Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania

Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania

Comments

USAILI WA KWENDA KUSOMA ASIA Uongozi wa chuo cha KONERU LAKSHMAIAH EDUCATION FOUNDATION (KL UNIVERSITY) kilichopo katika bara la ASIA nchini INDIA kupitia Kwa muwakilishI wake inchini Tanzania kinatangaza nafasi ya usaili wa kwenda kusoma degree ya kwanza pamoja na masters katika chuo hicho Kwa muhula wa masomo mwaka 2018/2019. KL UNIVERSITY ni chuo Bora na chenye hadhi ya kimataifa (grade A world class) kina mandhari na mazingira Bora na rafiki Kwa wanafunzi wa jinsia zote kujisomea kuanzia madarasa, hostels, cafeteria,maabara, maktaba sehem za ibada kama makanisa na misikiti sehem za mazoezi pamoja na sehem za kupumzka chuo kinatoa kozi zote zenye ushindani katika soko la ajira duniani kama zilivyoainishwa katika vipeperushi. ADA zake ni nafuu (affordable price/ cost) zinazozingatia na uchumi wa inchi husika pia kinaruhusu kulipa ada zake Kwa awamu masomo yataanza August hivyo wahi usaili mapema USAILI UPO WAZI Kama utavutiwa na unahitaji kwenda kusoma huko Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia namba zetu zifuatazo WhatsApp no +919701691947 WhatsApp no 0719008008 Call no 0767805690 Call no 0719008009 ELIMU BORA NI CHANZO CHA MAARIFA HIVYO USIMUCHE ELIMU AENDE ZAKE EWE MZAZI AU MLEZI MLETE MWANAO KL UNIVERSITY KWA ELIMU BORA NA YENYE TIJA NB ukisoma tangazo hili mjulishe na mwenzako ASANTE.
Mungu akupe BARAKA tele pale utakapo kuchangia ununuzi Wa viti katika kanisa letu jipya usharika Wa kkkt mavimba wilayani ulanga kuputia namba 0717 12 87 83 mungu awatangulie wote pia atakuzidishia Mara dufu
barikiwa sana
God is God no one else is like him ,
CHUKUA DAKIKA ZAKO KADHAA TU KUSOMA SOMO HILI NA KUIPITIA PAGE HII #UmojawavijanawaKikristotanzania ILI UPATE MUENDELEZO WA SOMO HILI LAWEZA KUSAIDIA WEWE NA WENGINE WALIO OA AU OLEWA AU WALIO NA MAONO YA KUOA NA KUOLEWA "Barikiwa Sana"
KUHUSU TALAKA NA KUOA/KUOLEWA MARA YA PILI SEHEMU YA KWANZA: TATIZO NI MOYO WA MTU ATOAYE TALAKA! Japokuwa watu wengi wanaamini kwamba talaka nyingi zinatokana na uzinzi/ukosefu wa uaminifu kwenye ndoa lakini Yesu anaonesha tatizo jingine kabla ya hilo. Ukifanya tafiti utagundua kweli wanaume wamekuwa wagumu kuendelea na mke wanapogundua mke si mwaminifu (amekuwa mzinzi) lakini wanawake wamekuwa wavumilivu zaidi wanapogundua mume ameanza mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine. Tukilitazama jambo hili kwa akili za kawaida na kwa haraka tunaweza kuona ni halali kabisa kutoa talaka lakini kabla hatujahalalisha hebu tuone Yesu analizungumziaje jambo hili: MATHAYO 19:8-9 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Kwa nini Yesu alitumia neno ‘uasherati’ au ‘porneia’ kwa kigiriki na sexual immorality kwa kiingereza badala ya neno uzinzi au ‘moichos’ kwa kigiriki na adultery kwa kiingereza? Yesu alikuwa anarejea utamaduni wa Kiyahudi ambao baada ya posa mwanamwali alihesabika kama mke wa kijana aliyemposa. Ukisoma habari za Mariam na Yusufu utaona kwamba malaika anamuonya Yusufu asimwache mke wake Mariam lakini ukweli ni kwamba Yusufu alikuwa bado hajamuoa Mariam. Kwa hiyo malaika anasema Mariam ni Mke wa Yusufu kwa sababu ya posa ambayo imekubaliwa na wazazi na posa hii iliambatana na kiapo ambacho kilifanyika kwa kunywa mvinyo. Baada ya posa binti anawekwa kipindi cha maangalio (kwa sasa tunaweza kusema ni kipindi cha uchumba) kwa muda wa mwaka mmoja na ikiwa atapatikana na tabia za uasherati ndipo mposaji atampa talaka kwa sababu ya uasherati na kisha mwanamke atapewa adhabu ya kupigwa mawe hadi kifo. Kwa hiyo kwa utamaduni wa kiyahudi wachumba ni sawa na mke na mume wasioishi pamoja. Mafarisayo walimwuliza Yesu kama hakuna sababu yoyote inayoweza kuwapa kibali cha kutoa talaka lakini Yesu akawarejesha kwenye mpango wa Mungu tangu Mwanzo kwamba ni watu wawili wanakuwa mwili mmoja kwa hiyo aliowaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe. Baada ya kuona jibu hili ni zito wakaamua kumtumia Musa kwamba aliwaruhusu kuandika hati ya talaka lakini Yesu akawaambia ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao kitu ambacho kinaonesha kwamba hata Musa hakupenda kufanya hivyo kwa sababu alifahamu kwamba talaka si mpango wa Mungu. Kwa hiyo kwa wachumba wanaweza kupeana talaka lakini wanandoa wanatakiwa kuangalia msingi wa neno la Mungu kwamba wamekuwa mwili mmoja. Fuatilia somo nililofafanua maana ya kuwa mwili mmoja. Kumbe sababu zetu zote zinazotupa ujasiri au uhalali wa kuandika hati ya talaka zinatokana na mioyo yetu kuwa migumu. Kama mioyo yetu ikiwa laini hatuwezi kuipenda talaka, hatuwezi kuwaza talaka, hatuwezi kuiweka talaka kama suluhu ya matatizo ya ndoa. Moyo mgumu bila shaka ni moyo wa kujihesabia haki, moyo wa kutosamehe, moyo wa kuhukumu wengine, na moyo unaotazama sheria badala ya neema ya Mungu. Sasa ni kazi kwako mpendwa wangu unataka kuongozwa na Roho Mtakatifu ili uzae matunda ya roho (upole, uvumilivu, msamaha, utu wema, fadhili, kiasi, nk,) au unataka kuendelea kuwa na moyo mgumu ili uendelee kuifuata sheria ya Musa ambayo katika hiyo hakuna wokovu? BY MUSSA KISOMA 0753469525 Facebook: FURAHIA MAHUSIANO Unaweza kupata masomo haya na mengine mengi kwenye application ya simu yako. Nenda playstore andika Furahia Mahusiano .
Kama ni nguvu zangu Mimi singefika mahali nimefika lakini yesu ni Ebenezer ndipo nasema ameniwezesha....kama milima Mimi nimepanda miteremko nimeteremka ndipo nasema ameniwezesha

Lengo ni kumtumikia Mungu bila kujari madhebu yetu kama Vijana. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu. Zaburi 60:12

Umoja Wa Vijana wa kikristo Tanzania ulianzishwa mwaka 2009 mwezi septemba tarehe 17 kwa Lengo la kuunganisha vijana wa wote kikristo TANZANIA kwa hiyari yao ili tuweze kumtumikia MUNGU katika hali zote bila kujari udhehebu wetu. Shabaha ikiwa kuhubiri habari ya ufalme wa MUNGU katika kila eneo la TANZANIA kwa njia ya Uimbaji,uinjilisti,uwalimu,unabii,uchungaji na utume ikiwa ni kwa kuandaa mikutano ya injili,semina za ndani na nje,makongamano ya kusifu,kuabudu na maombi. Pia kama vijana wa Kikristo tunapenda kutembeleana, kushauriana,kufundishana,kusaidiana,kubadilishana mawazo,ujuzi na ufahamu kuhusu maisha yetu ili tupate kufanikiwa kiroho na mwili. Kusaidiana katika changamoto za ujana hasa katika Uchumi,Mahusiano,Ndoa,Huduma,Elimu,jamii na Shughuli zinazo gusa maisha yetu ya kila siku na jamii inayo tuzunguka. NI HAJA YETU KUONA VIJANA TUNAMTUKUZA MUNGU KWA KILA JAMBO NA KITU AMBACHO MUNGU AMETUPATIA.

Mission: Kuhubiri habari ya ufalme wa MUNGU katika kila eneo la TANZANIA kwa njia ya Uimbaji,uinjilisti,uwalimu,unabii,uchungaji na utume ikiwa ni kwa kuandaa mikutano ya injili,semina za ndani na nje,makongamano ya kusifu,kuabudu na maombi. Kukaa na kujifunza na vijana, kumilki miradi ili kutoa fursa za ajira kwa vijana bila kujari dini.Kiutembelea wahitaji mbalili na ili kuwavuta kwa Yesu.

Operating as usual

[07/06/20]   MAAMUZI SAHIHI ILI KUFIKIA MALENGO AU MAONO YAKO. * Mithali 29:18
SEHEMU YA KWANZA (UTANGULIZI)

Maisha ya kila mwanadamu huongozwa na malengo au Maono.. bila kujali umri, jinsia, elimu, dini na uwezo wa kiuchumi.

Wapo ambao wanaweka malengo ili kuyatimiza na pia wapo ambao huwekewa malengo ili wayatimze na pia wapo ambao huwekewa na kuweka malengo ili wayatimize. Napia wapo ambao huiga malengo ya wengine ili wayatimize pia wapo wasio na malengo ila hufuata mkumbo wa wenye malengo na hukosa msimamo wa maamuzi ili kutimiza malengo yao.

Malengo ndiyo yanayo tutofautisha katika mifumo ya fikra, aina ya maisha na chaguo la vipaumbele katika maisha, na namna ya kuishi,

Malengo hayo ndiyo hutupa imani ya kuamini Jambo na kuachagua Mungu wa kumtumikia au Jambo la kuliwekea imani.Pia malengo haya ndiyo yatupayo aina ya jamii ya kuamabatana nayo.

JE UNAYO MALENGO, UNAAMINI NINI KITAKUSAIDIA KUTIMIZA MALENGO YAKO, TUKUTANE WAKATI MWINGINE... Shalom

Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania's cover photo

[07/03/20]   SHALOM
WE ARE BACK IN SERVICE, NI HAJA YETU KUKUTUMIKIA KATIKA BWANA WETU YESU KRISTO

[04/15/19]   Shalom Naomba kusshiriki Jambo nawewe na ikiwa unafahamu zaidi huhusu jambo hili tafadhali usisite kutueleza.

Unapokuwa na amani katika kutenda jambo au kitu fulani ambayo ni chema na umemshirikisha Mungu, bila kujali ugumu au changamoto unazokutana nazo katika kutimiza au kufikia malengo yako.
Fahamu jambo hili MUNGU HUFUNGUA MALANGO WA KUFANIKISHA JAMBO HILO.
* Yohana Mt: 14:27
- Amani huondoa shaka moyoni * 1 theasalonike 5:3
- Amani huleya uhuru katika kutenda jambo
- Amani hukuonyesha wema wa jambo *
- Amani hukupa kukamilisha jambo bila kuogopa changamoto
- Amani hukupa wasaidizi na watenda kazi pamoja nawewe
- Amani husaulisha maimivu ya moyo.* Galatia 5:22
- Amani hufungua macho kuona fulsa.
- Amani huleta furaha ya Moyo(Nafsi)
- Amani huleta maamuzi sahihi * kolosai 3:15
- Mungu nakuwazia amani
- N.K

FAHAMU ILI UFANIKIWE UNAHITAJI AMANI KATIKA YALE UYAFANYAYO.
* Ayubu 22:21
- Kuwa na amani na huduma yako
- Kuwa na amani na kazi za mikono yako
- kuwa na amani na familia yako ili ifasnikiwe
- kuwa na Amani na muonekano wako ili ujipende
- Kuwa na amani na maono yako yatatimia
- Kuwa na amani ili Mungu akae nawe
- Kuwa na Amani hata unaposhindwa kutimiza lengo ili uone mlango wa kutimiza
- N.K

NB: Mungu akupe kutafuta zaidi ya hapa
*FAHAMU ILI UISHI NA KUFANIKIWA KATIKA JAMBO AU MAMBO UNAHITAJI KUFANYA AMANI NAYO. * Ebrania 12:14

Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania's cover photo

Uwezo wako wa kutenda jambo kwa usahihi huanzia katika roho yako. Hisia za ndani moyo zenye msukumo chanya sizizo danganya zilizo beba ujasiri na uhalisia wako, hizo ndio za kuzifuata katika maamuzi na sio akili yako inaona nini au taka nini. Acha roho yako iongoze akili zako kwa kuipa msukumo toka ndani ya Moyo(Nafsi yako), bila kujari mazingira ya nje yanasema nini, fuata roho yako inasema nini. Usifanye maamuzi sawa na akili yako.

instagram.com

Instagram post by Umoja wa Vijana wa Kikristo Tz • Jul 31, 2017 at 9:57am UTC

KIJANA ULIYE MBEYA NA MIKOA JIRANI, NI MWEZI WETU, KUMBUKA NI WAKATI WETU HUU, KARIBU KKKT… https://t.co/R8vTaBFf2w

instagram.com 0 Likes, 1 Comments - Umoja wa Vijana wa Kikristo Tz (@umoja.wa.vijana.wa.kikristo.tz) on Instagram: “KIJANA ULIYE MBEYA NA MIKOA JIRANI, NI MWEZI WETU, KUMBUKA NI WAKATI WETU HUU, KARIBU KKKT…”

KIJANA ULIYE MBEYA NA MIKOA JIRANI, NI MWEZI WETU, KUMBUKA NI WAKATI WETU HUU, KARIBU KKKT BATHEL,(SAE), KARIBU NA TANESCO. USIACHE HII IPITE.

Hello vijana mlio mbeya na mikoa mingine mnafikkri tunafanya nini kwa mwaka huu kwaajili kongamano la kusifu na kuabudu La Umoja wa vijana wa Kikristo Tanzania THE VOICE OF VICTORY (VOV) SESON 6 kwa mkoa wa Mbeya.

Nasi tulio mikoa Mingine tunawaza nini kwaajili ya kuwafikia vijana wote wa kikristo, Nakufanyika baraka kwao.

Tulio Mwanza tunatarajia kufanya mwezi wa kumi. Na tutaanza kukutana hivi punde.
TUFANYE KWAAJILI YA KRISTO NA KWAAJILI YA VIJANA KUMTUMIKIA MUNGU NA KUJITAMBUA HASA.

[06/18/17]   KARIBU TEMBELEA UKURASA HUU, KWAAJILI YA KUWA NA UMOJA KATIKA KRISTO YESU

CHUKUA DAKIKA ZAKO KADHAA TU KUSOMA SOMO HILI NA KUIPITIA PAGE HII #UmojawavijanawaKikristotanzania ILI UPATE MUENDELEZO WA SOMO HILI LAWEZA KUSAIDIA WEWE NA WENGINE WALIO OA AU OLEWA AU WALIO NA MAONO YA KUOA NA KUOLEWA
"Barikiwa Sana"

HALISIA WA MAISHA YA NDOA NA VIKWAZO VYAKE.
MUENDELEZO WA SEHEMU YA TATU

Tunaomba radhi kwa wale wanaoliokuwa wanafatilia somo hili kuhusu Uhalisia wa maisha ya ndoa na vikwazo vyake, kwa kuwa kimya kwa muda mrefu.
karibu tutazame muendelelezo wa sehemu ya tatu kwa kuendelea kutazama Swali hili

1. KWANINI HAYO MAMBO MAGUMU YANATOKEA WAKATI WA NDOA.
Inaendelea kutoka sehemu ya Tatu

Fahamu wakati wa uchumba kinacho tumika zaidi kushikilia uhusiano ni upendo lakini wakati wa ndoa nguvu ya upendo ikipungua madhaifu huanza kuoneka hivyo kinacho shika ndoa ni upendo ulishikwa na msimamo na heshima ndani ya wajibu.
Waefeso 5:25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Ikiwa hakuna msimamo na ufuatiliaji wa dhati katika mipango na maamuzi yenu basi fahamu utaanza kuona ugumu wa ndoa hasa pale mwenzi wako anapo kuuliza na kukufuatilia au hata kufoka au kusema mbona wenzio hufanya hivi au vile(wanaume wengi hukasirika) na wengi huona wenzi wao hawawaelewi. Ikiwa mawazo yenu kwa asilimia kubwa yanatazama mambo yaliyo nje basi fahamu mtaona ugumu wa ndoa. Kwasababu hamtaelewana katika maamuzi na mtasahau uzuri wa uchumba. mambo mengi ya nje huwa ni vionjo lakini kinacho jenga ndoa ni mambo yaliyo ya msingi na yenye malengo kwa familia.

Wafilipi 2:2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.

Ikiwa msimamo wa mmoja wenu ukawa tofauti na ahadi ya ndoa na akafanya tofauti na vile ambavyo mwingine alitegemea basi fahamu uwaminifu hupotea na heshima huondoka upendo huwa mashaka na maumivu kwasababu kile kilicho tegemewa na moyo hakija patikana au kimepatikana katika hali ya wasiwasi na kupelekea upande mmoja kupoteza furaha ya ndoa na amani ya mwenzi. Mara nyingi hapa imani na uwaminifu hupotea, hofu hutawala zaidi ya upendo, kutenda kwa mashaka hutawala maisha upande mmoja wenye kosa. ama kutenda ili kumridhisha mwenzi wako na kutenda huku huwa ahakuzai matunda chanya waweza onekana waigiza

1 Wakorintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

Kumuacha mume sio kuondoka nyumbani au kuvunja ndoa wala kuomba talaka, ila kumtoa mume wako katika nafasi ile ambayo ulikuwa umempa kwanza na kuweka udhaifu au makosa yake zaidi ya ule uzuri ulio kufanya uvutiwe na kuolewa naye. hii husabisha vifo vya ndoa nyingi au kutoona hata mwelekeo wa maisha ya familia yako

Itaendelea.......

Tukutane wakati mwingine tuendelee kutazama ukweli katika ndoa!!
By (THE VOICE OF VICTORY)®.
© Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania
#umojawavijawakikristotanzania
#vijanawakikristotanzania

HALISIA WA MAISHA YA NDOA NA VIKWAZO VYAKE.
MUENDELEZO WA SEHEMU YA TATU

Tunaomba radhi kwa wale wanaoliokuwa wanafatilia somo hili kuhusu Uhalisia wa maisha ya ndoa na vikwazo vyake, kwa kuwa kimya kwa muda mrefu.
karibu tutazame muendelelezo wa sehemu ya tatu kwa kuendelea kutazama Swali hili

1. KWANINI HAYO MAMBO MAGUMU YANATOKEA WAKATI WA NDOA.
Inaendelea kutoka sehemu ya Tatu

Fahamu wakati wa uchumba kinacho tumika zaidi kushikilia uhusiano ni upendo lakini wakati wa ndoa nguvu ya upendo ikipungua madhaifu huanza kuoneka hivyo kinacho shika ndoa ni upendo ulishikwa na msimamo na heshima ndani ya wajibu.
Waefeso 5:25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Ikiwa hakuna msimamo na ufuatiliaji wa dhati katika mipango na maamuzi yenu basi fahamu utaanza kuona ugumu wa ndoa hasa pale mwenzi wako anapo kuuliza na kukufuatilia au hata kufoka au kusema mbona wenzio hufanya hivi au vile(wanaume wengi hukasirika) na wengi huona wenzi wao hawawaelewi. Ikiwa mawazo yenu kwa asilimia kubwa yanatazama mambo yaliyo nje basi fahamu mtaona ugumu wa ndoa. Kwasababu hamtaelewana katika maamuzi na mtasahau uzuri wa uchumba. mambo mengi ya nje huwa ni vionjo lakini kinacho jenga ndoa ni mambo yaliyo ya msingi na yenye malengo kwa familia.

Wafilipi 2:2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.

Ikiwa msimamo wa mmoja wenu ukawa tofauti na ahadi ya ndoa na akafanya tofauti na vile ambavyo mwingine alitegemea basi fahamu uwaminifu hupotea na heshima huondoka upendo huwa mashaka na maumivu kwasababu kile kilicho tegemewa na moyo hakija patikana au kimepatikana katika hali ya wasiwasi na kupelekea upande mmoja kupoteza furaha ya ndoa na amani ya mwenzi. Mara nyingi hapa imani na uwaminifu hupotea, hofu hutawala zaidi ya upendo, kutenda kwa mashaka hutawala maisha upande mmoja wenye kosa. ama kutenda ili kumridhisha mwenzi wako na kutenda huku huwa ahakuzai matunda chanya waweza onekana waigiza

1 Wakorintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

Kumuacha mume sio kuondoka nyumbani au kuvunja ndoa wala kuomba talaka, ila kumtoa mume wako katika nafasi ile ambayo ulikuwa umempa kwanza na kuweka udhaifu au makosa yake zaidi ya ule uzuri ulio kufanya uvutiwe na kuolewa naye. hii husabisha vifo vya ndoa nyingi au kutoona hata mwelekeo wa maisha ya familia yako

Itaendelea.......

Tukutane wakati mwingine tuendelee kutazama ukweli katika ndoa!!
By (THE VOICE OF VICTORY)®.
© Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania
#umojawavijawakikristotanzania
#vijanawakikristotanzania

KIJANA ULIYEPO MOROGORO KARIBU KWENYE HUU MKESHA.. USIKOSE

Bwana Asifiwe
Tuna kila sababu ya kumshukuru na Mungu kwaajili ya kutupa nafasi ya kufanikisha kufanya Kongamano la vijana Mkoa wa Mwanza CHANGING YOUTH CHANGING NATION (CYCN)
Pia Tunayo Heshima ya pekee na shukurani za pekee kwako kwa ushiriki wako wa kila namna; kwa kutuombea, kuhudhuria, kutuwazia, kutushauri na kutupa mkono wa shirika kwa sadaka yako. Ni maombi yetu kuwa Mungu akubariki sana na kukufanikisha
PIA USIACHE KUTUMIKA PAMOJA NASI TENA TUTAKAPO KUHITAJI.
"Tunakupenda sana"
UNAHITAJI KUTUMIKA PAMOJA NASI 0762060506 AU TUMA KWA WALL YA HII TUMA SMS JINA NA MAHALI ILIPO.

Karibu kesho pale AICT MAKONGORO MISSION MWANZA Tutakuwa na Semina ya Vijana na Mwl Tuntufye Mwakyembe CHANGING YOUTH CHANGING NATION(CYCN)
WEWE NI MUHIMU SANA KUWEPO MKARIBISHE NA MWINGINE. USIKOSE!!!!

MWANZA!! YES NI MWANZA.. KIJANA ULIYE NA MAONO, MALENGO NA NIA YA KUFANIKIWA USIKOSE KATIKA HILI KONGAMANO LA VIJANA. SISI WOTE TULIO MWANZA TUTAKUWEPO!!!

HALISIA WA MAISHA YA NDOA.

SEHEMU YA TATU

1. KWANINI HAYO MAMBO MAGUMU YANATOKEA WAKATI WA NDOA.

Fahamu kuwa ndoa ndio ngome kuu ya kufanikiwa na heshima na hakuna mwenye heshima kamilifu na kibari chema kama mtu aliye fanikiwa katika ndoa na maisha ya kawaida.

Jibu ni kwamba kuna tofautikubwa kati ya maisha ya ndoa na maisha ya uchumba, kuna tofauti kati ya majukumu wakati wa uchumba na wakati wa ndoa na kuna tofauti kati ya uwepo wa wachumba na uwepo wa wanandoa.

Pia kuna tofauti kati ya urafiki wa wachumba na urafiki wa wana ndoa, pia ni tofauti kubwa ukaribu wa wanandoa na ukaribu wa wachumba na kuna tofauti kubwa kati ya uhitaji wa mwenzi wakati wa uchumba na uhitaji wa mwenzi wakati wa ndoa.

Ili usikutane na ugumu unahitaji kubadilika kutoka kwenye uchumba hadi kwenye ndoa. Pia fahamu kuna tofauti kubwa katika mitazamo ya uchumba na mitazamo wakati wa ndoa.

Mathayo19:6-10“Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa”

Basi fahamu ndoa ni agano la ajabu sana, huwezi kuwa huru kama ushaoa na wala sio swala la kujifariji kuwa ndao ni jambo la kawaida. Linahitaji wepesi wa Moyo na kutambua kwa haraka sana kuwa hakuna mkamilifu kama mwenzi wako.

Hata kama unaona mapungufu au kubadilika kwa tabia. Fahamju ukimwacha mwenzi wako kwasabu ya upungufu basi wafanya kosa juu yako mwenyewe na hautakuwa huru kamwe, kumbuka kwa kosa la Hawa adamu hakuwa huru hadi kaburini na kwa kosa la hawa adamu aliadhibiwa, kosa halikuwa kwanini mkeo kakuletea tunda ila kwanini umekula tunda, sio kwanini mke wakakokosea. Watu wengi hutumia udhaifu wa wake zao au wenzi wao kuwa ni chanzo cha wao kufanya makosa.

Itaendelea.......

Tukutane wakati mwingine tuendelee kutazama ukweli katika ndoa!!

By (THE VOICE OF VICTORY)®.

© Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania
#umojawavijawakikristotanzania
#vijanawakikristotanzania

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

UHALISIA WA MAISHA YA NDOA.

MUENDELEZO WA SEHEMU YA PILI:

MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KABLA NA BAADA YA NDOA
Tuendelee na sehmu ya pili kama vile tulivyoona katika sehemu iliyopita kwa kutazama mambo matatu muhimu ya kufahamu kuhusu ndoa, basi tuendelee kutazama mambo mengine sawa vile Mungu anatupa kibari. "karibu"

4. Katika ndoa yako unataka uishi kama nani? Mke au Mume, mtawala au mtawaliwa, wengi huishi katika ndoa katika mfumo wa aina mbili, mtawala na mtawaliwa, na kusahau kuwa ndoa sio swala la kutawala na kutawaliwa au kufanya maamuzi na wenngine watekeleze au utumikiwe na mwenzi wako. Wengi hugawanya majukumu katika mfumo wa hili ni la baba au mama na kusahau kuwa hakuna mgawanyo wa majukuimu ndani ya ndoa ila mipango na makubaliano na utekelezaji na katika utekelezaji ndipo huja swala la majukumu ya wana ndoa. Kumbuka mwanaume na mwana mke wote waliumbwa siku moja na kupewa jukumu moja, ila walitofatiana siku za kuonekana katika Mwili " fahamu hakuna kufanana katika mfumo wa ndoa, usitake uishi kama ndoa ya fulani bali tambua ndoa huwa vile wewe na mwenzi wako mnaamua kuishi, ukiona ndani ya ndoa kila mtu anaishi anavyotaka au mmoja anajiona ni bora kuliko mwenzie basi elewa kuna tatizo katika hiyo ndoa"

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”(Mwanzo 1:27,28 )

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.( Mwanzo 2:7,8 ; 24-25).) utagundua kuwa Mungu aliumba wote siku moja na kuwapa jukumu moja.Ila walitofautiana siku ya kuoneka katika Mwili.

5. Nini msingi wa ndoa yako au naweza sema nini muhimili wa ndoa yako, kabla ya kuingia katika ndoa uhusiano wenu mliujenga katika nini, kama pesa ndiyo muhimili mkuu wa ndoa yenu basi fahamu siku hiyo pesa ikakosekana kuna hatari ya ndoa kuvunjika, na kama muhimili wenu ni vitu vya nje kwa maana ya muonekano wa uzuri wa sura na maumbo basi fahamu siku mmoja wenu akapoteza ule uzuri basi ndoa iko katika hatari, ikiwa ni maisha Fulani ya raha au kuwa vitu vya thamni ndio yamekusabiasha uwe na hiyo ndoa basi siku hayo maisha yakakosekana lazima uone ndoa ngumu. Kama ni swala uwaminifu ndio linakufanya uoe au kuolewa na huyo basi fahamu siku akikosea nje ya ule uwaminifu na vile ulivyo tegemea basi ni rahisi kuivunja hiyo ndoa.

6. Ni siri gani umemficha mwenzi wako au ni jambo gani mwenzi wako anajua kuhusu wewe na misimamo yako halisi ni ipi na sio ile ambayo imefichwa katika upendo na unahitaji wa kuwa naye kwa faida unazo zitazama kwa wakati huo, ni kitu gani unajua kuwa hakipo sawa kwako na unadhani ukimwambia atakuacha au ukimwambia kitakupunguzia heshima au kitu gani kinatia mashaka na unaogopa mwenzi wako akijua kitaleta shida au hata kuvunjika kwa mahusino yenu. Fahamu ni vema kumwambia ukweli mwenzi wako hata kabala hujaingia katika ndoa kwa sababu akijua akiwa ndani ya ndoa ni tatizo kubwa zaidi ya vile ambavyo ungemwambia mapema na imani juu yako hufa na kupotea kama sio kabisa basi ataishi kwa masha na wewe, “hakuna maumivu mabaya kama hayo”

7.Fahamu ndoa ni maisha ya milele kifo ndio kinacho watenganisha nje ya hapo ni kuamua kuvunja agano jambo ambaloo husababisha vifungo na laana na kutofanikiwa, majeraha na uchungu. hata kama ulikosea mtu wa kuingia naye katika ndoa haibadilishi uhalisia wako kuwa ni mwana ndoa kinacho takiwa ni kuhakikisha unakuwa na ndoa sahihi na yenye mafanikio na matunda ya fuaraha na upendo bila kujali mapungufu uliyo yaona kwa mwenzi wako. Pia fahamu upendo unatengenezwa na kujengwa ujapo potea hutafutwa, ujapo kosewa hurekebishwa na ujapo kasirika hutatunzwa salama kusubiri siku ya furaha.

Itaendelea..........

Tukutane wakati mwingine tuendelee kutazama ukweli katika ndoa!!
By (THE VOICE OF VICTORY)®.
© Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania

#vijanawakikristotanzania
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
NB: TUENDELEE KUJIULIZA HAYA MASWALI
ii). JE MTU HUBADILIKA BAADA YA KUOA AU KUOLEWA
iii). KWANINI YATOKEE BAADA YA KUOLEWA
iv). JE NI KWELI UMEKOSEA KUOA AU KUOLEWA
v). JE NI KWELI MWENZI WAKO HAKUPENDI
Ndoa ni mwili moja: Ikiwa ni mwili mmoja unapaswa kuulisha, kuujali, na kuutunza kama vile unavyo fanya kwako mwenyewe, unapaswa kufanya zaidi kwa mwenzi wako.
Mwanzo 2:23 “Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.”

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Migori?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Location

Telephone

Address


Mbeya
Mwanza
DODOMA, DAR-ES-SALAAM
Other Religious Organizations in Mwanza (show all)
Melkizedeki Hope International Melkizedeki Hope International
Plot No. 114 Block "B" Nyakato National, P.O. Box 1844
Mwanza, 25528

We support orphans and offer access to basic needs to the poor. Please give food, clothes, shoes, bedding or education to the needy.

ECG Church Mwanza Branch ECG Church Mwanza Branch
Pasiansi
Mwanza

This is the official page of Enlightened Christian Gathering church (ECG) MWANZA TANZANIA

ELVD - ELCT ELVD - ELCT
P.O. Box 423
Mwanza

East of Lake Victoria Diocese (ELVD) is part of the Lutheran Church in Tanzania (ELCT). Our home base is Mwanza, next to Lake Victoria.

Sports Gospel Ministry Sports Gospel Ministry
Tanzania
Mwanza

We are a Christian Sports organization empowering Young people to follow Jesus and learn Gods Kingdom through Sports Evangelism.

Confirmed Development & Relief Mission Confirmed Development & Relief Mission
Post Rd, Diocese Of Victoria Nyanza Offices
Mwanza, P.O.BOX 2983, MWANZA, TANZANIA

Community Development & Relief Mission

FPCT-Kitangiri FPCT-Kitangiri
83
Mwanza

Ratiba ya ibada Jumapili 07:30 -10:00 Asubuhi. Ibada kwa watu wote. 10:30 - 13:00 Asubuhi. Ibada kwa watu wote. 08:00 asubuhi. shule ya Jumapili ya watoto.

UHURU UHURU
ISAMILO
Mwanza

Uhuru wa mawazo fikra.kira mtu ana uhuru wa point ispokuwa usiende kinyume na sheri.

New Vine Church New Vine Church
Gloryland,Nyanembe-Buhongwa
Mwanza, +255

NVC is a Church committed to see the raising of great Godly generation with the aim of making impact, changing lives and influence the World.

Lumala Seventh-Day Adventist Church Lumala Seventh-Day Adventist Church
Lumala
Mwanza, 1724

Tumeitwa kuwa wajumbe wa Mungu duniani. Karibu tumwabudu na kumtumikia Mungu kwa kicho.

Nyakato Seventh Day Adventist Church Mwanza Tanzania. Nyakato Seventh Day Adventist Church Mwanza Tanzania.
Nyakato - Mwanza, Tanzania
Mwanza

About   Contact   Privacy   Login C