburi 37:23 na Mithali 16:9); na akunyang’anye “utayari” uliokuwa unakupa kufanikiwa kwenye kitu ambacho Mungu alikuwa anakuongoza ukifanye (Waefeso 6:15); na akunyang’anye mamlaka yako ya Kiroho mahali ulipo au utakapopapitia (Yoshua 1:3 na Luka 10:19)

Tena, ukiota nyoka amekuuma kwenye mkono maana yake shetani amelenga “kuua” au “kuharibu” Baraka za uchumi wako, unaotokana na kazi unazozifanya kwa mikono yako. Hii ni sawa na Kumbukumbu ya Torati 28:6 ; na Kumbukumbu ya Torati 33:11.

Mtu mmoja aliniandikia akisema aliota ndoto ambayo aliona nyoka akimuuma kwenye kidole chake, ambacho alikuwa amevaa pete ya ndoa. Baada ya miezi kadhaa kupita, ndoa yake ilivurugika na kuvunjika.

Naamini hali hiyo ilimpata kwa sababu ya kutokujua “ujumbe” uliokuwemo kwenye ndoto ile; na pia hakujua “uhalisia” wa ndoto aliyoota kwenye maisha yake!
Ni dhahiri ya kuwa alikuwa anapewa ujumbe na Mungu kufuatana na Ayubu 33:14,15 ya kuwa kuna “mlango” wa kiroho uliofunguka, na kusababisha ndoa yake kushambuliwa na roho ya shetani iliyojaa “sumu ya kuua” na iliyojaa udanganyifu!

Tena, ukiota umeumwa nyoka tumboni chini ya kitovu ujue shetani amepanga kuharibu tumbo lako la uzazi, na kuharibu uzao wako, na kuharibu ndoa yako kwenye eneo linalohusiana na kuzaa au kuzalisha.
Mfano wa 2: Ukiota nyoka ameingia mahali au katika eneo – maana yake nini?

Kufuatana na kitabu cha Mwanzo 3:24, ndoto hiyo ina ujumbe wa kumtaarifu mhusika ya kuwa “shetani” amenuia kukutengenezea mazingira ya mtu au watu waliopo kwenye “eneo” hilo, wafukuzwe na waondolewe toka eneo hilo; na wawekewe “zuio” linalowazuia kurudi kwenye “eneo” hilo!

Na pia kufuatana na Kitabu cha 2 Wakorintho 11:3, ndoto hiyo ina ujumbe wa kumtaarifu mhusika ya kuwa, “shetani” amenuia kukutengenezea hila zenye udanganyifu ili aharibu fikra za waliopo kwenye eneo aliloingia, ili makusudi wauache “unyofu na usafi” walionao katika Kristo.

Unapotafuta tafsiri ya ndoto ya namna hii – kwa kufuata hiyo mistari miwili niliyokupa, ni budi pia ujiulize nyoka kaingia chumba gani na yupo eneo gani kwenye chumba hicho.

Kuna mtu aliyeota ndoto ambayo aliona nyoka kaingia dukani kwake na yuko kwenye eneo analouzia vitu. Baada ya siku kadhaa biashara yake ikaharibika na akafunga duka lake.

Mwingine aliniandikia kuwa aliota nyoka kaingia nyumbani kwake kwenye chumba anacholala, na akapanda kwenye kitanda anacholala na mume wake. Halafu akaamka baada ya kuota ndoto hiyo. Baada ya miezi kadhaa kupita, ndoa yake ikaharibika na akafukuzwa na mume wake

Kwa Kufuata utaratibu huu wa Mwanzo 3:24, unaweza kuzielewa ndoto ambazo unaota nyoka kaingia kanisani; au madhabahuni; au jikoni; au shambani; au kwenye gari; nakadhalika
Kumbuka, hata kama nyoka aliyeingia eneo hajauma mtu lakini bado kuwepo kwake hapo ni ishara ya kuwa shetani amenuia kuwafanyia waliopo hapo sawa na Mwanzo 3:24 na 2 Wakorintho 11:3

Ninachotaka ujifunze kwenye mwongozo wa kibiblia juu ya kutafsiri ndoto zenye nyoka ndani yake ni:

1. Tafuta maana na ujumbe wa ndoto hiyo kwa kutafuta na kusoma na kutafakari mistari ya biblia inayohusika na “nyoka” sawa na picha uliyoiona kwenye ndoto;

2. Tizama mstari huo husika kwa uangalifu huku ukiombea – maana mara nyingi huwa inaambatana na namna ya kushughulika na nyoka huyo na madhara yake!
Kwa mfano – ‘nyoka’ anayetokea kwenye ndoto na malengo kama ya ‘nyoka’ wa Ufunuo wa Yohana 12:7-10, - Unamshinda kwa kutumia “damu ya Mwana – Kondoo”, na “kwa neno la ushuhuda” wako (Ufunuo wa Yohana 12:11).

Nimekuombea wewe uliyesoma somo hili leo ili Mungu akupe ushindi dhidi ya roho ya shetani inapojifunua kama nyoka kwenye ndoto.

Mungu akubariki sana.

Max Shimba Ministries

UONGO WA MTUME MUHAMMAD NA QURAN KUHUSU KUPASUKA KWA MWEZI NA KUTEMBEA KWA JUA

1. Mtume Muhammad adai kuwa alipasua Mwezi
2. Hakuna Ushahid wa wapi vilipo vipande hivyo vya Mwezi
3. Muhammad adai kuwa Jua linatembea.

Ndugu wasomaji, leo naanza kwa kusema, hakika Msingi wa Uislam ni uongo na shaka ambazo hazina Ushahid.

Ungana nami moja kwa moja na tuone huo uongo upo wapi katika dini hii ya Jibril ibn Allah.

KUPASUKA KWA MWEZI:
"Hitaji la wapagani kwa Nabii kuwa awaonyeshe miujiza. Nabii aliwaonyesha kupasuka kwa mwezi. ‘Abdullah bin Massud alisimulia: Wakati wa maisha ya Nabii mwezi ulipasuliwa vipande viwili na Nabii alisema kuhusiana na hilo, ‘Shuhudia (jambo hili).’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.830, uk.533.

"Anas alisimulia kwamba watu wa Makka walimwomba Mtume wa Allah awaonyeshe muujiza, na kwa ajili hiyo aliwaonyesha mwezi unaopasuka." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.831, uk.533.

"Ibn ‘Abbas alisimulia: Mwezi ulipasuliwa vipande viwili wakti wa uhai wa Nabii." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.832, uk.534.

Mwezi unaopasuka. Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 225 na.290, uk.273 na rejeo la 1 chini ya uk.273; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 287 na.387-391, uk.365-366; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 261 na.345, 349, uk.331; Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 265 na.368-370, uk.331, 336.

Kuupasua mwezi Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 37 na.6721, 6724-6730, uk.1467-1468.

Sura 54:1 inasema, "Saa (ya hukumu) imekaribia, na mwezi ulipasuliwa vipande viwili. (toleo lililorekebishwa la Yusuf ‘Ali).

Tambua kuwa kupasuliwa vipande viwili kunamaanisha kuwa mwezi uligawanywa nusu kwa nusu, na kitenzi kilichotumika hapa ni cha wakati uliopita. Hatuna kumbukumbu za watu wengine wowote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na jirani zao wa Misri, Syria, au Uajemi ambao waliuona mwezi uliopasuliwa vipande viwili. Kurani na hadithi hazisemi ni jinsi gani mwezi uliweza kurudi kuwa kitu kimoja tena.
Vile vile Imaam Ahmad amerekodi kuwa Jubayr bin Mutw'im alisema: "Mwezi ulipasuka vipande viwili wakati wa Mjumbe wa Allah na sehemu ya mwezi ulikuwa juu ya mlima na sehemu nyingine kwenye mlima mwingine. Wakasema (makafiri) "Muhammad ametufanyia uchawi". Kisha wakasema: "Angeliweza kututeka kwa uchawi asingeliweza kufanya kwa watu wote" [Imaam Ahmad]

Usimulizi wa 'Abdullaah bin 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma):

Ibn 'Abbaas alisema: "Mwezi ulipasuka wakati wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Ibn Jariyr alirekodi kwamba Ibn 'Abbaas alisema kuhusu kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَر))ُ (( وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ))
((Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!))
((Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea)) [Al-Qamar:1-2]

MASWALI:
1. Vipo wapi hivyo vipande viwili vya Mwezi ambao Waislam wanadai Muhammad aliupasua?
2. Upo wapi ushahid wa Kihistoria au Kisayansi ambao unasaidia madai ya kupasuliwa kwa Mwezi na Muhammad?

Hatuna kumbukumbu za watu wengine wowote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na jirani zao wa Misri, Syria, au Uajemi ambao waliuona mwezi uliopasuliwa vipande viwili. Kurani na hadithi hazisemi ni jinsi gani mwezi uliweza kurudi kuwa kitu kimoja tena.

MUHAMMADA ANADAI KUWA JUA LINATEMBEA NA LINASUJUDI KWA KITI CHA ENZI CHA ALLAH

"Abu Dhar alisimulia: Nabii aliniuliza wakati wa machweo ya jua, ‘Unafahamu mahali ambako jua linakwenda (wakati wa kuchwa)?’ Nilijibu, ‘Allah na Mtume wake wanafahamu vizuri zaidi.’ Alisema, ‘Linakwenda (yaani linasafiri) hadi linasujudu chini ya kiti cha enzi, na linapata kibali cha kusimama tena, na linaruhusiwa na kisha (muda utakuja ambapo) litakuwa linakaribia kusujudu lakini kusujudu kwake hakutakubaliwa …’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441 uk.283.

al-Tabari juzuu ya 1 uk.231 inasema, "Nilimuuliza Mjumbe wa Mungu [Muhammad] ‘[Jua] linazama wapi?’ Alinijibu: ‘Linazama mbinguni na kisha linachomoza kutoka mbingu kwenda mbingu nyingine hadi linachomoza kwenye mbingu ya juu zaidi, mbingu ya saba. Hatimaye, linapokuwa chini ya kiti cha enzi, linaanguka chini na kusujudu, na malaika wanaolisimamia wanasujudu pamoja nalo. Kisha jua linasema, Bwana wangu, ni wapi unakoniamuru nichomozee, ni upande ule nilikozamia au nilikochomozea?’ Aliendelea. Jambo hili ndilo (linalokusudiwa na) neno la Mungu: ‘Na jua: Hukimbilia mahali linapotakiwa kuwepo (usiku)’ linaposhikiliwa chini ya kiti cha enzi – ‘Jambo hilo limeamriwa na Yeye Mwenye Nguvu na Mwenye Kujua’ Bwana kwa mamlaka yake ya kifalme, Bwana ambaye ‘anavijua’ viumbe vyake. Aliendelea, Gabriel alileta kwenye jua vazi lenye kung’aa tokana na mwanga utokao kwenye kiti cha enzi, kwa kufuata vipimo vya saa na siku. Ni refu zaidi wakati wa majira ya joto na fupi zaidi wakati wa majira ya baridi, na lenye urefu wa wastani wakati wa majira ya kupukutisha majani na wakati wa majira ya kuchipua majani. [Mitindo ya majira ya kuchipua majani, kupukutisha majani na majira ya baridi!] Aliendelea. Jua huvaa vazi hio, kama mmoja wenu anavyovaa zavi lake. Kisha, huwa huru kuzunguka kwenye anga la mbinguni mpaka linapochomoza kutokea upande linaochomozea. … Njia hiyo hiyo hufuatwa na mwezi wakati wa kuchomoza kwake … Lakini Gabriel huuletea vazi kutoka kwenye mwanga wa miguunil. Hivi ndivyo neno la Mungu (linavyomaanisha) ‘Amelifanya jua kuwa angavu na mwezi kuwa mwanga.’"

HUYU MUHAMMAD wanaye dai kuwa alipasua Mwezi, anaendelea kusema uongo kuwa eti Jua linazunguka na kufika kwa Allah ili kusujudu?

MASWALI:

1. Kama Muhammad alishindwa kujua historia rahisi ya Jua, kwanini tumwanini kuwa alipasua Mwezi?
2. Kama Muhammad anadai kuwa Jua n Mwezi vinatembea, kwanini tumwanini kuwa alipasua Mwezi?

MUHAMMAD ANAENDELEA KUSEMA UONGO NA KUZIDISHA SHAKA KWENYE QURAN
SASA MUHAMMAD ANASEMA KUWA JUA LINAZAMA KWENYE CHEMCHEM YA MATOPE
Dhu al-Qarnaiyn [Zul Qarnain] "alishuhudia kuzama kwa jua kwenye sehemu yake ya kupumzikia kwenye bwawa lenye ute mweusi na wenye harufu mbaya sana." al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174 (Tazama Sura 18:82-97).

al-Tabari juzuu ya 1 uk.234 pia inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi yenye matope. Msemo "yenye matope" ni hami’ah, unaomaanisha udongo mweusi wa mfinyanzi, lakini hamiyah ni neno lenye kufanana nalo linaloweza kumaanisha kitu cha moto. (Tazama rejeo la 442 chini ya uk.234).

Ndugu zanguni, hii dini ni Msiba ambao hauta isha mpaka kihama.

Sasa Muhammad aliye dai kuwa alipasua MWEZI na kushindwa tuonyesha wapi vilipo vipande vya Mwezi alio upasua, anasema kuwa ETI Jua linazama kwenye tope. Huu kama si msiba ni nini?

MUHAMMAD ANAENDELEA KUWEZA SHAKA KATIKA IMANI YAKE:

MUHAMMAD ANASEMA KUWA ETI JUA LINAPOROMOKA TOKA KITI CHA ENZI MPAKA KWENYE BAHARI.

" [Muhammad] Aliendelea. Wakati jua linachomoza, linainuka juu ya kibandawazi (kinachokokotwa na farasi) toka kwenye moja ya chemchemi hizo likiwa pamoja na malaika 360 …. Wakati Mungu anataka kuvijaribu jua na mwezi, ili kuwaonyesha watumishi wake ishara na kwa njia hiyo kuwataka waache kutokumtii Yeye na kuanza kutii, jua huporomoka ghafla toka kwenye kibandawazi na kuanguka kwenye kina cha bahari, ambacho ni cha mduara. Wakati Mungu anataka kuongeza umuhimu wa ishara kuwatisha zaidi watumishi wake, jua lote hunguka, na hapawi na sehemu yake yoyote inayobaki kwenye kibandawazi. Huko ndiko kupatwa kukamilifu kwa jua, wakati ambapo mchana hujiwa na giza na nyota hutokeza." al-Tabari juzuu ya1 uk.236.

JAMANI, hivi hawa ndugu zetu, wanafanya nini Shule? Mbona madai ya Muhammad na Allah wao yamejaa shaka na ni DHAIF DHAIF DHAIF? Hakika Uislam ni uongo na ni didi ya warongo.

MUHAMMAD NA ALLAH SASA WADAI KUWA:

1. NYOTA ni Makombora ya kumpiga Shetani
2. VIMONDO ni silaha za kuwapiga Mashetani

"Mbingu za chini kabisa zina taa [nyota], na ‘Tumeziumba (taa) hizi kama makombora ya kuwafukuzia waovu, na tumetayarisha Adhabu ya Moto Uwakao kwa ajili yao.’" Sura 67:5.

"Kuumbwa kwa nyota hizi kuna madhumuni matatu, yaani, kulipamba anga, makombora ya kuyapiga mashetani,na alama za kuwaongoza wasafiri. Kwa hiyo kama mtu yoyote anajaribu kupata tafsiri nyingine amekosea na anapoteza nguvu zake tu..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 3 kabla na.421, uk.282.

Wakati mwingine vimondo hurushwa kwa mashetani ambao wanajaribu kusikiliza siri za mbinguni. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.902 na rejeo la 674 chini ya uk.243.

Vimondo vinapaswa kuwapiga malaika [wabaya] kabla hawajaeneza mambo walyoyasikia. Wakati mwingine malaika wabaya huwaambia watabiri kabla ya kuwapiga. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.194, uk.110.

Vimondo huyashambulia majini (genies) Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 24 na.5538, uk.1210.

Nyota hulinda dhidi ya shetani. al-Tabari juzuu ya 1, uk.223.

Ndugu wasoamji leo nimeonelea kuwa, ni vyma tuendelee kumuumbua Allah na Muhammad maana wao wamejama shana na uongo kwenye dini yao.

Mungu awabariki sana.

Katika Huduma yake,

Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na mwokozi wetu.

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Aruscha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Aruscha
0